2017-11-24 10:43:00

Papa:Wafranciskani wafungue mioyo kwa maskini na kwa kila kiumbe!


Bwana Papa kama Mtakatifu Francisko alivyokuwa akiwaita mapapa, ninawakaribisha kwa furaha ndugu wadogo Wafranciskani wanaioshi na kufanya kazi katika ulimwengu wote. Asante kwa yote mnayotenda na hasa kwa ajili ya kuhamasisha na kujali maskini na wasio kuwa na bahati.
Ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko asubuhi ya tarehe 23 Novemba 2017 mjini Vatican, alipokutana na wajumbe wa  familia ya  ndugu wadogo wafransiskani na Utawa wa tatu wa Mtakatifu Francisko waitwao Waoservanti. Baba Mtakatifu anasema, kwa pamoja wanaitwa ndugu  wadogo kama inavyosomeka katika Kanuni ya kwanza ya Mtakatifu Francisko wa Asizi,ambapo maelezo yake hayasemi lolote juu ya neno la ndugu zake wadogo zaidi ya lile la kuonesha jambo muhimu la ujenzi wa maisha na utume. 

Kwa maana hiyo katika maisha yao ya kawaida, jambo la udogo ndilo lenye msingi mkuu wa kindugu na kujikita katika undugu unatoa maana halisi ya mtindo wake; yaani wa kukutana na ndugu wadogo katika jumuiya moja. Kwa maana hiyo, kuzungumza juu ya undugu ni lazima kufikiri vizuri uwepo wa mtindo huo wa kifransiskani katika mahusiano ya kindugu ambayo yapo katiyao yao na  ndugu wadogo wote. Baba Mtakatifu akiendelea na maana ya undugu, anasema: ni kitu gani kilifanya, Mtakatifu Francisko atumie neno hilo la  undugu kama jambo msingi wa maisha ya kindugu katika jumuiya?

Kwa kufafanua zaidi anasema: ni katika Injili ambayo ilikuwa msingi wa maisha yake na usalama wa maisha yake yote, alichota maana ya udogo, pamoja na kwamba yeye alijikita kwa kina zaidi kufanya tafakari zake za  hali ya juu na hata  kijamii, kutafakari kwa kina juu ya Mwana wa Mungu aliyejifanya mtu ,  ambaye inakusanya sura halisi ya kuwa mdogo kama mbegu. Na akitumia maneno ya Paulo Mtume wa watu anafafanua zaidi kuwa: ni mantiki ya jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake. (2Kor 8,9). Hata leo hii ni mantiki inayojikita katika kuvua,na ambayo Mtakatifu Francisko alitenda wakati wa kuvua nguo zake, hata mali zote kwa kujikabidhi moja kwa moja kwa Mungu na ndugu.

Maisha ya Mtakatifu Francisko yalijikita katika kukutana na Mungu maskini ambaye yupo hata sasa kati yetu kwa njia ya Yesu wa Nazareth: Ni uwepo wa unyenyekevu, uliojificha ambao Maskini anaabudu na kutafakari Mungu aliyejifanya mtu, katika Msalabani na katika Ekaristi. Kwa upande mwingine tunatambua sehemu nyingi za Kiinjili zilizomshangaza sana Mtakatifu Francisko,kwa mfano ile ya kuosha miguu mitume wake wakati wa karamu ya mwisho.

Nafasi ya udogo kwa wafranciskani ni njia mwafaka ya kukutana na muungano na Mungu,ni nafasi ya makutano, kuwa na umoja na ndugu wote wake kwa waume katika kila sehemu yoyote ya makuntano, hata katika kazi ya umoja wa uumbaji. Katika nafasi ya udogo ndiyo mtindo wa uhusiano na Mungu, kwa maana ya mtindo wa Mt. Francisko, binadamu hana chochocte kilicho chake zaidi ya dhambi, mbele ya Mungu ni kitu bure, kwa maana hiyo uhusiano wao  na Bwana unapaswa uwe kama wa mtoto mnyenyekevu, mamwinifu, kama  Injili inavyoeleza,na zaidi kuwa na utambuzi wa dhambi binafsi. Ametoa onyo kwa ndugu wadogo: juu ya ukiburi wa tasaufi, ukiburi wa kifarisayo na mbaya zaidi ule wa kuishi kiulimwengu.

