2017-11-29 15:13:00

Papa ameadhimisha Misa Takatifu huko Kyaikkasan Yangon kwa maelfu ya watu!


Kabla ya kufika katika nchi hii, nimekuwa natamani ifike haraka siku kama ya leo. Ninatambua kwamba  wengi wenu wamesafiri kutoka sehemu mbalimbali na mbali sana na wengine kutembea kwa miguu kutoka hata milimani. Nimefika kama mhujaji ili kusikia na kujifunza kutoka kwenu na ili nipate kutoa maneno machache kwenu ya matumaini na faraja.  Ni maneno ya utangulizi wa Baba Mtakatifu Francisko wakati wa maadhimisho ya Misa Takatika katika uwanja wa Kyaikkasan hukoYangon nchini Myanmar tarehe 29 Novemba 2017, ikiwa ni fursa ya pili kuongea na umati wa namna hii akiwa nchini Myanmar.

Somo la kwanza kutoka katika kitabu cha Danieli, kinasaidia kuona kizingiti cha hekima kwa upande wa mfalme Belshaza na matokeo ya mkono wa mwanadamu. Wao walikuwa wanatambua jinsi ya kusifu miungu ya dhahabu, fedha, shaba, chuma,  miti na ya mawe (Dn 5,4), lakini wakati huohuo hawakuwa na hekima ya kusifu Mungu ambaye kwa mikono yake ndiye maisha na pumzi yetu. Kwa bahati nzuri  Danieli alikuwa na hekima ya Bwana na uwezo wa kutafsiri fumbo lake kuu.

Mtafsiri wa utimilifu wa mafumbo ya Mungu ni Yesu: Yeye binafsi ni hekima ya Mungu  (Taz:1 Cor 1,24). Yesu hakufundisha hekima yake kwa njia ya hotuba nyingi na ndefu au kwa njia ya kujionesha katika uwezo wa kisiasa na utawala wa ardhi, Yeye ajionesha katika kutoa maisha msalabani. Baba Mtakatifu anaongeza, wakati mwingine tunaweza kuingia katika mtego wa kujiaminisha na  hekima yetu binafsi, lakini kiukweli ni rahisi kupoteza maana ya mwelekeo huo. Na kwa njia hiyo,  tunapogundua kuwa tumepoteza  ndipo unakuja  ulazima wa kukumbuka kuwa tunaweza kujiaminisha mbele ya Bwana wetu msalabani. Ni katika msalaba sisi tunapata hekima ambayo inaweza kuongoza maisha yetu kwa mwanga utokao kwa Mungu.

Katika msalaba  kuna hata uponyeshwaji: Katika Msalabani Yesu alitoa majeraha yake kwa Baba kwa ajili yetu na ni katika majeraha yake, sisi wote tumeponywa (taz: 1 Pt 2,24). Baba Mtakatifu ameongeza kusema, tuombe ili tusikose daima kupata hekima hii kutoka katika majeraha ya Kristo, kisima cha uponyaji. Na akiongeza kufafanua kuhusu majerah amesema kuwamba, anatambua kuwa watu wengi wa nchi ya  Myanmar wanabeba majeraha ya migogoro na mateso yanayo onekana na yasiyo onekana. Na kwamba kishawishi kinaweza kujitokeza kuwa jibu la kutoa kuhusu majanga haya ni kwa njia ya kiulimwengu kama alivyofanya mfalme Belshaza, kwa maana alikuwa amedekezwa kwa kina. Hivyo wengine wanaweza kufikiria kuwa ili kuweza kuponywa, ni kuwa na hasira na kulipiza visasi, wakati huohuo kulipiza visasi haikuwa njia ya Yesu. 

Njia ya Yesu daima ilikuwa nitofauti na njia ya binadamu, wakati yeye anachukiwa na kukataliwa na watu wake hadi mateso na mwisho kifo msalabani, Yeye, alijibu kwa msamaha na upendo. Katika Injili ya siku inaeleza kuwa kama alivyo fanywa Yeye, hata sisi tunaweza kukutana na kukataliwa na vizingiti, lakini Yeye  anatupatia hekima ambayo hakuna awezaye kuishinda (Taz Lc 21,15) .Yesu amazungumza juu ya Roho Mtakatifu ambaye kwa njia ya upendo wa Mungu imejikita ndani ya mioyo yetu (taz Rm 5,5). 

Kwa njia ya zawadi ya Roho Mtakatifu sisi sote tunafanywa kuwa na  uwezo wa kuwa ishara ya hekima yake ambayo inashinda hekima zote za dunia hii, katika uruma yake,inayotoa faraja katika majeraha ya kuumiza. Katika mkesha wa mateso yake, Yesu alijitoa kwa mitume wake kwa namna ya pekee katika mkate na divai. Katika zawadi ya Ekaristi, hatutambui kwa macho ya imani na zawadi ya mwili wake na damu yake tu  bali hata kujifunza namna ya kupumzika katika majeraha yake na kutaswa dhambi zetu zote , na njia zetu mbaya. Ni lazima kukimbilia katika majeraha yake Kristo  ili kuweza kuonja dawa kweli ya kuponyesha ambayo ni huruma ya Baba. Na tunaweza kupata nguvu katika  kuchukuliana na wengine, kuwapaka mafuta wengine waliojeruhiwa na kila kumbukumbu ya uchungu. Kwa maana hiyo wote watakuwa waamini mashuhuda wa mapatano na amani ambayo Mungu anataka itawale kwa kila moyo wa binadamu na kila jumuiya .

Aidha Baba Mtakatifu anasema kuwa: anatambua Kanisa la Myanmar linajikita kwa kina katika kupeleka msaada wa wa huruma ya Mungu kwa wengine, haswa wenye kuhitaji. Zipo ishara wazi hata  katika zana dhaifu lakini jumuiya nyingi zinatangaza Injili kwa makabila mengi kwa njia ya matendo, bila nguvu au kulazimisha, lakini kwa kuwaalika  wote katikakati ya umaskini na matatizo ya wengi wanaoteseka, na kutoa huduma yao bila kujali rangi, dini au ukabila.

Kwa njia ya uangalizi wa maakofu, mapadre, watawa, makatekista, kwa namna ya pekee ya kazi ya chama Katoliki cha Karuna nchini Mynamar, pia msaada kutoka katika Baraza la Kipapa kwa ajili ya Kazi za kimisionari ambapo kama Kanisa nchini Myanmar wanasaidia watu wengi,  wakiwemo idadi kubwa ya wanaume,wanawake, watoto, bila ubaguzi wowote. Baba Mtakatifu anasema, kwa namna hiyo anaweza kushuhudia kwamba Kanisa lao ni hai kutokana na Kristo aliye hai kati yao kwenye  jumuiya zote za kikristo, na kwa njia hiyo anawatia moyo waendelee kushirikiana.  Na Bikira Maria aliye mfuata Yesu katika giza la mlima  wa Kalvario awasindikize katika hatua hizo,ili daima waweze kuwa daima wajumbe wa hekima, na huruma ya kina  kwa  wote wenye kuhitaji na wawe na furaha itokayo na kupumzika katika majeraha ya Yesu aliyetupenda hadi mwisho.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.