2018-01-02 08:47:00

Papa:Mama wa Mungu ndiyo sifa muhimu ya Maria na Kanisa linathibitisha!


Mwaka unafunguliwa na jina la Mama, Mama wa Mungu ndiyo sifa muhimu zaidi ya Mama. Lakini inawezekana kujiulizwa swali juu yake kwamba, je kwa nini tunasema Mama wa Mungu na siyo mama wa Yesu? Siku zilizopita wengi walijiuliza swali hilo, lakini Kanisa linathibitisha kuwa ni Maria na Mama wa Mungu. Hayo ni maneno aliyo anza nayo Baba Mtakatifu Francisko katika mahubiri yake katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Mjini Vatican, wakati mama Kanisa anaadhimisha Sikukuu ya Mama Maria Mama wa Mungu tarehe 1 Januari 2018 inayokwenda sambamba na siku ya Amani duniani.

Baba Mtakatifu ameendelea na mahubiri yake kuwa, tunapaswa kushukuru kwasababu ya maneno hayo kwani yanafungamana na ukweli unao angaza juu ya Mungu na juu yetu. Hiyo ina maana tangu Bwana alipojifanya mtu ndani ya umbu la Maria, ikawa tangu wakati huo na daima, anachukua ubinadamu wetu ambao umejipachika kwake. Hakuna Mungu tena bila binadamu. Yesu anatwaliwa katika mwili na pia mama Maria ni mwili wake, hata sasa na daima. Kusema Mama wa Mungu ina maana ya kutukumbusha hili kuwa, Mungu yuko karibu na binadamu kama mtoto na mama yake anayembebwa katika umbu lake.

Ameendelea na ufafanuzi kuwa, meno mama (Mater), linatukumbusha hata neno kitu. Katika umama wake, yupo Mungu wa mbingu, ambaye ni Mungu milele aliyejifanya mdogo, akajifanya kitu na si tu kwa ajili ya kukaa nasi, bali hata kujifanya kuwa kama sisi. Baba Mtakatifu anathibitisha kuwa, hiyo ndiyo miujiza, hiyo ndiyo habari yenyewe, kwa maana binadamu si peke yake tena wala si yatima, bali ataitwa mwana daima.
Mwaka unafunguliwa na habari hiyo mpya, Baba Mtakatifu anathibitisha! Na hata sisi tunaitangaza hivyo tukisema, Mama wa Mungu! Ndiyo furaha ya kuja kwakei hiyo inaonesha kuwa katika upweke wetu umeshinda. Ni uzuri wa kutambua kuwa hata sisi ni wana tunaopendwa, ni vizuri kutambua kuwa utu wetu hautatolewa kamwe.

Na kwa maana hiyo, Baba Mtakatifu anasisitiza, ni lazima kutazama Mungu aliye mdhaifu na mtoto katika mikono ya Mama, pia kutazama ya kwamba ubinadamu wetu ni upendo na utakatifu katika Bwana. Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu ametibitisha, kuhudumia maisha ya binadamu ni kuhudumia Mungu na kila maisha. Hiyo inatoka katika kiini, ndani ya umbu la Mama hadi kufikia uzee, mateso na mgonjwa, hadi kufikia maisha yale yanayotia kinyaa, lakini yote hayo yanapaswa kupokelewa, kupendwa nakusaidiwa.

Akiendelea na ufafanuzi wa  Injili ya Siku amesema, tuache tuongozwe na Injili hiyo. Kwa upande wa mama Injili inaeleza kuwa Yeye alikuwa akiyaweka yote hayo na kuyatafari katika moyo wake (Lk2,19). Kuyaweka kwa maana  rahisi alikuwa akitunza. Maria hakuwa anaongea. Hiyo inathibitika kutokana na kwamba Injili  hatoi neno lolote la Maria katika  Siku ya Kuzaliwa kwa Bwana. Hivyo Mama Maria anaungana na Mwanae.Yesu ni mwana, maana yake asiye kuwa na neno. Yeye ni Neno lililofanyika mwili, Neno la Mungu ambaye mara nyingi kwa namna nyingi kwa njia ya manabii alisema (Eb 1,1) na sasa ni kimya. Wakati maalumu ulipotimia (Gal,4,4) ni kimya. Mungu anayekuwa kimya ni mtoto ambaye haongei. Ukuu wake hauna maneno, fumbo lake la upendo linajionesha katika udogo. Udogo huo wa ukimya ni lugha ya ukuu wake. Mama anaungana na Mwanae na kuyaweka yote katika ukimya.

Ukimya huo, Baba Mtakatifu anasisitiza kuwa, hata sisi iwapo tunataka kuyaweka na kutunza, tunahitaji ukimya. Tunahitaji kubaki kimya kwa kutazama pango. Kwasababu mbele ya pango tunaweza kugundua jinsi gani tunavyopendwa, na kuonja maana nzuri ya maisha. Kutazama kwa ukimya na kuacha Yesu aongee katika mioyo ina maana ya kwamba, udogo wake unaondoa kila aina ya viburi vyetu; umaskini wetu unapata kusumbua haraka zetu na huruma yake inatingisha mioyo yetu migumu isiyo na huruma. Kutafuta muda kwa siku katika ukimya na kuwa na Mungu ni kutunza roho zetu; ni kutunza uhuru wetu dhidi ya matumizi mabaya na kelele nyingi za matangazo ya hapa na pale; inazuia kusambaza maneno matupu na mawimbi mengi yanayosabambaa katika masengenyo na uchochezi.