Maneno ya Mtakatifu Francisko, yanatoa msukumo wa kujiuliza kama ndugu, je tunakwenda wapi na tuko na nani,je tunao uhusiano, na ni hakina nani ?. Lakini kama ndugu tunaitwa kuwa na udugu na kila mtu, kwa maana hiyo ni fursa ya kila mmoja kufanya tathimini juu ya mtindo wake wa maisha, matumizi,namna ya kuvaa na kila aina ya mahitaji.  Aidha amewakumbusha kuwa kila mara wanapofanya shughuli kwa ajili ya wale wadogo, waliobaguliwa na wa mwisho, waifanye kwa unyenyekevu na siyo wa kujiona, kwa maana,wafikiri wafanyavyo hivyo wanatoa kile ambacho wamepokea bure.

Akichambua zaidi juu ya barua ya wosia wa Mtakatifu Francisko wa Asizi anasema:Na hata hivyo Mtakatifu Francisko alisema katika barua yake kuwa, msiweke chochote kwa ajili yenu ! Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu anasema, watoe nafasi na kuwapokea kila mtu katika maisha yao, hasa wanaobaguliwa,wanazurura mitaani, kwenye viwanja au vituo vya treni na kuwasaidia  maelfu ya wengi wasiokuwa na kazi,vijana na watu wazima, wagonjwa wengi ambao hawawezi kupata matibabu, wazee wengi walioachwa peke yao na watu wengi wanaoshi pembezoni, hata  ukosefu hata wa mwanga wa Injili.

Amewataka wafungue mioyo yao na mikono yao kwa ajili ya wakoma katika muda wao hasa kwa dhamiri ya huruma ambayo Bwana alionesha, akianzia kwa mwanzilishi wo Mtakatifu Francisko wa Asizi. Kama yeye nao wajifunze kuwa wagonjwa kwa wagonjwa , wanaosumbuka kwa wasumbuliwa.Kwa maana nyingine kushiriki maisha ya wote wanaoteseka. Hiyo ni kuonesha maana ya uhusiano wa kina unaobadilisha mioyo na kuwafanya washiriki utakatifu wa kweli wa mwanzilishi wao.

Nafasi ya udogo ni sehemu ya kukutana na kazi ya umbaji: Kwa upande wa Mtakatifu wa Asizi, utunzaji wa mazingira ilikuwa ndiyo kitabu cha mshangao ambapo Mungu anaonesha uzuri wake. Kazi ya uumbaji ilikuwa ni kama dada na ambaye wanashiriki maisha, pia  kama mama mzuri anayepokea watoto wake kwenye mikono yake. Masikitiko ya Baba Mtakatifu anasema: Leo hii dada na mama wamebadiliaka kwasababu hawajali tena mazingira. Kwa njia hiyo, mbele ya uharibifu wa mazingira duniani, anawaeleza: kama watoto wa maskini Francisko waingilie kati katika mazungumzo na kazi ya uumbaji, kwa kutoa sauti yao, kusifu kazi ya uumbanji kama alivyokuwa anafanya Mtakatifu Francisko. Wajibidishe kwa kila njia na kutunza mazingira kwa kupingana na kila aina ya vizingiti vya mahesabu kiuchumi na sintofahamu. Washirikiane kuanzisha mipango mbalimbali kwa ajili ya utunzaji wa mazingira nyumba yetu , wakumbuke daima uhusiano uliopo kati ya maskini na udhaifu wa sayari, kati ya uchumi, maendeleo, utunzaji wa mazingira na kujali kwa kuchagua upande wamaskini.
Amemalizia maneno ya Mtakatifu Francisko wa Asizi akiwatakia wawe daima wadogo na Mungu awalinde na kuendeleza mantiki ya udogo katika jumuiya zao kindogu.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.