2017-12-20 15:47:00

Papa:Katika Katekesi,Baba Mtakatifu amechambua sehemu za Liturujia


Leo hii ninataka kuingia mbashala katika maadhimisho ya Ekaristi. Mada hii ni mwendelezo wa Katekesi juu ya Misa: Misa imegawanyika katika sehemu kuu mbili: ya kwanza ni liturujia ya Neno na ya pili Liturujia ya Ekaristi,lakini  sehemu hizi zinakwenda sambamba kati yao kwa mtindo mmoja  (taz Sacrosanctum Concilium, 56; Misale Kuu ya  Roma, 28).

Ni utangulizi wa maneno ya Tafakari ya Baba Mtakatifu wakati wa katekesi ya siku ya Jumatano tarehe 20 Desemba 2017, katika Ukumbi wa Mwenye heri Paulo VI mjini Vatican. Katekesi ya leo imeongozwa na Neno la Mungu kutoka katika kitabu cha Matendo ya Mitume 2, 42-48, mahali ambapo inasomeka kuwa, hawa wote waliendelea kujifunza kutoka kwa mitume, kuishi pamoja kindugu, kuumega mkate na kusali……

Hivyo Baba Mtakatifu ameendelea kufafanua zaidi juu ya sehemu za Misa kwamba, imetanguliwa na baadhi ya visehemu vya maandalizi ya liturujia na kuihitimisha na mengine, kwa maana hiyo ni kiungo kimoja cha maadhimisho ambacho hakiwezi kutengenishwa, kwa ulewa bora. Sehemu hizo ni muhimu na kwasababu kila kimoja kina uwezo wa kuhimiza na kuhusisha ukubwa wa ubinadamu wetu. Baba Mtakatifu ameongza, ni lazima kutambua ishara hizi takatifu ili kuweza kuishi kwa kina Misa na ili kuonja uzuri wake wote.

Waamini wanapokutanika, maadhimisho yanafunguliwa na utangulizi ambao ni anayeadhimisha au waadhimishaji,  anaanza kwa salam, “Bwana awe nanyi”, Amani ya Bwana iwe nanyi, sala ya majuto,“ ninakuungamia , mahali ambapo sisi tunaomba msamaha wa dhambi zetu na kufuata, Bwana utuhurumie (Kyrie eleison),  sala ya Utukufu na maombi: haya yanaitwa maombi ya pamoja, si kwamba wanafanya kukusanya sadaka, hapana, ni kufanya maombi ya pamoja, kwa maana ya kukusanya nia za watu wote, na nia hizo ili zipate kwenda mbinguni kama sala moja inayokwenda kwa Mungu.

Lengo la utangulizi huo ni kwamba, waamini wote walio unganika kwa pamoja na  kufanya jumuiya moja, wanakuwa tayari kusikiliza kwa imani Neno la Mungu na kuadhimisha kwa heshima Ekaristi (Taz Misale ya Roma 46). Si jambo jema kuwa na tabia ya kutazama saa: Baba Mtakatifu ametoa mfano kwamba, ”bado nina muda nitafika baada ya utangulizi, kwa maana ninatimiza sheria”. Baba Mtakatifu amesema  si tabia njema ya kutazama muda na kuhesabu! Katika utangulizi wa liturujia, Misa inaanza na ishara ya Msalaba. Kwasababu ni pale inapofanyika tendo la kuabudu kama jumuiya. Na ndiyo maana ni muhimu kufika mapema bila kuchelewa ili unapofika mapema ujiandae katika moyo kwenye utangulizi huo wa maadhimisho ya liturujia katika jumuiya.

Wakati wimbo wa kuingia unaendelea, Padre na wahudumu wengine ujongea kwa maandamano katika altare, ambapo utoa salam kwa kupiga magoti, ikiwa ni ishara ya kuabudu pia wanabusu na kama kuna ubani wanafukizia. Je ni kwanini? Kwasababu ni altare ya Kristo: ni sura ya Kristo. Na tunapotazama altare  Baba Mtakatifu amethibitisha kuwa, hapo yupo Kristo.

Akifafanua zaidi  amesema Altare ni Kristo wakati  ishara hizo ziko hatari ya kutazamwa hivi hivi tu, na kumba zina maana yake kwani zinaelezea tangu mwanzo kwamba, Misa ni kukutana na upendo wa Kristo, ambaye anatoa mwili wake juu ya msalaba na akawa altare na zabihu na kuhani mkuu.(Taza maombi ya Pasaka V). Altare kwa hakika ikiwa ni ishara ya Kristo pia ni kitovu cha matendo ya neema ambayo yanakamilisha na Ekaristi (Misale ya Roma 296)  na Jumuiya nzima ikiwa imezunguka altare ambaye ni Kristo; si kutazamana usoni hapana, ni kutazama Kristo wakiwa wote  wamezunguka altare hiyo kwasababu Kristo ni kitovu cha jumuiya na yeye hayuko mbali (…).

