2017-12-06 15:49:00

Papa:Wakati ujao wa bara la Asia si kwa watengenezao silaha bali undugu!


Ndugu zangu, leo hii ninapendelea kuwasimulia ziara ya kitume ambayo nimeifanya  siku zilizopita nchini Mynamar na Bangladesh. Imekuwa ni zawadi kubwa kutoka kwa Mungu na hivyo ninamshukuru kwa kila jambo, kwa namna ya pekee ya mikutano niliyofanya huko. Ninarudia kutoa shukrani za dhati kwa viongozi wa nchi zote mbili, ikiwa ni pamoja na maaskofu kwa kazi kubwa ya maandalizi na mapokezi yangu na wale nilioambatana nao. Asante  pia iwafikie watu wa Birmania na wale wa Bengali ambao wameonesha imani  na upendo mkubwa Asante!

Ni maneno ya utangulizi wa Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Katekesi ya Jumatano tarehe 6 Desemba 2017 katika ukumbi wa mwenye heri Paulo wa VI, kwa mahujaji wote waliofika katika ukumbi huo. Katekesi  yake imetanguliwa na somo la kutoka Injili Mt 5,13-16, ni katika sehemu isemayo “nyinyi ni chumvi ya dunia, lakini ikikosa radha yake utupwa nje  na kukanyagwa na watu”.

Akiendelea na kuelezea ya ziara yake anasema, kwa mara ya kwanza Kharifa wa mtume Petro alitembelea nchi ya Myanmar muda kidogo, mara baada ya kuwa na mahusiano ya kidiplomasia ya nchi hiyo na Vatican. Kwa maana hiyo, anasema,naye alitaka kuoenesha ukaribu wa Kristo na wa Kanisa kwa watu ambao wameteseka kutokana na  migogoro na ghasia, pamoja na kwamba, sasa wanaendelea kidogokidogo  kurudia hali mpya ya huru na amani. Ni watu ambao, sehemu kubwa ni wabudha,wenye mzizi mkuu na misingi yake, kiroho na kimaadili. Ni nchi ambayo wakristo wanawakilisha zizi dogo na chachu ya ufalme wa Mungu. Kanisa hili hai na lenye uchachu, Baba Mtakatifu anaongeza, ameweza kuimarisha imani na umoja wakati wa kufanya  mikutano na maaskofu wa nchi na katika kuadhimisha Ekaristi Takatifu.

Maadhimisho ya kwanza yalifanyika katika uwanja wa mpira huko Yangon. Injili ya siku hiyo ilikumbusha kuwa, mateso juu ya sababu ya imani ya Kristo ni mtindo wa kawaida kwa wafuasi wake, ni kama fursa ya kuhushudia; pamoja na  hayo hata Yesu mwenyewe anathibitisha kuwa, “hakuna hata unywele mmoja utakao potea”( Lk 21,12-19). Misa ya pili ikiwa ni sehemu yake ya mwisho nchini  Mynamar, ilikuwa ni kwa ajili ya Vijana: Baba Mtakatifu anasema, hiyo ni  ishara ya matumaini na zawadi maalumu ya Bikira Maria,iliyofanyika katika Kanisa Kuu linaloitwa kwa jina lake. Kutazama nyuso za vijana hao waliojaa furaha, Baba Mtakatifu anasisitiza, aliona maisha endelevu ya Bara la Asia:Lakini maisha endelevu ambayo si kwa yule anaye tengeneza silaha, bali yule anayepanda mbegu za kindugu. Vilivile ,na ili iweze kuwa  ishara ya matumaini daima, aliweza kubariki mawe ya  kwanza ya  makanisa  16 na ya jjenzi wa Seminari na Ubalozi .

Pamoja na kukutana Jumuiya Katoliki, aliweza pia kukutana na viongozi wakuuu wa nchi ya Myanmar,ili kuwatia moyo katika juhudi  za ujenzi wa amani ya nchi, na kuwatakia matashi mema hata  viongozi wote wa nchi. Kuwahimiza juu ya ulinzi na utetezi wa watu na kwamba  hasiwepo hata mmoja wa kuhisi kubaguliwa, bali waweze kushirikiana  katika mchakato wa kuheshimiana. Kwa roho hiyo, Baba Mtakatifu anaongeza kusema, alipendelea kukutana na wawakilishi wa jumuiya mbalimbali za dini  zilizomo katika nchi. Kwa namna ya pekee ya Baraza Kuu la wamonaki wa Kibudha, mahali ambapo alionesha sifa ya wabidha kutoka kwa  Kanisa kutokana na  kutunza utamaduni wa kale wa kitasaufi na imani ambayo, anasema kuwa wakristo na wabudha kwa pamoja wanaweza kusaidia binadamu aweze kupenda  Mungu na jirani, kwa kupinga migogoro na ghasia na kupinga ubaya katika kukuza wema .

Baada ya kuacha nchi ya Mynamar, Baba Mtakatifu  aliekea nchi ya Bangladesh mahali ambapo jambo la kwanza mara baada ya kufika, lilikuwa ni kwenda kutoa heshima kwa mashujaa waliotetea uhuru  na Baba wa Taifa hilo. Sehemu kubwa ya watu wa Bangladesh ni  dini ya Kiislam, kwa namna hiyo, akifuata njia ya mtangulizi wake Mwenye heri Paulo VI na Mtakatifu Yohane Paulo II anasema, kwa nchi hiyo wamepiga hatua kubwa katika mchakato wa  njia ya kuheshimiana na mazungumzo kati ya wakristo na waislam.

Katika mkutano huo, aliwakumbusha viongozi wakuu wa nchi kwamba, Vatican imekuwa nao bega kwa bega,  tangu mwanzo wa utashi wa Wabengali  kuwa   huru, hata katika mahitahi ji ya dharura na  katika utetezi wa uhuru wa dini. Na hivyo kwa namna ya pekee alipenda kuonesha mshikamano kwa nchi ya Bangladesh katika shughuli ya kuwasaidia wakimbizi wa Rohingya ambao ni wimbi kubwa katika maeneo ya nchi hiyo, yenye idadi kubwa tayari ya watu katika dunia.

Misa iliyoadhimishwa katika uwanja wa kihisoria huko Dhaka ilitajirishwa na utoaji wa Daraja Takatifu la Mapdre kumi na sita,  hiyo ilikuwa ni tukio mojawapo la maana na furaha ya safari hiyo. Baba Mtakatifu anaongeza; kwa hakika katika nchi ya Bangladesh kama vile Myanmar na chi nyingine za Asia ya kusini mashariki, shukrani kwa Mungu miito haikosekani, ni ishara ya jumuiya hai, mahali ambapo bado sauti ya Bwana inasikika ya  kuita na kufuatwa!

Eneo hilo Baba Mtakatifu alishikirishana kwa furaha na Maaskofu wa Bangladesh na kuwatia moyo katika shughuli zao za ukarimu na ukaribu  kwa familia , maskini, elimu , mazungumzo na amani ya kijamii. Alishirikishana pia furaha hiyo na mapadre, watawa, kama vile hata waseminari, manovisi, ambapo anathibitisha kuwa hao ni vichipukizi vya Kanisa katika nchi hiyo!

Katika Mji mkuu wa Dhaka Baba Mtakatifu anasema, aliishi kipindi cha nguvu katika mkutano wa viongozi wa kidini na kiekumene, anbao waliomwezesha aweze kusisitiza juu ya kufungua mioyo,  ambayo anasema ni msingi wa utamaduni wa makutano na mani . Zaidi alitemblea Nyumba ya Mama Teresa wa Kalkuta , mahali ambako yeye alikuwa akipumzika wakati akiwa katika ziara ya mji huo. Nyumba hiyo inakaribisha watoto  yatima wengi na walemavu. Kwa mujibu wa Karama ya shirika, watawa wanaishi kila siku katika sala, kuabudu na huduma  ya Kristo kwa njia ya maskini na anayeseka. Lakini Baba Mtakatifu anathibitisha kuwa, pamoja na huduma hiyo,  hawakosi kamwe kutabasamu: ni watawa wanao sali sana, wanahudumia watu wanaoteseka na kuendelea kutabasamu.Huo ni ushuhuda mzuri, anawashukuru sana watawa hao!

Tukio la mwisho Baba Mtatifu anasema, ilikuwa ni kukutana na vijana wa Bangladesh, wenye utajiri wa ushuhuda , nyimbo na ngoma. Jinsi gani wanacheza vizuri ! Amewasifu!. Na ilikuwa ni sikukuu iliyo onesha furaha ya Injili katika kupokelewa na utamaduni ule. Furaha ambayo inatokana na sadaka nyingi za wamisionari wengi, makatekista wengi na wazazi wakristo. Kati ya vijana hao, walikuwapo hata vijana wa kiislam na hata madhehebu mengine ya kidini: hiyo ni ishara ya matumaini kwa nchi ya Bangladesh, bara la Asia na katika dunia nzima.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

 

 
All the contents on this site are copyrighted ©.