2017-12-26 07:00:00

Papa Francisko: Jengeni kesho inayofumbatwa katika udugu na mshikamano


Baba Mtakatifu Francisko akiwa ameambatana na Kardinali Leonardo Sandri, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki pamoja na Kardinali Prosper Grech, Jaalim mstaafu wa vyuo kadhaa vya Kipapa mjini Roma, aliyebahatika kutoa tafakari elekezi kwa Baraza la Makardinali kunako tarehe 12 Machi 2013, alitoa baraka za Sherehe ya Noeli kwa waamini na mahujaji waliokuwa wamefurika kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, Sherehe ya Noeli 2017.

Kwa namna ya pekee, Baba Mtakatifu Francisko amewakumbuka na kuwaombea waamini na watu wote wenye mapenzi mema, waliokuwa wanafuatilia ujumbe wa “Urbi et Orbi” kwa njia mbali mbali za mawasiliano ya jamii kwa kuwatakia heri na baraka ya Sherehe ya Noeli. Kuzaliwa kwa Kristo Yesu, Mkombozi wa ulimwengu, kuleta upya katika nyoyo za watu, ili kuamsha tena kiu ya kujenga kesho bora zaidi inayofumbatwa katika udugu na mshikamano; ili kudumisha furaha na matumaini! Amehitimisha ujumbe huu kwa kuwatakia wote Noeli Njema!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Vatican News.
All the contents on this site are copyrighted ©.