Injili inaendelea kueleza kuwa, Maria alikuwa akiyaweka maneno hayo na kuyatafakari: Je yalikuwa ni mambo gani hayo? Baba Mtakatifu anafafanua : yalikuwa ni furaha na uchungu: kwa upande mmoja ni kuzaliwa kwa Bwana; upendo wa Yosef una kutembelewa na wachungaji katika usiku ule wa mwanga. Na kwa upande mwingine anafafanua kuwa ni maisha endelevu yasiyo na uhakika, ukosefu wa nyumba, kwasababu hapakuwapo na nafasi katika nyumba ya wageni (Lk 2,7); upweke wa kubaguliwa ambao unajikita katika masikitiko ya kuona Yesu anazaliwa katika holi la ng’ombe. Baba Mtakatifui anaonesha kwamba, matumani na uchungu, mwanga na giza ni mambo yote hayo yanayojikita katika kina cha moyo wa Maria. Na yeye alifanya nini? Jibu lake ni kwamba, aliyatafakari! maana yake aliyapokea katika moyo wake na kuyakabidhi kwa Mungu.

Yeye hakuficha lolote ili kutunza kwa ajili yake yake tu, hakubaki katika upekwe au kusongwa na uchungu, yote alimkabidhi Mungu. Ndiyo hivyo alivyo yatunza kwa maana ya kuamini katika kutunza. Hakuacha kusongwa na mawazo na katika mtego wa hofu au kukata tamaa, au kukimbilia katika ushirikina, hakujifunga yeye binafsi au kutafuta kusahau: alifanya jitihada ya kila njia na kujiweka katika mazungumzo na Mungu. Mungu ambaye anatupenda kwa moyo wote hadi kuja kuishi nasi katika maisha yetu. Hiyo ndiyo siri ya mama wa Mungu! Baba Mtakatifu anabainisha, ni kuyaweka katika moyo na kupeleka kwa Mungu. Injili inahitimisha: yote alikuwa akiyaweka katika moyo wake. Kwa namna hiyo, moyo unatualika kutazama kiini cha binadamu, katika upendo na katika maisha. Hata sisi wakristo katika safari, tunapoanza mwaka mpya lazima tuhisi haja ya kuanzia katika kiini, na kuacha nyuma mizigo mizito iliyopita kwa kuanza kujikita katika kile kinachohesabika.

Leo hii mbele yetu tunayo sehemu ya kunzia, maana tunaye mama, hivyo ni kuanzia kwa Mama wa Mungu! Baba Mtakatifu anaongeza, Maria ni kama Mungu anavyopenda nasi tuwe; kama anavyopenda Kanisa liwe, yaani ukarimu, maskini wa vitu na mwenye utajiri wa upendo, uhuru wa kupinga dhambi, anayeungana na Yesu,anayetunza Mungu katika moyo na jirani katika maisha. Ili kuanza safari hiyo hatuna budi kutazama Maria. Katika moyo wake unaodunda moyo wa Kanisa. Ili tuweze kwenda mbele, sikukuu ya leo inahitaji kutazama nyuma tukianzia katika pango, kuanzia kwa Mama ambaye amempakata Mungu mikononi mwake.

Baba Mtakatifu anafafanua kwamba, ibada ya Maria siyo sheria ya kiroho, ni mahitaji ya maisha ya kikristo. Kwa kumtazama Maria, tunatiwa moyo kuacha mambo mengi yasiyo na maana na kupata yale yaliyo msingi. Zawadi ya Maria, zawadi ya kila mama na kila mwanamke ni yenye thamani kubwa kwa ajili ya Kanisa ambalo ni mama na mwanamke. Kama mwanaume anakiuka, yeye anahimiza kwa mawazo, mwanamke na mama anatambua kuyaweka, yeye anaunganisha katika moyo na kufanya kuwa hai. Ili kutopoteza sifa ya mawazo au mafundisho katika imani, tunahitaji wote kuwa na moyo kama wa mama, kutambua kutunza kwa huruma ya Mungu na kusikiliza mapigo ya moyo wa binadamu. Mama ni muhuri wa Mungu katika binadamu. Mama Maria alinde Mwaka huu, ili kuweza kufikia amani katika mioyo na katika ulimwengu itokayo kwa mwanae Yesu Kristo.

Na kama watoto, Baba Mtakatifu Francisko akihitimisha mahubiri yake, amewaalika waumini wote kumsalimia  Mama leo hii  na  sala ya wakristo wa Efeso mbele ya maaskofu wao, mara tatu  kwa moyo wote na kumtazama kwa kutamka kwamba  “Mtakatifu Mama wa Mungu.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News








All the contents on this site are copyrighted ©.