2017-12-26 15:16:00

Nchi Takatifu:Wadogo lakini walio wazi na kukaribisha,hiyo ndiyo Noeli


Wadogo ndiyo lakini walio wazi, wachache ndiyo lakini wanaokaribisha , maskini ndiyo lakini wakarimu katika kushirikisha kile tulicho nacho ili kuishi na  watu ndiyo lakini ambao kweli ni wana wa Mungu; hiyo ndiyo Noeli! Ni maneno ya Msimamizi wa Kutume katika Upatriaki wa Yerusalem Askofu Mkuu Pierbattista Pizzaballa wakati wa mahubiri yake katika misa ya asubuhi  ya Noeli  tarehe 25 Desemba 2017 huko Betlehemu.

Askofu Mkuu anakumbusha kuwa,Noeli ni sikukuu ya kukutana na Mungu na binadamu, mbingu na dunia, umilele na wakati; kwa njia hiyo umilele usioisha na unaoisha ambavyo vinakumbatiana na kuungana bila kuchanganyikana, na hata kuachana , kama vile itokeavyo kwa yale makutano yaliyofanikiwa.
Neno la Mungu alifanyika mtoto, lakini mtoto huyo alikuwa ni Neno la milele katika binadamu. Inatosha kutamka hilo neno  ili kuhepukana na hatari ya kupunguza kiurahisi fumbo la Noeli, kwa maana ya kuwa mbali na neema hiyo, ambayo inatokana na  hisia ndogo zisizo na thamani na zilizojaa utupu. Na ndiyo maana inasikika kila Liturujia inayo adhimishwa katika maeneo matakatifu.  Ni heshima na furaha ya kuweza hatmaye kugeuza itikadi zinafungamana na chuki lisilo kuwa nasababu, au kujidai au ukiburi ambao unataka kuondoa au kuwaua wengine.

Halikadhalika ameendelea kueleza kuwa, kuta za nje zisizo za haki, ambazo zinafanya watu wateseke, zinaweza kugeuka  kuwa kuta ndani ya binadamu na kugeuka kuwa vizingiti na tabia za vikwazo dhidi ya kuwakaribisha wengine. Askofu Mkuu ameendelea kusema kwamba, iwapo usiku walitafakari mbele ya holi la ng’ombe na kumpokea binadamu katika sikukuu hiyo ya Noeli, asubuhi waamshe mioyo yao kwa msaada wa Injili ya Mtakatif Yohane mahalia ambapo Noeli inataka kuwapeleka juu ya utukufu wa Mungu aliyejionesha katika nchi. Na ukuu wa Yesu unathibitishwa  kuwa upo katika kuuishi na kuugeuza ukawa zawadi na siyo ubinafsi.

Sisi sote tutakuwa tumekombolewa  amesema, lakini, iwapo uzalendo huo utageuka kuwa zawadi na sio ubinafsi, na iwapo tutabadilishana na  wengine zawadi na msamaha ambao unatufanya tuwe ndugu na sio kuonana kama adui katika ardhi ambayo kabla ya kuwa yetu ni ya Bwana. 
Yote hayo yanathibitishwa ameongeza, na maelfu na maelfu ya mahujaji ambao kwa neema ya mbingu wamekwenda  wengi na wataendelea kuwepo katika barabara hizo na katika  madhabahu ya Nchi Takatifu  kwa ajili ya kukumbusha hali halisi ya tukio hilo daima!

Kwa kumalizia mahubiri yake amesema, ni jambo gumu kubaki daima kufungua kuwa wazi, pia uwezekano wa zawadi hiyo na hasa katika dunia na katika kipindi ambacho ugaidi wa zamani na mpya unaendelea kuleta ugumu  wa mahusiano kindugu: lakini moja ya mivutano yenye hadhi ya kuishi ni ule  mvuto wa Neoli wenye kuwa na tofauti ya mivutano mingine.Hiyo ni kwasababu, mivutano ambayo ipo katika ulimwengu ni mivutano inayoleta utenganisho, migawanyiko, kuharibu na kuua. Na kinyume chake, mvuto wenye shida na wenye heri ya Noeli unawakusanya wote kwa pamoja, unaunganisha, unajenga na kuishi kwa pamoja.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News

 








All the contents on this site are copyrighted ©.