2017-12-15 17:11:00

Papa amekutana na wajumbe wa Shirikisho la Kiinjili Duniani!


Tarehe 14 Desemba 2017 jioni Baba Mtakatifu amekutana na wajumbe wa Shirikisho la Kiinjili Duniani kwa mkutano wa faragha. Na katika mkutano huo mada zao zilihusu safari ya kiekumene. Sorin Mureşan, ni mmojawapo wa watoa huduma ya kijamii katika Shirikisho la kiinjili ambaye ni kati ya wale waliokutana na Baba Mtakatifu Francisko jioni ya tarehe 14 Desemba 2017 ambaye kabla ya kutana naye aliacha maelezo mafupi kwa waandishi wa habari kwamba, “Tunakutana na Papa ili kujadiliana mambo ya kiekuemene  na hasa namna ya kutafuta njia ya pamoja. Kwa mwezi wa Oktoba mwaka huu,walitoa Hati ya Shirikisho la Kiinjili Duniani ikiwa na mada za kitaalimungu. 

Na kwa lengo la kukutana na Papa ni kutaka kutoa mapendekezo ya kuunda Kamati ya kudumu ya mazungumzo kati ya Kanisa Katoliki ambalo ni Kanisa kubwa la Ulimwengu , na Shirikisho la Kiinjili Duniani. Ni matarajio yao kuwa Baba Mtakatifu atakuwa na ufunguzi huo maalumu kwa maana ni rahisi kuongea naye!

Historia ya Shirikisho hili ilianzia karne ya XIX. Wazo la shirikisho la kiinjili linajikitia katika muungano na ushirikiano kati ya Makanisa yote ya kiinjili katika nchi mbalimbali , ambapo kwa mara ya kwanza ilitokea nchini Uingereza mwaka 1848. Wakati Bara la Ulaya liko kwenye vuguvugu la mapinduzi , waanzilishi wa Shirikikisho hili walitangaza kwa shahuku kubwa umuhimu wa kuunda Shirikisho lenye msingi wa kiinjili ambao ndio ulikuwa unawaongoza. Kuanzishwa kwa tendo hili baadaye uliigwa  na kuchanua ndani ya mataifa mengine. Baada ya kupatikana wadau wengi kutoka sehemu kubwa ya shirikisho la  kiinjili kitaifa ndipo ikaundwa Shirikisho la Kiinjili Duniani.

Sala na matendo ya huruma:Katika Karne ya kwanza ya uwepo wake, shirikisho hili limefanya mipango mingi  na hasa ya matendo ya huruma na kati yake, uhamasishaji wa Wiki ya sala kwa ajili ya dunia nzima. Mwaka 1958 ilianzishwa Shirikishi la Kiinijili la kimisionari, ambalo linaunganisha karibu jamii zote za kimisionari kiinjili. Mwaka 1973 ikaanzishwa Shirika la msaada wa  kibinadamu (Tearfund) inayojikita katika shughuli za kutoa sadaka na matendo ya huruma  katika nchi mbalimbali. 

Mwaka 2004 , kama shirika la lisilo la kiserikali la kikristo , waliweza kusaidia zaidi ya watu 700,000 katika nchi za Bara la Asia Mashariki na kati ya nchi hizo ni Sri Lanka na Indonesia waliokuwa wamekumbwa na tetemeko la ardhi na matukio ya vimbunga.
Idadidi ya Watu wa Kiinjili: Hakuna idadi kamili ya wakristo wa maakanisa ya kiinjili duniani, bali kwa mujibu wa mwanahistoria Sébastien Fath na mtafiti wa Kituo cha Kitaifa cha Sayansi Centre national de la recherche sciéntifique (Cnrs) mjini Paris Ufaransa, anasema ni makadirio ya mioni 620. Hawa zaidi ni kutoka katika Bara Asia ambao ni  (milioni200),  Afrika (milioni 170). Amerika ya Kusini  ni karibia  milioni 120 na Ulaya ni karibia  milioni 23.

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.