2017-11-20 11:17:00

Papa ameshiriki chakula na watu 1,500 katika ukumbi wa Paulo VI Vatican!


Mara baada ya sala ya malaika wa Bwana na ujumbe mbalimbali kwa mahujaji, Baba Mtakatifu alielekea moja kwa moja katika Ukumbi wa Mwenyeheri Paulo VI ili kuweza kushiriki chakula cha sikukuu na watu 1,500 wahitaji, wasiokuwa na makazi na maskini, waliosindikizwa na wahudumu wa kujitolea kutoka vyama, mashirika na taasisi kutoka duniani kote. Sambamba na hiyo katika Jimbo lote la Roma na majimbo yote ya Italia  kwenye vituo mbalimbali vya parokia walifanya tukio kama hilo la kutoa chakula cha pamoja katika sikukuu ya Maskini duniani 2017.

Mara baada ya Baba Mtakatifu kuingia katika ukumbi ilifuatia salam ya Kardinali Rino Fischella, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya kuhamasisha Uinjilishaji mpya na baadaye Baba Mtakatifu  FRancisko alitoa salam fupi na kuongoza  sala ya chakula.

Katika maneno yake ya kuwakaribisha wote amesema: “karibunyi nyote na kujiandaa  muda huu pamoja: kila mmoja katika moyo wake amejaa utashi mwema na urafiki kati ya wengine ili kushiriki chakula cha mchana na kutakiana mema mmoja na mwingine. Kwa njia hiyo tusali kwa Bwana ili abariki chakula hiki, abariki wale waliokiandaa , abariki sisi sote, abariki mioyo yetu, familia zetu, matamanio yetu, maisha yetu na kutupatia afya na nguvu Amina”. Vilevile  ameongeza kusema: “baraka hizi ziwaendee hata watu wote ambao wanashiriki meza ya chakula katika vituo  vingineza vya Roma sambamba na hiki, maana leo hii Roma vituo hivyo vimejaa: tuwapigie makofi ya kuwashangilia tukiwa hapa……..”

Ikumbukwe kwamba, kutokana na tukio hili la Siku ya Maskini Duniani 2017, Baraza la Kipapa kwa ajili ya Uinjilishi waliandaa tukio moja muhimu la kuwakaribisha  zaidi ya watu 4,000 wenye shida na maskini ambao walisindikizwa na watu mbalimbali  kutoka vyama vya kujitolea vya  mkoa wa Lazio nchini Italia na hata katika majimbo mengine ya dunia kama vile  kutoka miji ya ufaransa (Paris, Lione, Nantes, Angers , Beauvais; Uholanzi  (Warsaw, Kraków, Solsona, Malines-Bruxelles na  Lussemburg) kufika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro ili waweze kushiriki misa ya Baba Mtakatifu Francisko kwa Siku ya Maskini duniani.

Misa iliyo iliyoanza Jumapili majira ya saa 4.00 asubuhi masaa ya Ulaya. Kutokana na wingi wao,waliwagawanya katika makundi mbalimbali. Watu 1,500 walichaguliwa kushiriki meza ya chakula katika Ukumbi wa Mwenye heri Paulo VI wakiwa pamoja na Baba Mtakatifu Francisko. Wengine  2,500 wakaganywa kwenye makundi na kupelekwa katika seminari na Taasisi za kipapa za Amerika ya Kaskazini, Taasisi ya Kipapa ya Leoniano, Kituo cha Mtakatifu Petro, Kituo cha Caritas Roma, Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, Seminari Kuu ya Kipapa Roma, na Taasisi ya Kipapa ya Regina Apostolorum ili nao washiriki meza ya chakula cha sikukuu ndiyo maana Baba Mtakatifu alitoa baraka ziwandee katika vituo hivyo wakishiriki chakula cha sikukuu hiyo.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio  Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.