2017-12-01 11:08:00

Papa ametoa daraja Takatifu la Upadre kwa Mapadre 16 huko Dhaka Bangladesh!


"Hawa watoto wetu wameitwa katika daraja Takatifu.Tutafakari kwa kwa kina kuhusu utume wao watakaofanya katika Kanisa".Ni maneno ya utangulizi wa Baba Mtakatifu Francisko katika misa ya kutoa daraja Takatifu la Upadre kwa mapadre wapya 16 kutoka katika majimbo na mashirika ya kitawa. Misa hiyo imefanyika katika uwanja mkubwa wa Suhrawardy Udyan huko  Dhaka nchini Bangladesh tarehe 1 Desemba 2017 akiwa katika hatua yake ya pili ya ziara ya kitume barani  Asia.

Katika mahubiri yake anasema, Bwana Yesu ni kuhani, na  Mkuu wa Agano jipya lakini pia hata watu watakatifu wa Mungu ambao pia wamewekwa kuwa makuhani. Na si kwa bahati mbaya kati ya mitume wake, Bwana Yesu alitaka kuchagua miongoni mwao wengine kwa namna ya pekee, ili waweze kutenda wazi katika Kanisa kwa jina lake shughuli ya kikuhani kwa watu wote na kuendeleza fumbo lake la  utume wa  kikuhani na kichungaji. Kama yeye alivyotumwa na Baba, ndivyo naye anafanya katika  ulimwengu kwa kuanzia na Mitume, baadaye maaskofu wafuasi wao na mwisho kuwapatia wasaidizi ambao ni mapadre ili kuungana na utume wa kikuhani unaojieleza katika kutoa huduma kwa watu wa Mungu.

Akiwalenga mapadre wateule anasema, kwa kupewa daraja la kikuhani wao watatenda utume Mtakatifu katika mafundisho na kushiriki katika utume halisi wa Kristo mmoja na Mwalimu. Wataweza kutangaza Neno la Mungu ambalo wao binafsi wamepokea kwa furaha. Wasome Neno la Bwana bila kuchoka kwa kuamini walichokisoma , kufundisha walichopokea katika imani na kuishi kile ambacho wanafundisha. Mafundisho yao yawe chakula kwa watu wa Mungu na mafundisho yawe ya furaha na msingi kwa waamini wa Kristo, arufu nzuri ya maisha yao iwe kwa maneno na mifano katika ujenzi wa nyumba ya Mungu ambayo ni Kanisa.

Waendelee na utume wa utakatifu wa Kristo kwa njia  ya fumbo la sala ya kiroho kwa waamini ambao watakabidhiwa , ili sadaka ya Kristo kwa mikono yao na kwa jina la Kanisa, itolewa kwa namna ya ukarimu katika altare ya maandhimisho ya mafumbo matakatifu.
Badaya ya mahubiri ya Baba Mtakatifu, imefuata hatua ya kutoa daraja takatifu akiwalika mapadre watarajiwa kufuata mfano wa Mchungaji mwema, ambaye hakuja kwasababu ya kutumikiwa bali kutumikia.

Na kwa waamini wote amesema , anatambua walivyofika katika sikukuu hiyo kubwa ya Mungu kwa ajili ya daraja la upadre kwa makuhani wapya, na jinsi gani wametoka sehemu mbali sana kwa kutembea siku nyingi. Na kwa njia hiyo anawashukuru kwa ukarimu huo, kwasababu anasema,inaonesha upendo walio nao wa Kanisa na kuonesha upendo walio nao kwa ajili ya Yesu. Amewashukuru kwa uaminifu huo na waendelee mbele na moyo wakuwa na heri, pia  kusistiza wasali kwa ajili ya mapadre wao hasa hao waliopokea daraja Takatifu.

Baba Mtakatifu anasema, watu wa Mungu wanawasaidia makuhani katika maombi na hivyo ndiyo wanao wajibu wa kuwasaidia makuhani. Je ni kwa njia gani? Ni kwa njia ya ukarimu! Moyo wa ukarimu walio nao utawapatia msaada mapadre wao, lakini msaada wa  kwanza kwa ajili ya mpadre ni ule wa maombi anathibitisha! Na hivyo wasichoke kusali kwa ajili ya mapadre, kwa maana anatambua kuwa watafanya hivyo!

Imekuwa furaha kubwa katika Kanisa dogo la Bangladesh , baada ya miaka 31 moja tangu Mtakatifu Yohane Paulo II alipoadhimisha misa ya kutoa daraja takatifu kwa baadhi ya mashemasi wa Golden Bengal katika hatua  ya ziara yake ya kitume nchini humo. Mwaka 1989 walikuwa mashemasi vijana 18 na ilikuwa ni maadhimisho hayo tu ya wazi katika mji wa Dhaka iliyoongzwa na nyimbo za Kibengali. 

Na kwa upande wa Baba Mtakatifu Francisko ametoa daraja Takatifu la mapadre wateule 16 ambao 10 wakiwa ni mashemasi kutoka katika jimbo na  mashemasi 6 kutoka katika mashirika ya kitawa, mbele ya waamini zaidi ya mia moja elfu katika uwanja wa  Suhrawardy Udyan. Uwanja ambao zamani ulikuwa ni club ya wanajeshi wa Kingereza na baadaye uwanja wa michezo. Vijana wameweza kulala kufudifudi katika jukwaa la altare rahisi wakati wa kuimba litania ya watakatifu, na jukwaa hili limetengenezwa kwa miti ya mianzi na majani.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.