2017-11-21 15:46:00

Papa:Mashemasi ni watangulizi wa ustaarabu mpya wa upendo!


Mashemasi ni watangulizi wa  ustaarabu mpya  wa upendo, kama alivyokuwa anapenda kusema Mtakatifu Yohane Paulo II. Ni maelezo ya Baba Mtakatifu Francisko katika dibaji ya Kitabu chenye kichwa cha habari “ Ushemasi kwa mtazamo wa mawazo ya Papa Francesco” Kitabu hicho kinaonesha hotuba zake zote alizozitoa zinazohusiana na ushemasi tangu akiwa Askofu huko Buenos Aires Argentina, hadi hotuba zake za hivi karibuni kama kharifa wa mtume Petro. Ni kitabu kilicho andikwa na Enzo Petrolino ambaye ni Shemasi wa kudumu katika Majimbo ya Reggio Calabria- Bova, na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mashemasi wa Kudumu nchini Italia. Kitabu hicho kimewasilishwa kwenye ukumbi wa Marconi, Makao ya Radio Vatican mjini Roma.

Katika dibaji hiyo Baba Mtakatifu anasema kuwa, Kanisa linapata kielelezo cha uhai wake kutoka kwa mashemasi wa kudumu  ambao  ni sawa na ishara wazi inayoonekana ya ushemasi wa Kristo Mtumishi katika historia ya binadamu. Aidha katika dibaji hiyo anaongeza kuwa Mtakatifu Francisko wa Asizi katika  historia yake alikuwa  ni shemasi kwa maana ya kwamba, mashemasi lazima waigwe mfano wa uinjilishaji, kusali kwa ajili ya miito na mantiki msingi 

Katika dibaji hiyo pia Baba Mtakatifu anakumbusha jinsi gani utume wa ushemasi kwa Kanisa zima umekuwa ni pigo la moyo linalodunda  katika Fumbo la Ekaristi kwa hasa katika kuwa matari wa mbele katika huduma kwa maskini ambaye ni sura ya Kristo anayeteseka.  Anatoa mfano wa Shemasi Laurenti, kuwa  alipoombwa na mfalme wakati ule apeleke utajiri wa jimbo na kulipa chochote ili asiuwawe, yeye alichagua  kurudi kwa maskini. Naye  Enzo Petrolino anasema changamoto ya sasa ni ile ya umaskini mpya wa sasa yaani  wahamiaji  na wakimbizi kwa ujumla kiini cha ushemasi ni kutoka na kwenda kuhudumia.

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.