2017-12-18 16:12:00

Papa:Jumapili ya tatu ya majilio inatualika katika furaha,sala na shukrani


Katika Domenika ziliozopita, liturujia imesisitiza maana ya kuwa na tabia ya kukesha na jinsi ya kutengeneza njia ya Bwana. Katika Domenika ya tatu ya Majilio, inayoitwa domenika ya furaha, liturujia inaalika  kuwa na  roho ya kumkaribisha  anaye kuja na furaha. Ni utangulizi wa maneno ya Baba Mtakatifu Francisko wakati wa tafakari yake ye siku ya Jumapili ya tatu ya majilio katika sala ya Malaika wa Bwana kwa mahujaji wote waliofika viwanja vya Mtakatifu Petro, tarehe 17 Desemaba 2017.

Mtakatifu Paulo anatualika kuandaa kumpokea Bwana kwa kujikita katika tabia tatu, na kusikiliza vizuri tabia hizo zina maana gani: kwanza ya furaha ya daima, pili sala isiyo na kikomo na tatu kutoa shukrani daima. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu anasisitiza, furaha ya daima, sala isiyo na kikomo na kuendelea daima kutoa shukrani! Akifafanua tabia ya furaha daima, iyokanayo katika kitabu cha Mtakatifu Paulo kwamba furahini daima(1Ts 5,16), anasema, ina maana ya kuwa, kudumu daima na furaha hata kama mambo hayaendi kwa mujibu wa mataka yetu: lakini kuna furaha ya kina ambayo ni amani na hata hiyo ni furaha ya kina na kwa ngazi ya kina.

Aidha Baba Mtakatifu anazidi kueleza kuwa ni lazima na furaha hata katika  huzuni, matatizo na mateso yanayojikita katika maisha ya kila siku ambayo tunayafahamu na mara nyingine hali halisi inayotuzunguka utafikiri ni kavu na ngumu kama ya jangwa ambalo limesikika katika sauti ya Yohane Mbatizaji na kama Injili ya siku inavyokumbusha…(Gv 1,23). Kwa maneno ya Yohane Mbatizaji yanaonesha kwamba furaha yetu inajikita katika uhakika, katika jangwa ambalo wanaishi. Inathibitika katika maneno ya Injili: “Katikati yenu, anasema, yupo mmoja ambaye hamjuhi”,  huyo ni Yesu , aliyetumwa na Baba yake, kama anavyotabiri Nabii Isaya , kuleta habari njema ya uhuru kwa watumwa na wafungwa kuwa huru, kwa kutangazia mwaka wa neema ya Bwana (Is 61,1-2).

Katika maneno ya Yesu huko Nazaret (Lk 4,16-19) anathibitisha kuwa, utume wa dunia hii unajikita kuokoa, kuhurumia dhambi na utumwa binafsi na kijamii unatokana na mambo hayo. Yeye alikuja dunia kutoa ahadi ya watu na kuwapa uhuru wana wa Mungu, kwa maana ni yeye anayeweza kuzungamza hilo  na kutoa furaha kwa ajili yake. Furaha inayojikita katika kusubiri Masiha, inasimamia juu ya maombi bila kuchoka: na ndiyo tabia ya pili ambayo Mtakatifu Paulo amesema,salini bila kuchoka (1 Ts 5,17). Kwa njia ya sala tunaweza kuingia katika uhusiano wenye msimamo na Mungu ambaye ni kisima cha furaha ya kweli. 

Furaha ya kikristo hainunuliwi, Baba Mtakatifu ansisitiza, huwezi kuinunua kwa maana  inatokana na imani na kukutana na Yesu Kristo ambaye ni sababu ya furaha yetu. Ikiwa tumesimika  mizizi katika Kristo ndiyo tunaweza kuwa karibu na Yesu na zaidi kuzidi  kuchota ule utulivu wa ndani , pamoja na kuwa katikati ya mambo yanayokwenda kinyuma na hali halisi ya maisha yetu ya kila siku. Kwa njia hiyo mkristo anayekutana na Yesu hawezi kuwa nabii wa matukio tu, bali ni shuhuda anayeonesha furaha. Furaha ya kushirikishana na wengine, furaha ya kuambukiza na kufanya safari ngumu ya maisha kuwa rahisi.

Akifafanua tabia ya tatu iliyoelekezwa na Mtakatifu Paulo, Baba Myakatifu anasema, ni ile ya kuendelea kuwa na shukrani. Kwa maana ya kuwa na utambuzi wa upendo mbele ya Mungu. Kwa dhati yeye ni mkarimu kwetu sisi, nasi pia tuaalikwa kutambua mema mengi ya upendo wa huruma, uvumilivu na wema ambao unatufanya kushi namna hiyo kwa shukrani.

Furaha, sala, na shukrani, ndiyo tabia ambazo zinatusaidia kujiandaa na kuish siku ya Noeli kwa dhati na hivyo Baba Mtakatifu amemalizia akiomba watamke wote kwa pamoja  furaha, sala na shukrani kama kiitikio cha maandalizi ya sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana. Na kwa maana hiyo hatua ya mwsho wa kipindi cha majilio, tujikabidhi chini ya maombi ya Bikira Maria, yeye ni sababu ya furaha na siyo tu kwasababu amemzaa Yesu bali anatuhimiza kwenda kwake daima.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Vatican News

 








All the contents on this site are copyrighted ©.