2017-12-01 17:00:00

Papa ameshiriki Mkutano wa Madhehebu ya kidini na Kiekumene kwa ajili ya amani!


Mchana wa tarehe 1 Desemba 2017 Baba Mtakatifu amekutana na viongozi wa madhehebu ya kidini kwa ajili ya amani katika makao makuu ya Askofu wa Dhaka nchini Bangladesh. Katika hotuba yake, kwa wawakilishi  kutoka katika jumuiya mbalimbali za kidini za nchi hiyo amesema, ni fursa kwa mtazamo wa nchi ya Bangladesh ili kuweza kujikita katika tafakari ya urafiki wao na kuonesha matashi yao mema hasa ya zawadi ya amani kamili na ya kudumu.
Shukrani kwa Kardinali  D’Rozario kwa hotuba yake, kwa makaribisho ya furaha kwa jina la jumuiya ya waislam, wahindu, wabudha n,hata kwa viongozi wa madaraka ya kiraia. Anamshukuru pia Askofu wa Kianglikani wa Dhaka kwa uwepo wake na jumuiya nyingine za kikristo, wakiwemo hata wadua mbalimbali waliochangia kufanikisha mkutano huo.

Nyimbo na ngoma zilizotumbuizwa anasema, zimewezesha kuchangamsha makutano hayo, ambazo zinajieleza kwa namna ya pekee ya utashi wa umoja, undugu  na amani katika mafundisho yaliyomo kwa kila dini duniani. Mkutano huo anaongeza, unaweza kuwa kweli ishara ya juhudi kwa viongozi na wafuasi wa madhehebu mengine ya dini yaliyomo katika nchi hiyo, kuishi kwa pamoja katika kuheshimiana na matashi mema.  Nchi ya Bangladesh hawali ya yote ni mahali ambapo haki  na uhuru wa dini ni msingi wa kwanza, huo  ndiyo wito wa kuheshimu, lakini pia hata kupambana na yule atakayetaka kuzusha mgawanyiko, chuki na vurugu kwa jina la dini.

Ni ishara kubwa ya matumaini katika nyakati zetu, ambazo waamini na watu wenye mapenzi mema wanataka kuitikia katika kushirikiana kwenya mafunzo ya utamaduni wa makutano, mazungumzo na kushirikiana katika huduma ya familia ya kibinadamu. Yote haya yanahitaji hasa uvumilivu wa kweli. Uvumilivu huo  unaweza  kuwa na tabia ya kuchukuliana kwa pamoja, kuwa na imani, uelewa kwa kujenga umoja na kwa kutambua kuwa utofauti siyo tishio, bali ni nguvu na kisima cha utajiri na kukua kwa pamoja!

Wote wanaalikwa kujenga aina ya ufunguzi na kupanua mioyo, kwa maana ya kuwaona wengine kama njia ya upamoja na si kama vizingiti.
Baba Mtakatifu akifafanua zaidi juu ya aina msingi ya kufungua mioyo ambayo ni tabia ya utamaduni wa makutano amesema: hawali ya yote ni kama mlango aambayo  siyo wa kutoa historia za abunuasi, bali ni uzoefu halisi wa kushi. Hiyo inasaidia kutambua vema mazungumzo ya maisha, si tu kubadilisha mawazo bali uthabiti wa kuishi ki ukweli. Kwa maana inahitaji utashi mwema wa mpyo katika , kukaribisha, si katika kuchanganya na tofauti au katika kuelezea kile ambacho unaamini kwa kina. Ni kwa njia ya kujikita kwa kina kuwa na  mwingine, maana yake ni kushirikishana uraia na utofauti wa kidini,na kiutamaduni, lakini zaidi kwa njia ya unyenyekevu, uaminifu na kuheshimiana. Kwa kufanya hivyo inakuwa ni  ishara wazi ya kchukuliana na kuthaminiana na wengine kwa kila hali ya maisha ikiwa ni dini, lugha, kabila na yote . Na ndani yake ipo hekima na nguvu muhimu za kuonesha mshikano kuwasaidia wengine kwa dhati.

Kuwa na moyo uliofunguka ni kujionesha katika  kupokea na kukaribisha, kushikishana kati ya waamini na zaidi katika kuchangia kwenye utamaduni wa umoja, maelewano, ambayo ynatoa msukumo ndani ya moyo. Baba Mtakatifu anasisitiza kusema, jinsi gani dunia hii inahitaji moyo unao dunda kwa nguvu  ili kipinga virusi vya rushwa kisiasa, itikadi kali za kidini zinazoharibu, vishawishi vya kufunga macho mbele ya mahitaji ya wengine kama vile ya maskini, wahamiaji na makundi madogomadogo ya watu katika ulimwengu, kwa namna ya pekee kwa vijana ambao mara nyingi wanahisi upweke, wakitafuta maana ya kweli ya maisha. 

Amemalizia awashukuru kwa jitihada zao za kuhamasisha utamaduni wa makutano na kuomba kuwa, maonesho ya juhudi za pamoja za wafuasi wa dini katika kung’amua mema na kujikita katika vitendo vya dhati ili waweze kuwasaidia waamini wakue kwa hekima na utakatifu, kwa kushirikiana katika ujenzi wa dunia ya kibinadamu na umoja.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.