2017-12-01 08:54:00

Papa katika nchi ya Bangladesh:Ni muhimu kutatua masuala ya wakimbizi!


Katika hotuba rasmi ya kwanza ya Baba Mtakatifu Francisko alipofika  katika nchi ya Bangladesh tarehe 30 Novemba 2017, mawazo yake yamehusu wimbi la wakimbizi nchini Bangladesh wanaotoka katika Serikali ya Rakhine na Myanmar Mashariki. Ameonesha wasiwasi wake hotuba huko Dhaka katika mkutano wa viongozi wakuu wa nchi, wa kidiplomasia na jamii. Baba Mtakatifu hakuficha juu ya matatizo makubwa ya hali halisi ya wakimbzi hao, ambapo anatoa wito kwa ngazi ya Kimataifa kuingilia kati kwa dhati katika suala hili.

Hiyo ni nchi ambayo kwa mujibu wa hotuba ya Rais wa nchi ya Jamhuri Bwana Abdul Hamid alikuwa ameileza kuwa ni nchi ya  umoja wa kidini, amani na  ubinadamu katika hotuba yake kwa Baba Mtakatifu. Hata hivyo Baba Mtakatifu anakumbusha kuwa, watu hawa wamepata mahali pa kukimbilia kwa muda  pia hata mahitaji muhimu kwa ajili ya maisha. Ni mahitaji  yanatolewa kutokana na sadaka ya nchi! Na hivyo ni vitendo ambavyo vimetukia mbele ya macho ya dunia nzima, Baba Mtakatifu anathibitisha!

Akiendelea na hotuba yake anasema, hakuna yoyote hasitambue hali ngumu iliyopo, hata gharama kubwa ya mateso ya kibinadamu kwa ndugu zetu hao katika mateso na ugumu wa maisha wanayoishi, hasa wanawake na watoto waliorundikana katika makambi ya wakimbizi. Ni lazima jumuiya ya kimataifa kujikita kwa dhati katika kudhibiti  hali ngumu hii ya kipeo hicho, si tu kufanya kwa ajili ya kutoa suluhisho la masuala ya kisiasa ambayo yamesababisha wimbi la watu kuhama hivyo, lakini hata kutoa fursa za kuwasaidia zana za haraka nchini Bangladesh ambao wanafanya jitihada za dhati kwa dharura ya mahitaji ya kibinadamu.

Baada ya kukutana na Rais wa nchi na kumshukuru kwa mwaliko wa kutembelea nchi za Asia mahali ambapo walikwenda  hata Papa Paulo VI na Mtakatifu Yohane Paulo II, Baba Mtakatifu Francisko anakumbusha juhudi za nchi ya Bangladesh  kufikia umoja wa dhati wa kuwa na lugha moja na utamaduni, kwa kuheshimu na hadhi ya tamaduni mbalimbali na jumuiya, kwa njia hiyo anawapongeza kwamba kiukweli hakuna utamaduni,taifa au Serikali inaweza kuishi na kuedelea ikiwa imejitenga.

Kama familia moja ya binadamu tunahitaji kusaidiana mmoja na mwingine, hatuwezi kuishi kipekee! Katika hilo, Baba Mtakatifu anakumbuka  Rais wa kwanza wa nchi baada ya kupata huru kutengana na  Pakistan, Sheikh Mujibur Rahman kwamba Yeye alifikiri kuwa jamii ya kisasa, mchanganyiko na yenye umoja,na  kila mtu ndani ya jumuiya waweze kuishi na uhuru, amani usalama, kwa kuheshimu hadhi ya kila mtu, usawa na haki kwa wote.

Ni kwa njia ya mazungumzo na heshima ya kila utofuati wa watu inawezakana  kuleta mapatano dhidi ya migawanyiko, kushinda mitazamo potofu ya migawanyiko na kutambua udhati wa upeo wa utofauti. Hiyo ni kwasababu mazungumzo ya pamoja yanatazama upeo wa wakati ujao wa kujenga umoja katika huduma ya pamoja, kuwa makini kwa mahitaji ya wazalendo wote, hasa zaidi maskini, wale ambao kwa bahati mbaya hawana sauti.

Aidha Baba Mtakatifu Francisko amekumbusha juu ya Mkutano wa Ramna na viongozi wahusika wa kiekumene na majadiliano ya kidini, utakao fanyika tarehe 1 Desemba 2017, ili kuweza kusali na kuomba amani, zaidi kudhibitisha jitihada za pamoja kwa ajili ya amani. Kwa njia hiyo amezungumza juu ya heshima ya kweli, kukua katika hali ya mazungumzo ya kidini ambayo inaruhusu waamini kujieleza binafsi, kuwa na uhuru wa kina katika kutenda na kuamini, kutambua maana yake na juu ya lengo la maisha; vilevile kuhamasisha thamani za kiroho ambazo ndiyo msingi mkuu wa jamii ya kweli inayoongozwa na amani.

Baba Mtakatifu akiendelea juu ya dini, anasema, katika dunia hii, mahali ambapo dini daima zinatumiwa kwa misingi binafsi wa kutaka kuleta migawanyko, ushuhuda wa mapatano na umoja ndiyo lazima katika hali hiyo. Hayo ni kutokana na kukumbuka juu ya mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea mwaka jana huko Dhaka nchini Bangladesh, ambapo katika Ujumbe wa Baba Mtakatifu kwa viongozi wa wa kidini na taifa, alisema jina la Mungu haliwezi kutumiwa kwa nia ya  kusambaza chuki na vurugu dhidi ya binadamu wanaofafana. 

Aidha akitazama kwa upande wa wakatoliki nchini Bangladesh, anasema wakatoliki ni wachache lakini wanafanya kila njia kujihusisha katika nafasi ya ujenzi wa maendeleo ya nchi, hasa kwa njia ya matendo, kama vile  mashule, vituo vya afya na zahanati. Hata hivyo anathibitisha kuwa Kanisa linatoa pongezi kwa kupewa  uhuru ambao Taifa limewezesha kutoa, ili kuendelea kuonesha na kukiri imani katika kutenda shughuli zao za upendo, kati ya  shughuli hizo ni kujikita kwa ajili ya vijana ambao wanawakilisha maisha endelevu ya jamii,kuwapatia elimu yenye msingi na mazoezi adilifu ya thamani za maadili na ubinadamu.

Katika shule, Baba Mtakatifu anakumbusha kama taifa au Kanisa ni liazima kujitahidi kwa kila njia ili kuhamasisha utamaduni wa makutano ambao unasaidia wanafunzi vijana kuwa na uwezo wa kujizatiti , uwajibikaji kwanza wao binafsi, na katika maisha ya jamii. Hao ni vijana pamoja na walimu ambao siyo wakristo lakini wanaotoka katika tamaduni za dini nyingine. Baba Mtakatifu anawatakiwa matashi mema, kwamba makubaliano ya barua na roho ya katiba ya taifa, jumuiya Katoliki mahalia inaweza kuendelea kufaidika na uhuru wa kupeleka mbele matendo  msingi kwa ajili ya wema kwa wote!

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.