Ishara ya msalaba: Padre anayeadhimisha misa anafanya ishara ya msalaba na wote wanafuata, kwa utambuzi kuwa ni tendo la liturujia linalotendeka kwa jina la Baba,la Mwana na la Roho Mtakatifu. Pamoja na hayo Baba Mtakatifu ametaka kutoa nemo moja dogo kwa msisitizao kwamba,wote watambua jinsi gani watoto wanafanya ishara ya msalaba. Wao hawajuhi ni nini wanafanya kwa maana hiyo, mara nyingi urudia ishara hiyo. Watoto wanajua kuchora msalaba, lakini siyo ishara ya msalaba, hivyo, Baba Mtakatifu, ameomba wazazi wote, babu na bibi kuwafundisha watoto ili waweze kufanye vizuri ishara ya Msalaba. Na kwamba waweleze kuwa tendo la kufanya Ishara ya msalaba lina maana ya kuwa na ulinzi kwa njia ya Msalaba wa Yesu na kila Misa inaanza na ishara ya Msalaba.

Maombi yote yanaendelea  hivyo katika nafasi ya Utatu Mkatakatifu, ambaye ni Baba, Mwana na Roho Mtakatifuni nafasi ya umoja usioshia; ni kama vile upo mwanzo na mwisho wa upendo mmoja na Utatu, unajionesha na kujitoa  kwetu katika Kanisa la Kristo. Hiyo inajithibitisha katika fumbo la Pasaka ambalo ni zawadi ta Utatu na Ekaristi  ambayo daima ni  moyo ulichomwa na mkuki. Kwa kufanya ishara ya msalaba, si tu kufanya kumbukumbu ya ubatizo wetu, bali ni kuthibitisha kwamba sala ya liturujia ni kukutana na Mungu katika Yesu Kristo aliyejifanya mtu, akafa  na kufufuka kwa ushindi. 

Padre baadaye anatoa salamu ya kiliturujia akisema, “Bwana awe nanyi au sala nyingine inayofanana na hiyo, kwa maana zipo aina nyingi za salam; waamini wanajibu “iwe na roho yako”. Hapo ni kipindi cha mazungumzo; ni mwanzo wa Misa, katika kuingia kwa umoja ambao unaitikiwa kwa sauti mbalimbali , ikiwemo hata sehemu za ukimya na kujiundia utulivu wa ndani kwa wote wanaoshiriki, yaani kwa kuongozwa na Roho moja na yeye  na kwa lengo hilo moja. Hiyo  ndiyo pia inaonekana katika salam ya Kuhani na jibu la waamini wakionesha fumbo la Kanisa lililo unganika.( Taz Misa Roma 50) . 

Ni kujieleza kwa namna hiyo ya pamoja na imani na shahuku ya pamoja ya kutaka kukaa na Bwana na kuishi umoja pamoja  katika jumuiya nzima. Hii ni kama kwaya katika sala ambayo imeundwa na inawalika, ni sehemu  vyenye vionjo vya usikivu wa ndani kwasababu anayeadhimisha Misa anawalika wote kujitambua dhambi binafsi. Wote tu wadhambi, Baba Mtakatifu amesema, ila hajuhi vema, inawezekana kuna mwingine kati  yao hana dhambi. Na kama yeye si mdhambi, basi aamshe mikano juu na ili wote waweze kumtazama…. Basi kama hakuna mikono iliyo amshwa juu ina maana wote wana imani njema! Amesifu Baba Mtakatifu… Kwa maana wote tu wadhambi na ndiyo maana katika utangulizi wa Misa tunaomba msamaha, ndiyo tendo la maungamo.

Hii siyo jambo la kifikiria mara moja tu dhambi ambazo tumetenda, bali ni kufanya tendo hili mara nyingi: Ni wito wa kwenda kuungama dhambi mbele ya Mungu na mbele ya jumuiya, mbele ya ndugu, kwa unyenyekevu na wazi, kama alivyofanya  mtoza ushuru katika hekelu. Na kama kweli Ekaristi inawakilisha fumbo la Pasaka, hatuna budi kufanya hatua hiyo ya Kristo kutoka mauti hadi maisha  na kwa namna hiyo jambo moja tunalotakiwa kufanya ni lile la utambuzi wa hali halisi  za kifo chetu na  ili tupate kufufuka naye na kupata maisha mapya. Hiyo inatufanya tuwe na uelewa muhimu wa tendo la maungamo. Na mwisho Baba Mtakatifu amesema watendelea wiki ijayo ya katekesi ili kuendeza kufafanua sehemu hizo mbalimbali za Liturujia ya maadhimisho ya Misa. Kwasasa ni kwenda hatua kwa hatua katika kuelezea nini maana ya Misa,lakini amewapa tafadhali kwamba, wafundishwe watoto kufanya ishara ya Msalaba!

Mara Baada ya Katekesi: Baba Mtakatifu katika Katekesi yake iliyoudhuliwa na waamini zaidi ya elfu 5 amewabariki wanafamilia waliohitimisha  miaka 25 na 50 ya ndoa,  hata wale wapya. Pia katika salama zake kwa waamini wote, amewatakia matashi mema ya siku ya Kuzaliwa kwa Bwana na kwamba, Usiku wa Noeli unaangazwa na furaha na amani ya maisha ya kila mmoja na kwa namna ya pekee watu walio na upweke, wanaoteseka na wasio kuwa na nyumba. Na mwisho amewashukuru wasanii wa maonesho kutoka nchi ya Cuba ambao wameoonesha ujuzi wao mbele yake kwa kufurahisha alaiki mzima ya waamini wote waliofika kusikiliza tafakari ya Katekesi hii ya Baba Mtakatifu kabla ya Sikukuu ya kuzaliwa kwa Bwana.

Sr Angela Rwezaula
Vatican News
All the contents on this site are copyrighted ©.