2017-12-14 17:12:00

Bwana Burke amewasilisha yatokanayo na Baraza la Ushauri wa Makardinali 9


Baraza la ushauri la Makardinali,wanaoshirikiana na Baba Mtakatifu Francisko wamekuwa na mkutano wao kwa siku tatu kuanzia tarehe 11 hadi 13 Desemba 2017. Wameudhuria wajumbe wote wa Baraza la ushauri, isipokuwa Kardinali George Pell na Kardinali Laurent Monsegwo Pasinya, aliyewasiri Jumatatu jioni kutokana na ndege kufuta ratiba yake ya usafiri kwasababu ya hali mbaya ya hewa.

Amayesema hayo kwa waandishi wa habari Msemaji Mkuu wa Vatican Bwana Greg Burke, wakati wa kuwasilisha habari kamili  juu ya mkutano huo tarehe 13 Desemba 2017, kwa waandishi wa habari na  kwamba Baba Mtakatifu ameudhuria vikao vyote ispokuwa asubuhi ya Jumatano, kutokana na Katekesi yake katika ukumbi wa Mwenye heri Paulo VI. Mkutano wa Jumanne 12 Desemba ulikuwa mfupi zaidi ya ulivyotarajiwa na  kuwawezesha makardinali kuudhuria misa iliyoongozwa na Baba Mtakatifu Francisko kwa tukio la Sikukuu ya Bikira Maria wa Guadalupe msimamizi wa bara la Amerika ya Kusini.

Bwana Burke akiendelea na maelezo hayo amesema, kwa kawaida, shughuli zao za vikao huanza asubuhi ya saa tatu hadi sita na nusu, na mchana kuanzia saa kumi na nusu hadi saa moja za jioni, kwa njia hiyo, katika vikao hivyo  walijikita kwa upya katika kutafakari  juu ya Vatican, kama chombo ya uinjilishaji na huduma kwa ajili ya Papa na kwa ajili ya Kanisa mahalia. Kikundi cha makardinali hawa 9, zaidi wametafakari kwa kina masuala yanayohusu Mabaraza manne ya kipapa: kama vile ya Makleli, Uinjilishaji wa watu, elimu Katoliki na utamaduni . Sehemu nyingine ya kazi ilikuwa inahusiana shughuli zilizotolewa na wakuu wa Mabaraza ya Kipapa kwa ajili ya Walei, familia na maisha; Sekretarieti ya Mawasiliano na katika kitengo cha wahamiaji na wakimbizi cha Baraza la Kipapa kwa huduma ya Maendeleo ya binadamu.

Naye Kardinali Kevin Ferrell, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Walei, familia na Maisha, ameonesha  kuundwa kwa Baraza jipya, lililoanzishwa tarehe 1 Septemba 2016 kwa tahadhari maalumu katika uhusiano wa Baraza hilo na vijana, lakini si tu kwa mtazamo wa Sinodi. Makardinali pia wamewasikiliza Padre M. Czernyna padre Fabio Baggio, ambao ni Makatibu wasaidizi katika Kitengo cha wahamiaji na wakimbizi wa Baraza la Kipapa kwa huduma ya Maendeleo endelevu, ambao wameelezea mchakato wa kuandaa kitengo kilichowekwa kwa muda chini ya uongozi wa Papa.

Wafanyakazi kwa sasa ni 21 na kati ya wanaofanya kazi hao, wapo hata wa kujitolea. Shughuli zote zilizo anzishwa mwaka 2017 zina wajumbe wake ndani ya Baraza ambao wanajumuisha hata Makanisa mahalia katika kubuni na utekelezaji wa jibu la kichungaji lenye ufanisi na linalokabiliana na changamoto za ulimwengu wa sasa, kuhusu wahamiaji, wakimbizi na waathirika wa biashara ya binadamu.

Aidha Bwana Burke amesema, miongoni mwa shughuli kuu: ilikuwa ni Mkusanyiko na utaratibu wa habari juu ya masuala ya uhamiaji moja kwa moja kutoka msingi, utekelezaji wa kampeni mbalimbali za vyombo vya habari  kwa ajili ya maelezo mazuri juu ya wahamiaji na wakimbizi, kuandaa hati yenye matendo ishirini (20 Action Points) katika mtazamo wa Wahamiaji na Wakimbizi kwa mwaka 2018 (Compact Global Global 2018); kufafanua mkakati wa kimataifa na watendaji wakuu Katoliki (Sekretarieti ya Vatican, Mikutano ya Mabaraza ya maaskofu, Mashirika yasiyo ya kiserikali Katoliki na Mashirika ya kidini) na baadhi ya misaada ya moja kwa moja kutoka kwa Mabaraza ya Maaskofu.

Kardinali  Sean Patrick O'Malley amesasisha wajumbe wengine wa Baraza kuhusu kazi ya Tume ya Kipapa ya Ulinzi wa Watoto, ambapo wanachama wake wanakaribia kumaliza muda wake, kwa mtazama hasa kuhusu kazi ya kusaidia Makanisa mahalia. Mkutano wa Makardinali Washuri 9  ujao umepangwa kufanyika kuanzia tarehe 26 -28 Februari 2018.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.