2017-12-08 15:57:00

Papa:Neno la Mungu ndiyo siri ya Mama Maria na dhambi inazeesha roho!


Leo hii tunatafakari uzuri wa Maria Mkingiwa wa dhambi ya asili. Katika Injili inaelezea juu ya Maria kupashwa habari na kutusaidia kuelewa zaidi ya kile tunachosheherekea hasa kwa njia salamu ya Malaika.  Ni maneno ya Takafakari ya Baba Mtakatifu Francisko  tarehe 8 Desemba 2017, wakati wa sala ya Malaika wa Bwana kwa mahujaji wote katika uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, Mama Kanisa akiadhimisha Sikukuu ya Mama Maria Mkingiwa wa dhambi ya asili.

Baba Mtakatatifu Francisko katika tafakari hiyo anasema:Malaika wa Bwana alimsalimia Maria kwa neno ambalo ni gumu kutafsiri,kwa maana ya: umetulizwa na neema,  umeumbwa na neema, umejaa neema (Lk 1,28).  Lakini kabla ya kumwita Maria, alimwita umejaa neema,  kwa njia hiyo anaonesha jina jipya ambalo Mungu ameongeze zaidi ya lile alilopewa na wazazi wake. Hivyo hata sisi wenyewe tunamwita hivyo “Salam Maria”. 

Je nini maana ya kujaa neema? Baba Mtakatifu anafafanua, Maria amejazwa na uwepo wa Mungu. Mungu anaishi ndani ya maisha yake, kwa maana hiyo hana nafasi ya dhambi ndani yake. Ni jambo la hajabu, kwasababu dunia nzima kwa bahati mbaya imeambukizwa na ubaya. Kila mmoja akijitafiti nafsi yake, ataona kuwa kuwa kuna sehemu yenye giza.

Hata watakatifu wakuu walikuwa wadhambi na katika hali halisi hadi kufikia hata mambo yaliyo mazuri zaidi yameshambuliwa na ubaya. Ndiyo ni yote japokuwa ni Maria peke yake hasiyekuwa na dhambi. Yeye ni  ("Oasis) ni chem chemi ya kijani ya ubinadamu; Ni yeye pekee ambaye hakuambukizwa, alieyeumbwa bila dhambi kwa ajili ya kupokea kwa ukamilifu ile ndiyo yake ambayo Mungu alikuwa anakuja ulimwenguni na hivyo akaanza historia mpya.
Kila mara tunapokuwa na utambuzi wa kujaa neema, Baba Mtakatifu anabainisha kuwa, tumpe sifa kubwa,ambayo ndiyo pia alimpatia Mungu. Ni sifa nzuri ya kumpa mwanamkea ambaye anajionesha kijana.Tunposema Salam Maria umejaa neema, kwa maana nyingine tunaitamkwa kwa ngazi ya juu.

Kwasababu tunao utambuzi kuwa, yeye ni kijana kwasababu hakuzeeshwa na dhambi. Baba Mtakatifu anafafanua na kusema, kuna jambo moja pekee la ukweli linalofanya kuzeesha roho. Si umri bali ni dhambi. Dhambi inazeesha, kwasababu inagandisha moyo. Inafunga na kufanya moyo isichanue. Lakini aliyejaa neema hana dhambi. Kwa namna hiyo yeye daima ni kijana zaidi ya dhmbi, na ni kijana anayezaa ubinadamu.

Leo hii Kanisa linatoa sifa, na pia  Maria kwa kumwita yeye ni mzuri kama wimbo wa (tota pulchra).Lakini, ujana wake si katika umri,au uzuri wake si ule wa nje nje.  Kama inavyoonesha Injili ya Siku,si katika mtazamo wa nje: kwa maana ilikuwa ni familia rahisi ambayo alikuwa anaishi kwa unyenyekevu huko Nazareth, kijiji kisichojulikana.Yeye hakuwa maarufu; hata Malaika alipomtembelea hakuna yoyote aliye jua,na siku ile hapakuwapo na mtoa ripoti. Maria hakupata maisha ya mepesi, bali yaliyojaa mahangaiko na hofu:Yeye alikuwa na wasiwasi (Lk 1,29)  kwa maana Injili inaeleza kuwa,mara tu Malaika alipoondoka, matatizo yalizidi kuongezeka (Lk 1,38).

Lakini pamoja na  hayo “umejaa neema” aliishi maisha mazuri. Je ni siri gani aliyokuwa nayo? Baba Mtakatifu anafafanua:tunaweza kugudua kwa kutazama picha ya kupashwa Maria habari na Malaika. Wasanii wengi wanachora picha za Maria akiwa amekaa mbele ya Malaika, ameshikilia kitabu Mkononi. Hivyo ni kitabu cha maandiko matakatifu. Ni kuonesha kuwa  Maria, kawaidia alikuwa akisikiliza Mungu na kuzungumza naye.

Neno la Mungu lilikuwa ni siri yake: lilikuwa karibu na moyo wake, na kwa njia hiyo akachukua mimba yake. Kukaa na Mungu, kuzungumza naye kila wakati, kulimfanya Maria awe mzuri katika maisha yake. Leo hii kwa furaha kubwa ni kutazama aliye jaa neema. Na kumuomba atusaidie kubaki kijana, na kupinga dhmbi ili tupate kushi maisha mazuri yanayotamka ndiyo kwa Mungu.

Mara baada ya sala ya malaika wa Bwana, amewasalimia mahujaji wote waliokuwapo,hasa familia na makundi kutoka katika parokia.

Katika sikukuu ya Mkingiwa dhambi ya Asili, chama cha utume katoliki wa vijana nchini Italia leo hii wanarudia hatamu zao kwa upya, kwa njia hiyo mawazo yanawandea vyama vyote vya vijana kitumea  vya kijimbo na kiparokia, akiwatia moyo wote ili wajikite kwa juhudi kubwa ya mafundisho ili yaweze kuleta matunda ya mapendekezo yake ya kuhudumia utume wa uinjilishji wa Kanisa. 

Aidha amewataarifu ya kwamba mchana wa sikuu ya Mama Maria mkingiwa wa dhambi ya asili atakwenda katika Uwanja wa Spagna mjini Roma ili kama utamaduni, kusali chini ya miguu ya sanamu ya Mama Maria Mkingiwa dhambi ya Asili . Na kwa njia hiyo anawaomba wote kuunganika kiroho kwa sala katika ishara hiyo ya kuonesha kwa udhati wa kuwa mtoto kwa Mama yetu wa Mbinguni.

Sr Angela Rwezaula 
idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.