2017-11-20 16:26:00

Papa kwa Polisi:Kazi ya Polisi mara nyingi haina sifa,lakini kuweni na huruma!


Jumatatu 20 Novemba 2017 Baba Mtakatifu amekutana na Viongozi na wakuu wa Polisi usalama barabarani na  Polisi usalama wa Reli ambapo  amemshukuru Mkuu wa Polisi kwa maneno ya hotuba yake. Katika hotuba yake anasema, kila mzalendo anapaswa kutoa shukrani kwa kazi yao wanayojikita kwa jina la Taifa na kwa ujumla wakihakikisha kwa njia nyingi kuzuia na kulinda usalama kwa wale ambao wanasafiri kwa njia ya barabara na treni. Dunia yetu kwa sasa imekuwa haja kubwa ya kusafiri hapa na pale lakini, ikiwa inahitaji hawali ya yote usalama wa jamii inayoendelea kuzunguka na kwa ajili ya kuhakikisha wema wa watu wake.

Baba Mtakatifu anasema lakini pamoja na  ukiukwaji wa miiko barabarani, foleni za magari, kuzui na kutoa msaada katika ajali, ni mambao yanayolazimika kukabiliana na hali halisi na zaidi kumekuwa na changamoto ya kutisha kwa ujumla. Anazitaja sababu za changamoto hizo kuwa ni ukosefu wa mfumo mzuri wa barabara, ukosefu wa wadau  wa uwekezaji katika kukarabati na kuweka njia za usalama, vilevie hata suala la  ukosefu wa uwajibikaji kwa upande wa madreva, ambao mara nyingi wanaonesha matukio mabaya ya ajali kwa mfano wa kutumia simu za mkononi wakati wakiendesha magari.

Akiwalenga Polisi wa vituo vya Reli nasema: kama ilivyo ya usalama barabarani , matendo ya Polisi yanahitaji zaidi utaalaamu wa kina, kuendeleza  uwelewa zaidi katika sheria na kazi za vifaa na teknolojia. Lakini kwa kufanya hivyo ni muhimu kuendelea kuwasiliana zaidi na watu ili kazi isiwe tu ya kutaaluma ma kutaalamu bali iliyojaa utajiri na utambuzi hawali ya yote kwa binadamu na si kwa manifaa binafsi.

Wakati operesheni zao, Baba Mtakatifu amewaonya zaidi wawe binadamu kwa maana anasema, ni muhimu wasitumie  nguvu ambazo baadaye zinasababisha vurugu. Kwa namna hiyo anasema inahitaji hekima kubwa katika ukaguzi hasa polisi kwa maana  mara nyingi waonekana kuogopwa na pia kuwa adui, badala yake anasema waonekane walinzi kwa wema wa pamoja. Lakini kwa masikitiko, anaongeza; kwa bahati mbaya tabia hiyo ndiyo imesambaratika katika baadhi ya wengi  na kuleta upinzani wa jamii na Serikali inayowawakilisha.

Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu anatoa wito akisema kuwa; kama alivyofanya kwa Kanisa zima na Jamii wakati wa mwaka wa Jubilei ya huruma 2015, nao anawashauri wawe na mtindo wa kutumia  huruma inayokwenda moja kwa moja na shughuli zao. Anaasema kwamba; huruma haina maana ya udhaifu wala kutumia nguvu. Maana yake ni kutofautisha aliye na kosa na hasiye na kosa, ambayo inaweza mwisho kuharibu maana yake. Huruma ni ule uwezo wa kujikita katika kutambua mahitaji na sababu za watu ambao wanakutana nao katika kazi zao.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.