2017-11-27 09:49:00

Papa amewasili nchini Myanmar na kupokelewa kwa shangwe kubwa!


Baba Mtakatifu ametua uwanja wa ndege wa Yangon nchini Myanmar kabla ya saa mbili asubuhi masaa ya Ulaya, wakati nchini myanmar  ilikuwa ni saa 7.22 mchana. Hivyo ndiyo ziara yake ya 21 ya Kitume ambayo pia ataendelea nayo katika nchi ya Bangladesh. Baada ya kutua uwanjani ,ndani ya ndege amepokelewa na Balozi wa Vatican, Askofu Mkuu Paul Tschang In-Nam na Kiongozi wa Protokali.

Rasmi nje ya ndege katika uwanja wa Yangon Papa alikuwa anasubiriwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya nchi Bwana  Htin Kyaw, Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Myanmar na mamia ya watoto na makundi mbalimbali ya asili wakiwa na mavazi ya utamaduni.
Ratiba ilikuwa inaonesha  guaride la heshima kwa ajili ya Papa bila hotuba. Kwa njia hiyoPapa amekwenda moja kwa moja katika makao makuu ya askofu wa Yangon ambaye atakuwa mwenyeji wake kwa kipindi chote atakachokuwa nchini Myanmar. Baada ya misa ya faragha,Papa  anatarajia kupata mlo wa jioni.

Na zira ya 21 ya Kimataifa ya Baba Mtakatifu ilianza kutoka Katika Uwanja wa kimataifa wa Leonardo da Vinci saa nne za usiku masaa ya Ulaya   tarehe 26 Novemba 2017 kuelekea uwanja wa kimataifa wa Yangon nchini Myanmar kwa ndege ya ('Airbus A-330)  Alitalia. Akiwa na mkoba wake mweusi kama kawaida yake , amesalimia badhi ya viongozi wa nchi na wakijeshi, hata wa dini na kupanda ndege tayari kwa safari yake. Ndani ya ndege amewapungia mkono kwa ishara ya salam wasafiri wote wanaoongozana naye katika ziara hiyo.

Aidha wakati akiwa njiani , amewatuma ujumbe wa salam  kwa njia ya telegram kwa nchi zote ambazo alikuwa anapitia, kuanzia kwa Rais Matarella wa nchi ya Italia. Na ujumbe wake anasema kuwa, anasali kwa ajili ya watu wa Italia ili waweze kuwa na mtazamo daima wa imani na matumaini endelevu, katika ujenzi wa mema kwa wote na hasa kujikita katika umakini kwa wenye shida na wazalendo wote. Aidha anasema anayo shahuku kubwa ya kumtumia salam zake wakati anaacha Roma kulekea Myanmar na Bangladesh kama mhujaji wa amani na kuwatia moyo jumuiya ndogo katoliki yeye ari ya kijumuiya katika nchi hiyo.

Halikadhalika ametuma pia telegram na salama kwa nchi nyingine zinazopitwa na ndege angani kwa nchi za:Croazia, Bosnia na  Erzegovina, Montenegro,Serbia,Bulgaria,Uturuki,Georgia,Azerbaigian,Uturukmenistan,Afghanistan, Pakistan.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.