Baba Mtakatifu anaonesha masikitiko makubwa kufuatia kifo cha Kardinali Andrea Cordero Lanza di Montezemolo, Askofu Mkuu wa mstaafu wa Kanisa Kuu la Kipapa la Mtakatifu Paulo nje ya Ukuta mjini Roma. Barua yake aliyo mtumia dada yake, Adriana Cordero Lanza di Montezemolo, Baba Mtakatifu anasema Kardinali Andrea alikuwa mtu wa Kanisa, aliyeishi kwa imani na matumaini katika kipindi chake cha maisha ya kikuhani, akitumikia Injili na Vatican. Aidha anakumbuka kazi yake ya kutume kuwakilisha ubalozi wa Vatican katika nchi nyingi kwa namna ya pekee Papua Guinea, Nikaragua, Hunduras, Uruguay , Israeli , Italia, mahali ambapo alijikita kwa upendo mkuu na hekima kwa wema wa watu, kama vile katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo.
Kardinali Andrea Cordero Lanza di Montezemolo alizaliwa huko Torino Italia tarehe
27 Agosti 1925. Tarehe 15 Oktoba 2016 Baba Mtakatifu alikwenda kumtembelea katika
nyumba ya matunzo ya Villa Betania aRoma mahali ambapo alikuwa amelazwa.
Mazishi yatafanyika tarehe 21 Novemba 2017 saa tano na nusu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu
Petro, ambapo misa itaadhimishwa na Kardinali Giovanni Battista dekano msadizi wa
Baraza la Makardinali na Baba Mtakatifu anataongoza sehemu ya mwisho ya ibada ya
mazishi. Kufuatia kifo cha Kardinali Andrea Cordero Lanza,Baraza la makardinali wanabaki
217, ambao kati yao wenye haki ya kuchagua 120 na wasio na haki ya kuchagua ni 97.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |