2017-12-04 16:32:00

Papa ameweka maua ya mawaridi katika Kanisa Kuu la Mama Maria Mkuu Roma!


Jumapili tarehe 3 Desemba asubuhi, Baba Mtakatifu amekwenda katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu kutoa shukrania kwa Mama Maria, baada ya ziara yake nchini Mynamar na Bangladesh. Katika Kikanisa Kidogo mahali ambapo kuna Picha ya kuheshimu Mama Maria, mama wa watu wa Roma, Baba Mtakatifu ameweka altareni mawaridi meume na njano, kamaishara ya shukrani kwa ulinzi wa safari yake, kwenda na kurudi mjini Vatican. Aliwasiri uwanja wa kimataifa wa ndege Fiumicino saa 3. 40 masaa ya Ulaya.

Wakati yuko safarini kurudi Roma Baba Mtakatifu Francisko ametuma telegramu kwa Marais wa nchi alizokuwa akipitia akiwa angani. Kwa namna ya pekee rais wa Jamhuri ya Bangladesha Bwana Abdul Hamid na watu wote wapendwa wa nchi. Baba Mtakatifu amerudia kutoa shukrani kwa ukarimu kwa  mapokezi mema aliyoyapata wakati wa ziara yake, anathibitisha kuendelea kuwakumbuka  katika sala, na kuwatakia baraka za Mwenyezi Mungu ili waendelee kuwa na umoja na matarajio mema ya nchi.

Na ndiyo mtashi mema ya  maelewano  kwa wazalendo wa nchi za Turkmenistan, Bosnia na Erzegovina, katika telegramu za marais wa nchi hizo ambao ni Gurbanguly Berdimuhamedow na  Dragan Čovič. Aidha  Ustawi na amani ndiyo baraka aliyoomba kwa mwenyezi Mungu kwa ajili ya nchi y ’India  katika telegramu aliyomtumia rais Ram Nath Kovind, wakati  huohuo rais wa Pakistan,Bwana Mamnoon Hussain amemtakia baraka zenye wingi wa maelewano na nguvu ya nchi .

Na ndiyo pia zawadi ya nguvua na  maelewano alioomba kwa Mungu kwa nchi ya Georgia katika telegramu aliyomtumia Rais wa nchi Giorgi Margvelashvili. Wingi wa zawadi na neema ya nchi aliyomwamba Mwenyezi Mungu kwa ajili ya nchi ya Afghanistan na Uturiki katika telegramu aliyowatumia marais hao ,Ashraf Ghani  na Recep Tayyip Erdoğan. Maelewano na amani ndiyo matashi ya Baba Mtakatifu kwa Mungu kwa ajili ya nchi ya Azerbaigian katika telegramu kwa rais wa nchi Bwana Ilham Aliyev na watu wote wa nchi. Kwa wazalendo wa nchi ya  Bulgaria na Rais wake Bwana, Rumen Radev, Baba Mtakatifu anaomba Baraka kwa Bwana na kuthibitisha  sala zake na hata kwa nchi za  Serbia na  Croazia, akiwaandikia marais wa nchi hizo, Aleksander Vučič na Kolinda Grabar-Kitarovič.

Mwisho telegramu yake kwa Rais wa Jamhuri ya Italia Bwana Sergio Mattarella ambaye amemsimulia juu ya mkutano wake  na watu ambao wako katika mchakato wa ujenzi wa maisha rahisi ya kijamii inayoheshimu haki na ufunguzi wa mazungumzo kwa wote. Baba Mtakatifu anamtuma baraka kwa nchi ya Italia ili walendelee kuwa wajasiri katika nia za mshikamano na walibaguliwa katika jamii na wale walio wadhaifu.

Pamoja na hayo Rais wa nchi ya Italia, amemjibu telegramu yake kwa maneno ya kirafiki na kusema kuwa, hija yake katika Bara la Asia italeta matunda na mwangwi katika nchi hizo ambazo zimempokea kwa shangwe. Na kwamba anao uhakika kuwa maneno yake juu ya kuhamasisha mazungumzo, maelewano na hata ushuhuda wa kuwa karibu kwa upendo wa Kanisa  ni mambo ambayo yamewafikia wengi na kuwa faraja ya nchi ya Myanmar na Bangladesh.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

 
All the contents on this site are copyrighted ©.