2017-12-26 14:58:00

Askofu Mkuu Galantino amesema tutazame Noeli kwa macho ya haki!


Maisha ni elimu ndefu ya kukutana na Mungu na wengine, ni safari ndefu inayahitaji kutazama kwa kina  macho na moyo ili kuweza kukutana na kuishi katika ukweli. Ni maandishi yaliyomo katika Gazeti Katoliki la Avvenire ya Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa nchini Italia  Askofu Mkuu  Nunzio Galantino, akiwa anajikita kutazama kwa kina ishara mbalimbali za sikukuu ya Noeli na zaidi kwa kuwazatama watu wanaomzunguka Yesu katika holi la ng’ombe.

Askofu Mkuu Galantino anaandika kuwamba, ili kuwatazama watu hao, inahitiaji mtazamo wa macho ya haki kwa namna ya kushinda zile tabia za kukimbizana kila siku bila kuacha hata ile nafasi ya kukaa na kutafakari kwa mantiki ya utamaduni na umakini. Anayasema hayo akiwa na maana ya kutaka kulinda ishara za kidini kama vile zinazopamba kila aina ya pango au tamasha la nyimbo za asili katika Sikukuu ya kuzaliwa kwa Bwana.

Amesisitiza kuwa, ina maana ya kuweza kujikomboa dhidi ya macho ya mikogo, ambayo inaweza kuruhusu au kuanza kuwa na macho yenye chuki na uhalifu kama vile ya Erode. Katika ufafanuzi huo anaandika kuwa, kipofu kwa kawaida anaona giza hata mahali palipo na mwanga. Na mwenye macho ya kiburi cha moyo, mara nyingi anahisi hatari ya kujiofia binafsi, hata kwa yule mwenye kunyosha mikono yake ya kutaka kumsaidia. Na hakatai kusaidiwa tu, bali hata kuumuumiza yule anayetaka kumsaidia. Na baadaye anajifanya kutoa sababu kwamba amefanya hivyo kwa  ajili ya wema wake, ikiwa ni katika hali ya kutafuta  sababu ya kujitetea kwa lile tendo.  Pamoja na watu wa namna hiyo, katika tukio la historia ya binadamu  lilotukia,  hapakuwapo na watazamaji hata waandishi wa habari. Na kwa bahati nzuri yapo hata macho yenye kutambua tukio hilo, kwa mfano wa mamajusi.

Shauku haina umri na wala haikui katika ardhi yenye fursa. Ili kuweza kukua inahitaji wanaume na wanawakea ambao wanapenda maisha na wanayo hamu na kuwa na ahadi zao, kujikita kila wakati katika safari, anakumbusha Askofu Mkuu Galantino. Aidha anaendelea na mitazamo ya wazee, kwamba kuna hekima ya binadamu ambayo tunajifunza kwa shida kutoka katika vitabu, lakini pamoja na hiyo, ipo hekima nyingine ambayo huwezi kufundishwa kutoka katika vitabu. Na kwa njia hiyo ni ile ya  macho safi ya Malaika  na urahisi wa wachungaji.

Watu wa kwanza walipoleta  habari ya kuzaliwa kwa Yesu, walichagua kuwatangazia  wale wa  mwisho kati ya watu. Askofu Mkuu anatoa onyo hasa  kwa wale ambao wanafanya kazi kidogo au wanafanya kwa ajili yao binafsi,kwamba hawataweza kamwe kuwa na macho rahisi kama ya wachungaji. Kwa maana amesema,unaweza kufanya kazi sana, lakini kwa ajili yako binafsi, ili upate kujulikana , wakushukuru na kukupa sifa. Na iwapo mambo hayo yote yatakosekana, basi kichwani ni mahangaiko ya hapa na pale. 

Kwa kumalizia na watu hao wanaozunguka pango,anatazama sura ya Yosefu, mnyenyekevu na  uwezekano na macho makubwa ya Maria. Amebainisha kuwa maisha yetu ni kile tunacho tafakari. Na sisi ni kile tunachopenda. Na kama ilivyo kwa kila mama, macho makubwa ya Mama Maria yalijionesha kwake Yesu. 

Sr Angela Rwezaula 
Vatican News.

 
All the contents on this site are copyrighted ©.