2017-12-14 16:49:00

Papa:Mabalozi wapya wawe chombo cha ushuhuda wa haki na amani kati ya tamaduni



Baba Mtakatifu Francisko Alhamisi 14 Desemba 2017 amekutana na kuzungumza na mabalozi wapya kutoka: Yemen, New Zelanda, Swaziland, Azerbaigian, Chad, Liechtenstein na  India katika ukumbi wa Clementina Mjini Vatican. Baba Mtakatifu amewakaribisha na kuwapongeza katika kuwakilisha barua ya kupokelewa Vatican kutoka katika nchi zao. Amewaomba waweze kufikisha  pongezi na uhakika wa sala zake kwa ajili ya watu wa nchi watokako.

Baba Mtakatifu katika hotuba yake amesema, mwanzo wa utume wao, yeye binafsi anao utambuzi wa utofuti wa nchi ambazo wanawakilisha, zenye  tamaduni,mila na dini tofauti zinazowakilisha historia ya kila nchi zao. Na kwa njia hiyo amesema, inampa fursa yake ili kusisitiza juu ya jukumu kuhamasisha na kuendeleza katika ujenzi,  ambao kutokana na tofauti hizi, ndiyo chagizo katika tamasha la mataifa.

Jumuiya ya kimataifa inakabiliwa na mfululizo wa vitisho vingi katika  ulinzi na uendelezaji wa mazingira, mbele ya ekolojia  ya kijamii na binadamu ndani ya sayari nzima, kama vile pia vitisho vya amani na mapatano vitokanavyo na itikadi kali  za nguvu na migogoro ya kikanda, ambayo mara nyingi huonekana katika mwelekeo wa kutaka maslahi na kupinga maadili.  Hata hivyo anaongeza, ni muhimu kukumbuka kuwa tofauti za familia ya kibinadamu haiwezi kuwa ndiyo sababu ya changamoto hizi kusababisha ukosefu wa umoja wa amani.  Hakika, nguvu za kitovu cha vikosi ambavyo vinapenda kutenganisha watu, siyo za kutafuta katika tofauti zao, bali ni katika kushindwa kuanzisha njia ya mchakato wa  mazungumzo na uelewa kama njia bora zaidi ya kukabiliana na changamoto hizi.

Baba Mtakatifu anasisitiza kuwa, uwepo wao Vatican  ni mfano wa jukumu muhimu ambalo mazungumzo hufanywa katika kuruhusu uzoefu wa kuishi utofauti katika njia halisi na kwa manufaa ya jamii yao  inayozidi kuongezeka zaidi katika utandawazi. Na  mazungumzo ya heshima husababisha ushirikiano, hasa katika kukuza upatanisho, mahali ambapo inahitajika zaidi. Ushirikiano huo husaidia mshikamano, ambao ni hali ya ukuaji wa haki na inayostahili heshima ya hadhi, haki ya binadamu na na matakwa ya wote. 

 Baba Mtakatifu anaongeza. Wajibu wa mzaungumzo na ushirikiano ni lazima kuwe isara ya  nguvu kwa kila taasisi ya jumuiya ya kimataifa, na kama  vile kwa kila taasisi ya taifa na mahalia, wakati wote wakiwa wamepewa jukumu ya kutafuta wema wa pamoja. Lakini pamoja na hayo,kukuza mazungumzo, upatanisho na ushirikiano hauwezi kuchukuliwa kwa urahisi. Na hivyo inahitaji  sanaa maridadi ya kidiplomasia na kazi ngumu ya kujenga taifa. Ili kufanya hivyo ni lazima kujifunza daima na kwa kila kizazi kipya na endelevu. Ni lazima kushirikishana wajibu wa pamoja wa kuwaelimisha vijana kuhusu umuhimu wa misingi hii inayoungwa mkono na utaratibu wa kijamii. 

Kwa njia Baba Mtakatifu amewahimiza  waoneshe  urithi huu wa thamani kwa watoto wa kizazi hiki na endelevu na wajukuu kwamba si tu kuwakikishia amani na mafanikio ya baadaye, bali hata kutakidhi mahitaji ya haki ya asili na maendeleo ya kibinadamu ambayo ni ya kila mtu, awe mke na mtoto wote  wanayo haki. 

Amemalizia kwa kusema, wakati wao wanachukua jukumu la ngazi ya juu katika  huduma ya kuwakilisha nchi zao, anawakikishia kuwasindikiza kwa msaada utakaohitajika katika shughuli zao  ofisini Vatican. Na hivyo amewapa  baraka na kuwatakia kazi njema wanayo ananza.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.