2017-12-12 15:46:00

Kard.Bassetti:Kanisa ni mstari wa mbele kumsindikiza mgonjwa hatua zote!


Kuhifadhi hospitali Katoliki dhidi ya makapuni binafsi ni wito wa Baba Mtakatifu uliomo katika Ujumbe wa Siku ya Wagonjwa Duniani kwa mwaka 2018. Baba Mtakatifu amerudia kusisitiza juu ya kuweka kiini cha binadamu kulingana na mahusiano ya uchumi, ambayo mara nyingi wanafanya mchezo katika  afya ya binadamu. Kuhusiana na wito huo, pia hata wito wa  hivi karibuni  alioutoa kwa wajumbe wa Mkutano wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Maisha. Mwandishi wa habari wa Radio Vatican, amemhoji Kardinali Gualtiero Basseti, Askofu Mkuu wa Perugia-Citta della Pieve, ambaye pia ni Rais wa Baraza la Maaskofu wa Italia kuhusiana na suala hilo la maisha.

Katika suala hili, Kardinali anaeleza na hasa kwa kujikita zaidi  na ujumbe wa Baba Mtakatifu alioutoa kwa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Maisha ambapo amesisitiza juu ya umuhimu wa kuwajibika hasa  kuwasindikiza binadamu katika mchakato wa maisha ya mateso na zaidi wale  wenye magonjwa yasiyo pona, pia  kutungwa kwa maisha na katika mchakato mzima wa maisha hadi mwisho wake.  Kardinali Bassetti anasema kuwa, ni kazi ngumu ya kung’amua na kutumia busara ya upendo kwa ajili ya watu wote na hasa wale wali huru na kuhamasika, ambao ni kama wachungaji na si mbwa mwitu. 

Kuhusiana na mashirika binafsi ambayo Baba Mtakatifu anataja katika Ujumbe wa Siku ya Wagonjwa duniani, Kardinali Bassetti anasema, hatari ya mashirika binafsi inaweza kuhepukwa na kushinda kuwa na inguvu zaidi iwapo inaweza kutambua zaidi kuweka kiini kwa namana ya  macho na moyo wake kwa kina juu ya binadamu anayeteseka.  Na ndiyo maana si kwa bahati mbaya Baba Mtakatifu ametaja Kanisa kwa kulifananisha kama Injili ya msamaria mwema. Ametaka kukumbusha kuwa  Kanisa ni kama msingi mkubwa kwani kamwe haliwezi kumwacha peke yake mgonjwa. Msamaria anatazama na kujihusisha kwa kina, akiweka nguvu zake zote na rasilimali zake zote ili  aweze kukabiliana na aliyejarehiwa. Na  ndiyo utofauti uliopo wa kuhani na Mlawi ambao  wanatazama na kugeukia sehemu nyingine. 

Kardinali  Basseti  akifafanua juu ya hotuba ya Baba Mtakatifu  hasa anaposema juu ya kukatisha maisha, anasema  kwamba maneno ya Baba Mtakatifu ni bayana kwasababu ya kutaka  kuhamasisha Kanisa mbele ya changamoto za binadamu, na kuhamasisha daima hasa kwa namna ya kuchangia ili maisha ya binadamu yaweze kusindizwa  kwa hali zote, kuanzia maisha anapotungwa, ya mateso katika ugonjwa na katika kukaribia kifo. Na kwa njia hiyo mchakato wa kukatisha maisha ya binadamu,sehemu hiyo ni nyeti sana kwasababu, daima siyo rahisi kuthibitisha ukweli zaidi kati ya yule anayetoa uamuzi kulingana na  utashi wa mgonjwa  na dhamiri na ujuzi wa daktari. Katika moyo wa mang’amuzi hayo unatazama hasa uhusiano kati ya mgonjwa,na dakari au hali ya pamoja katika tiba ambayo kamwe isiwe sehemu ya utamaduni wa ubaguzi ambao umetajwa na Baba Mtakatifu.

Lakini kama mwakilishi wa Baraza la Maaskofu wa Italia kuhusina na suala nyeti la Eutanasia na mwisho wa maisha kibayolojia anasema , kufa ni sehemu ya maisha ya mwanadamu  ni kukutana na kizingiti cha maisha: kwa njia hiyo ni kufanya uzoefu wa udhaifu na mahitaji ya kujikabidhi kwa mwingine, hasa yule aliye wa juu kabisa ambaye ni Bwana mwenyewe. Katika hali hii, inahitaji ukaribu wa tiba na upendo. Hivyo ndipo inachukua umuhimu wa matibabu ya muda ambayo yanasaidia kuleta unafuu wa maisha katika ugonjwa usiopona na hata unafuu katika hatua zake za mwisho wa ugonjwa kwa kuhakikisha kuwa mgonjwa anasindikizwa kibinadamu (Evangelium vitae 65).

Wakati inapojitokeza hali ya kukataa tiba kulingana na hali ya mgonjwa na kwa kwa mtamzamo wake, siyo sababu ya kukataa kuonesha ishara msingi za kumsaidia kwa njia zozote huyo mtu. Kama Cei wanajikita kwa moyo wote ili uwepo uwezekano wa kukataa dhamiri za daktari binafsi katika suala hili la kukatisha maisha, jambo ambalo anasema  linaathiri vituo vingi vya afya nchini Italia.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.