2017-12-07 16:35:00

Papa kwa wanakwaya wadogo:nyimbo zenu zinaleta utulivu kwa watu wanaoteseka


Mungu alijifanya mtoto na kuwa karibu na binadamu wa kila wakati kwa kumuonesha huruma isiyo kuwa na kikomo. Hayo ni maneno ya Baba Mtakatifu aliyotoa wakati wa kukutana na kikundi  kwaya za nyimbo za watoto kiitwacho “Piccolo Coro Mariele Ventre” cha Mtakatifu Antoni huko Bologna Italia, ambao kwa mwaka huu wamaadhimisha miaka 60 tangu kuanzish mashindano ya “Zecchino d’oro”.

Mkutano na watoto hao umefanyika katika ukumbi wa Clementina Vatican. Nyimbo za watoto kwa mashindano tayari zimeanza ambazo zinaoneshwa mbashala katika Televisheni ya Italia (RAI) hadi Jumamosi tarehe 9 Desemba 2017. Hawa ni watoto walio mstari wa mbele kuanzia miaka 3-12. Ni  nyimbo 999 ambazo zimatafisiriwa na kuimbwa tangu mwaka 1959 hadi sasa. Ni kwaya inayo chukua jina la mwanzilishi wake na mkurugenzi  Mariele Ventre,ambaye aliongaza kwaya hiyo miaka 30  na mwaka 1995 Mungu akamwita kwake.

Katika hotuba yake Baba Mtakatifu anasema,ni matanio yake kutoa shukurani na sifa ya kuwadhimisha kwaya yeno ambayo inaendelea kwa miaka mingi kwa njia ya kutumbuzi wa nyimbo na muziki, ambao umepata kupendwa sana katika ulimwengu wa wadogo na hata kwa watu wazima.Hiyo yote ni kutokana na nyimbo zao rahisi na zenye busara, wakiimba kwa namna ya utulivu ambao ni muhimu kwa wote hasa katika familia zile zenye majaribu ya matatizo na mateso. 

Baba Mtakatifu amewahimiza waendelee na safari yao katika kuimba thamani ya kweli ya maisha; kwa njia ya nyimbo wasifu na kushukuru Mungu kwa yote anayotujalia. Katika kipindi cha Majilio, ya  maandalizi ya kuzaliwa kwa Bwana, nyimbo zao zinazohusu majilio ya kuzaliwa kwa Yesu, zinaweza kuwasaida wale wanaosikiliza na kutambua upendo na mshangao wa kile kilichotokea huko Betlehemu mika 2,000 iliyopita. Mungu aliyefanyika mwana, ili kuweza kuwa karibu na binadamu wa kila nyakati, kumuonesha  huruma yake isiyokuwa na kikomo.

Baba Mtakatifu mara baada ya hotuba yake kwa wadogo hao amewaomba wakae mahali walipo kwa utulivu na kutazama Maria anayesubiri mtoto Yesu, kwamba hata sisi tunasubiri Yesu ili aje katika mioyo yetu. Na kwa njia hiyo wamesali sala ya Salamu Maria…..

Salam Maria..... 

Na baada ya sala amesema kila wakati tunapokuwa na shida, huzuni au matatizo yoyote kama vile magonjwa, tutazame Maria ambaye anafundisha kusubiri Yesu, na Yesu anakuja daima. Lakini inahitaji uvumilivu kama yeye alivyovumilia katikati ya  matatizo makubwa ya kumsubiri na kupokea Yesu. Amewabariki.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican 
 
All the contents on this site are copyrighted ©.