2017-12-27 14:28:00

Noeli ni siku ya Kuzaliwa Yesu Kristo, Mwana wa Mungu na Bwana wa historia!


Noeli ni siku ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo Mwana wa Mungu na Bwana wa historia. Iwapo dunia inatazama kutoa majina mengine kwa siku hiyo Takatifu, kuijaza au kwa namna nyingine ya kuipamba na mwanga na rangi za mambo mengi ya sikukuu, ukweli wa kikristo unabaki pale pale kama ulivyo tangazwa na kubaki kwa waamini wa imani katika dunia.

Hayo ni maneno katika mahubiri ya Kardinali Angelo Bagnasco, Askofu Mkuu wa Genova, na Mwenyekiti wa Baraza la Mabaraza ya Maaskofu Ulaya katika aliyota katika misa ya Kuzaliwa kwa Bwana, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Lorenzo Genova Italia. Kardinali Bagnasco anasema, Noeli inatufanya kutafakari fumbo la maisha, zawadi ambayo Mungu anaweka katika mikono yetu, si kama kusimamia, bali kama mlinzi. Lakini anasema, kwa upande mmoja, ipo tabia ya kutaka kuwa na maisha mapya kwa gharama zozote na kwa upande mwingine wa kutaka kuharibu maisha ya binadamu. Na katika tabia hizo, moja au nyingine, ipo  kasumba ya kutaka pia kuwa wasimamizi tu  na si kama walinzi wa kutetea maisha. Hiyo ndiyo inaitwa ubinafsi wa kweli ambao si wa mshikamano binafsi na wala  wa pamoja.

Kinyume na hiyo Kardinali Bagnasco amesema, jamii ya kibinadamu ni ya kweli iwapo inajikita hawali ya yote kwa ajili kutetea wadhaifu ambao ni watoto, wazee, wagonjwa; pamoja na kwamba yapo mawazo ya kisasa katika mantiki ya uchumi na ukosefu wa upendo ambao daima inazidi kuongezeka na kutawala hali ya umimi badala ya sisi. Kardinali Bagnasco pia amekumbuka kuwa familia ya sasa iko chini ya shambulio la utamaduni ambao unataka kuiharibu hasa kuondokana na vifungo ambavyo vinaonekana katika mfululizo wa utaratibu wa siku na majukumu ambayo ni vigumu kuyabeba, badala ya kufanya muundo unaounga mkono wa kuleta unafuu wa kuishi.

Kwa njia hiyo anawashauri waamini wapambane na mizizi hiyo inayotaka kuharibu familia na ili isitenguliwe kama Mungu alivyoiumba, na kama uzoefu wa dunia unavyoitambua maana ya familia. Kwa maana msimamo wake hutoa utulivu imara, ukomavu na kuunda jamii inayoaminika.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News

 








All the contents on this site are copyrighted ©.