2017-12-23 09:26:00

Ujumbe wa Papa katika tukio la miaka 800 ya Wafranciskani kusimamia Nchi Takatifu


Katika tukio la Mkutano wa Kimataifa wa siku mbili kwanza Roma na baadaye Asizi kuhusu miaka 800 tangu kuanza kwa Wafransikani kuwa usimamizi wa Nchi Takatifu, Baba Mtakatifu Francisko, ametuma ujumbe kwa washiriki wa Mkutano huo, ujumbe ulio tiwa sahini na Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican. Katika ujumbe huo Baba Mtakatifu anatoa matashi mema ili kwamba, kwa mfano wa Mtakatifu Francisko wa Asizi, urafiki, mshikamano na amani vipate kuenea kila mahali.

Baba Mtakatifu pia katika ujumbe huo anawashukuru kwa walio andaa tukio hilo, watoa mada, na  washiriki wote, kwamba anapendelea kuonesha shukrani hata kwa kauli mbiu iliyochanguliwa kuongoza mkutano huo isemayo “Mazungumzo kati ya tamaduni na dini katika kukuza amani” . Anaongeza kusema kuwa ni muhimu sana hasa katika kipindi nyeti cha maisha ya mji wa Yerusalem, mahali ambapo ni ishara  kwa wote katika amani ya kuishi kati ya watu na dini tofauti.

Pamoja na hayo pia Baba Mtakatifu amehimiza kujikita katika huduma ya kweli katika maisha na hadhi ya mtu, kwa kuzingatia tamaduni tofauti za dini na namna ya kuishi, kama vile utajiri wa kibinadamu na kiroho ambao unapaswa kutambuliwa na kupokelewa kwa heshima kuu.
Taarifa zaidi kutoka Gazeti la Osservatore Romanano zinasema kuwa kati ya mikutano miwili wa kwanza mjini Roma umeandaliwa na Ofisi za Waziri wa Mambo ya nchi za Nje nchini Italia unahusu mtazamo wa dini zilizo chache katika dunia na kuhusu kuheshimu uhuru wa dini, mkutano uliofanyika tarehe 21 Desemba 2017 katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Antonianum Roma, ukiwa na mada ya “Tangu enzi za Mtakatifu Francisko, kufikia Papa Francisko:unabii wa dunia iliyopatana”.

Kati ya watoa mada wakati wa  asubuhi wa mwisho aliyepta nafasi ni  Kardinali Leonardi Sandri, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki. Na jioni nafasi ya kuzungumza alikuwa ni Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Italia na Padre Francesco Patton Msimamizi wa maeneo ya Nchi Takatifu , Balozi wa Israeli nchini Italia na Meya wa mji wa Betelehemu.

Ijumaa tarehe 22 Desemba 2017 katika mji wa Asisi Mkutano umeendelea na mada ya “Ufransiskani katika nchi Takatifu,kutoka asili hadi sasa: Maneno na ishara”, ambapo kipindi cha tafakari ya kwanza kimeanzia katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Francisko huko Asizi ikiwa na mada ya “ Kaburi :Urithi wa utume kindugu”.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.