2017-12-11 15:56:00

Ujumbe wa Papa Francisko kwa Siku ya 26 ya Wagonjwa Duniani 2018


Mater ecclesiae "Mama wa Kanisa “Tazama huyo ndiye mwanao … tazama huyo ndiye mama yako. Na tangu saa ile huyo mwanafunzi alimchukua akae nyumbani kwake”(Gv,19,26-27)
Huduma ya Kanisa kwa wagonjwa na wote wanojikita katika kuhudumia, lazima daima wajikite  kwa kina na kwa uaminifu wa utume wa Bwana (Lk 9,2-6: Mt 10,1-8; Mk 6,7-13), kwa kufuata mfano wa maneno mazuri ya mwanzilishi wake na Mwalimu. Mwaka huu kauli mbiu ya Siku ya Wagonjwa Duniani, inatupatia maneno ya Yesu aliyotamka msalabani, akimwelekea mama yake Maria na Yohane: “Tazama huyo ndiye mwanao … tazama huyo ndiye mama yako. Na tangu saa ile huyo mwanafunzi alimchukua akae nyumbani kwake”(Yh 19,26-27). 

Huo ni utangulizi wa Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko uliotolewa tarehe 11 Desemba 2017, kutokana na tukio la  siku ya Maadhimisho ya 26 ya Wagonjwa duniani mwaka 2018 inayoongozwa na kauli mbiu “Mama wa Kanisa “ tazama huyo ndiye mwanao… Tazama huyo ndiye mama yako”. Na tangu wakati huo mtume wakamkaribisha nyumbani kwake Yh 19,26-27. 

Katika ujumbe huo, Baba Mtakatifu anasema, Maneno ya Bwana yanaangaza kwa kina fumbo la Msalaba. Maneno hayo hayawakilishi janga hilo bila matumaini, bali ni mahali ambapo Yesu anaonesha utukufu wake alijiachia kwa utashi wa upendo wake upeo, ambapo huo nsiyo  unakuwa mpango wa katiba ya jumuiya ya kikristo na ya maisha ya kila mkristo

Hawali ya yote maneno ya Yesu yanatoa chanzo cha wito wa umama wa Maria mbele ya binadamu wote. Yeye kwa namna ya pekee anakuwa mama wa mitume na mwanae. Achukuwa wajibu wa kuwatunza na katika safari yao. Wote tunatambua kuwa utunzaji wa mama kwa mwanae huanzia katika mantiki zote ziwe katika nyenzo na hata kiroho kwa mafundisho yake. Injili inasema, “katika uchungu ulio kama upanga mkali utauchoma moyo wa Maria” (Lk2,35) lakini haumwogopeshi. Badala yake, kama Mama wa Bwana anaanza yeye safari moja kwa moja  ya kujiotoa yeye binafsi. Akiwa msalabani,Yesu anahangaikia Kanisa na binadamu wote, na Maria naitwa kushirikisha wasiwasi wa Yesu.

Baba Mtakatifu Francisko anaongeza kusema, katika kitabu cha Matendo ya Mitume, kikielezea juu ya tukio la Roho Mtakatifu Siku ya Pentekoste, kinaonesha kuwa Maria alianza shughuli yeke katika Jumuiya ya kwanza ka Kanisa. Ni kazi ambayo haina mwisho.
Mtume Yohane, mpendwa, anawakilisha Kanisa, ambao ni watu kinabii.Yeye ni lazima atuambie kuwa Maria  ni mama yake. Na katika utambuzi huo, anaalikwa kupokea na kutafakri Maria  kama mfano wa utume na hata wito wa mama ambaye Yesu amemkabidhi, ikiwa ni pamoja na wasiwasi wake na mipango yote itokanayo na wito huo; kwa maana  ni mama anaye penda na kuzaa watoto wenye uwezo wa kupenda kwa mujibu wa amri ya Yesu. Kwa njia hiyo wito wa mama Maria yaani  wito wa kutunza watoto wake, unapitia kwa njia ya Yohane na Kanisa zima. Na Jumuiya nzima ya mitume wanahusika katika wito wa mama Maria.

Yohane kama mtu anayeshirikishana na Yesu kila kitu anatambua jinsi gani Mwalimu wake anataka kuwakusanya watu wote wakutane  na Baba.Yeye anaweza kushuhudia kuwa Yesu alikutana na watu wengi wakiwa wagonjwa wa kiroho roho na kwasababu wamejaa kiburi (Yh 8,31-39) pia wagonjwa kimwili (Yh 5,6). Na kwa watu wote aliwapa huruma na msamaha. Na wagonjwa kimwili wakapona, na ishara ya maisha yaliyojaa Ufalme, ni mahali ambapo machozi yanakaushwa. Kwa njia hiyo, kama Maria, mitume wanaalikwa kuhudumiana. Pia wanatambua ya kwamba, moyo wa Yesu huko wazi kwa wote bila ubaguzi. Wote wanapaswa kupashwa habai ya  Injili ya Ufalme, wote ambao wanahitaji, wanapaswa kuelekezwa katika upendo wa kikristo kwa urahisi, kwasababu ni watu, na wana wa Mungu.

Wito wa umama katika Kanisa, kwa ajili ya wahitaji na wagonjwa umejidhihirisha katika historia ya miaka elfu mbili iliyopita, katika utajiri wa kuanzisha mipango mingi kwa ajili ya wagonjwa. Ni historia ya kujikita katika shughuli hiyo bila kusahau. Hata leo hii inaendelea katika dunia. Baba Mtakatifu anafafanua akisema kuwa:    katika nchi ambazo kuna mipango ya Afya ya umma inayojitosheleza, shughuli ya mashirika Katoliki, katika majimbo na mahospitali, zaidi ya kutoa tiba za hali ya juu pia wanatafuta kwanza kumweka  binadamu awe ni kitovu katika mchakato wa tiba na kuendelea na utafiti wa kisayansi kulingana na maisha na thamani zake za kimaadili ya kikristo.

Katika nchi ambazo kuna uhaba wa mipango ya afya, au kutokuwapo kabisa, Kanisa linajikita kutoa kile ambacho inawezekana kwa watu, kama vile utunzaji na afya, ili kuondoa na kupunguza vifo vya watoto wachanga. Aidha hata kuwasaidia baadhi ya wengine wanye magojwa ya kuambukiza. Kila mahali Kanisa linajitahidi kutibu, hata kama haina uwezo wa kuponyesha. Sura ya Kanisa ”kama hospitali iliyoko katika kambi”, inapokea wote  walio jeruhiwa katika maisha. Ni hali halisi na ya dhati kwasababu katika maeneo mengi ya ulimwengu, zipo hospitali za wamisionari na katika majimbo ambayo wanatoa huduma ya tiba muhimu kwa watu.

Kumbukumbu ndefu ya kihistoria ya huduma kwa wagonjwa; ni sababu ya furaha kwa jumuiya ya kikristo na kwa namna ya pekee kwa wale wanaotoa huduma hiyo nyakati za sasa. Baba Mtakatifu anafafanua kuwa: ili kuweza kufanya hivyo, lakini ni lazima kutazama yaliyopita ili kujitajirisha kutokana nayo. Yote hayo ni lazima kujifunza kutokana na ukarimu hadi kujitoa sadaka ya moja kwa moja kwa waanzilishi wengi wa mashirika ya huduma ya wagonjwa kama vile : ubunifu unao elekezwa kutokana na upendo; shughuli nyingi zilizo anzishwa katika mihongo mingi; shughuli za utafiti kisayansa, ili kuweza kutoa tiba kwa wangojwa kwa njia ya ubunifu na matibabu ya kuaminika. 

Anathibitisha zaidi kwamba, urithi huo wa kizamani unasaidia kupanga vizuri mipango ya baadaye. Kwa mfano wa kuhifadhi mahospitali Katoliki ambayo yako hatari ya  kuchukuliwa na mashirika binafsi, ambayo duniani kote yapo yanatafuta kuingiza tiba za afya lakini kwa mantiki ya masoko, na mwishowe kuishia katika ubaguzi wa maskini. Mipango ya busara  na upendo vinahitaji zaidi kwamba binadamu mgonjwa, aheshimiwe katika hadhi yake na kuwekwa katika kitovu daima cha mchakato wa tiba. Maelekezo hayo yanapaswa kuwa hata kwa wakristo wanaotoa huduma katika mahospitali ya serikali, kwa maana katika huduma yao wanaalikwa kutoa ushuhuda mwema wa Injili. 

Yesu aliacha zawadi kwa Kanisa ya nguvu ya huponyaji:”Na ishara hizi zitaandamana na wale wanaoamini:(…) watawawekea wagonjwa mikono, nao watapona” (Mk 16,17-18). Katika kitabu cha matendo ya Mitume, tunasoma maelezo ya uponyaji uliofanywa na Petro ( Mdo 3,4-8) na  Paulo (Mdo At 14,8-11). Katika zawadi ya Yesu inafanana na Shughuli ya Kanisa ambayo inatambua kujikita  kwake kwa  wagonjwa, kwa mtazamo wa ukarimu mwingi na huruma ya Bwana wake.  Kwa namna hiyo Baba Mtakatifu anathibitisha kuwa, shughuli za kuchungaji katika afya zinabaki na zitaendelea daima kuwa shughuli ya lazima na muhimu  ili  kuweza kuishi na msukumo mpya kuanzia katika jumuiya za parokia hadi kufikia vituo bora zaidi vya matibabu.

Anasisitiza kuwa, hapo hatuwezi kusahau huruma na uvumilivu ambao familia nyingi hufuatilia watoto wao, wazazi na jamaa, wagonjwa sugu au walemavu. Utunzaji ambao hutolewa katika familia ni ushuhuda wa ajabu wa upendo kwa mwanadamu na lazima uungwe mkono kwa kutambuliwa vya kutosha na sera za kisiasa zinazofaa. Kwa njia hiyo, madaktari na wauguzi, makuhani, watu waliowekwa wakfu, wakujitolea, wanafamilia na wale wote wanaoshiriki katika huduma ya wagonjwa, washiriki katika wito huu wa Kanisa. Ni jukumu la pamoja ambalo linaboresha na kutajirisha thamani ya huduma ya kila siku ya kwa kila mmoja.

Kwa Maria, Mama wa huruma, tunataka kumtolea  wagonjwa wote, ikiwa ni kimwili na kiroho, ili awaweke katika tumaini. Kwake yeye tunamwomba pia kutusaidia tuwe wakarimu kwa kuwapokea  ndugu wagonjwa. Kanisa linatambua kuwa na kuwa na  haja ya neema malumu ili kuweza kujikita katika huduma yake kiinjili kwa ajili ya wagonjwa. Kwa njia ya sala kwa mama wa Bwana, atutazame wote tunaounganika katika maombi ili kila mwanachama wa Kanisa awe hai na upendo wa wito wa huduma ya maisha na Afya.

Baba Mtakatifu anamalizia ujumbe wake:Bikira Maria aombee siku ya 26 ya Wagonjwa duniani, asaidie wagonjwa wote waishi katika mateso yao na muungano na Bwana Yesu; awasaidie hata ambao wanawasaidia katika matibabu. Na kwa wote: wagonjwa, wahudumu wa Afya, watu wa kujitolea, anawapa Baraka yake.

Vatican tarehe 26 Novemba 2017
Sikukuu ya Bwana wetu Kristo Mfalme wa Ulimwengu.

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.