2017-12-22 09:28:00

Papa ametuma ujumbe wa Video kwa waamini wa Peru:Ninashahuku ya kuwaona!


Baba Mtakatifu Francisko ametuma ujumbe wake mfupi kwa njia ya Video kwa waamini wa Kaskazini mwa nchi ya Peru, mwezi mmoja kabla ya Ziara yake ya Kitume katika Bara la Amerika ya Kusini. Baba Mtakatifu anawasalimia sana waamini wote hasa wa  Kaskazini ambao atakutana nao huko Trujillo tarehe 20 Januari 2018,ambao watafika kukutana naye wakiwa na picha za watakatifu wao wasimamizi pia ya Bikira Maria .

Katika ujumbe huo kwa njia ya Video, Baba Mtakatifu amesema kuwa,anayo shahuku kubwa ya kukutana nao, kusifu na kumshukuru Mungu kwa ajili ya historia ya utakatifu, anaongeza kuthibitisha kuwa nchini Peru, ina watakatifu wengi ! Kadhalika ameonesha salam hizi za dhati kwa wote na kuwabariki na kuwaomba pia wasali kwa ajili yake,na kumwomba Bikira Maria aweze kuwalinda kwa namna ya pekee waamini wote wa nchi ya Peru.

Pamoja na hayo Baraza la Maaskofu nchini Peru (Cep) wametoa Wimbo maalumu ya ziara ya Baba Mtakatifu nchini Peru kwa njia ya Video yenye kauli mbiu “ Tutembee pamoja na Francisco”. Wimbo huo umetungwa na mwana muziki mmoja aitwaye Oscar Quiñones Enciso, na kutafsiriwa na dada yake Elizabeth; wimbo huo umechaguliwa kati ya nyimbo 120 zilizokuwa zimependekezwa katika Baraza la Maaskofu wa Peri ambapo walifanya tukio la tamasha la mashindano ya nyimbo katika Kanisa nchini Peru.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News

 








All the contents on this site are copyrighted ©.