2017-11-30 16:41:00

Matokeo ya Ziara ya Papa Myanmar:Serikali imetangaza Mkutano wa makabila !


Kama matokeo ya ziara ya Papa Myanmar, Serikali ya Birmania, imetangaza  kuitisha Mkutano wa tatu na makabila madogomadogo, kama mwendelezo wa juhudi za kusitisha uhasama kati ya serikali na makundi madogomadogo ya kikabila na kidini .  Mkutano huo ujao wa Pinglong, utafanyika katika wiki la mwisho la Mwezi Januari.  Kwa zaidi ya miaka 60, makundi madogomadogo yamekuwa yakiendesha  mashambulizi katika taifa hilo.  

Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya kuwasili Myanmar, alikutana na Mkuu wa Jeshi la Myanmar , Jenerari Min Aung Hlaing katika makao ya Askofu Mkuu wa Yangon. Kiongozi huyo wa Kijeshi alimthibitishia  Papa kwamba, hakuna ubaguzi wa kidini au ukabila katika nchi yake. Na Serikali ilikwisha weka sahihi katika hati ya makubaliano ya kusitisha mapigano dhidi ya vikundi vinane vyenye sialaha, ambavyo ni vikundi vya kikabila.

Habari inataja kwamba, kati ya vipengere vitakavyojadiliwa katika Mkutano wa Januari ni pamoja na Matazamio na nafasi za kusonga mbele katika majadiliano ya kisiasa , katika ngazi ya kitaifa na vikundi husika kati yake likiwemo kabila dogo la Shan na vikundi vya Kiislamu. Shirika la Kikristo lilieleza hili katika taarifa yake iliyopelekwa.

Thabita J. Mhella

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.