2017-11-30 12:20:00

Baba Mtakatifu amefika nchini Bangladesh na kupokelewa na Rais wa nchi!


Baba Mtakatifu Francisko amefika nchini Bangladesha ikiwa ni hatua ya pili ya ziara yake ya kitume barani Asia. Safari yake imeanza saa moja na dk. 55 asubuhi masaa ya Ulaya na kufika nchini Bangladesh kabla ya saa nne katika Uwanja wa kimataifa wa Dhaka. Uwanjani amepokelewa na Rais wa Jamhuri ya Bangladesh Bwana Abdul Hamid na baadhi ya viongozi  wa nchi na maaskofu wa Bangladesh. Kama utamaduni imefuatia  ngoma na chereko za kiasili kutoka kwa baadhi ya watoto pia wakiwa na mataji ya maua.

Badaya ya sherehe za mapokezi atatembelea Jumba la Makubusho huko Savar mahalia ambapo Baba Mtakatifu Francisko atatoa shahada la maua  katika kaburi la Baba wa Taifa Bangabandhu. Hapo hatahutubia viongozi wa nchi, raia na wakidiplamasia.

Kabla ya kuondoka nchini Myanmar, Baba Mtakatifu ametoa ujumbe wa shukrani kwa Rais wa nchi ya Mynamar Bwana Htin Kyaw, mahali ambapo Baba Mtakatifu anawashukuru na kuwsifu Taasisi zote za raia na watu wapendwa wa nchi hiyo kwa ukarimu wao na makaribisho mema aliyopokea. Na mwisho amewabariki nchi zima na kuwahikishia maombi yake kwa ajili ya amani na umoja wa nchi.

Kabla ya kuaga  Myanmar kulekea Bangladesh, Baba Mtakatifu ametoa zawadi katika nyumba ya Askofu Mkuu alipokuwa amekaribishwa, sanamu ya Mtakatifu Francisko,wa Asizi inayoonesha akiwa anahubiri ndegu. Hii ni ishara ya undugu kati ya binadamu na viumbe vyote.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©.