2017-11-19 15:35:00

Papa awakumbusha maana ya Siku ya Maskini duniani 2017 na matukio mengine!


Mara baada ya mahubiri na sala ya malaika wa Bwana, Baba Mtakatifu amesema kuwa, Jumamosi 18 Novemba 2017 huko Detroit Marekani, ametangzwa Mwenye heri Francisko Solano, Padre wa Shirika la ndugu wadogo wafransiskani Kapuchini. Padre Francisko  Solano alikuwa mnyenyekevu na mwamifu mtume wa Kristo, ambaye alijikita kikamilifu bila kuchoka katika huduma kwa maskini. Ushuhuda wake usaidie makuhani, watawa walei kuishi furaha na uhusiano katika kutangaza Injili na Upendo kwa maskini.

Aidha amefafanua lengo la  kufanya Siku ya Maskini Dunia inayaofanyika, Roma na katika maparokia yote duniani ni kutaka kuelezea jinsi kuanzishwe mipango mingi na  madhubuti ya sala na kwa ajili ya kushirikishana. Kwa njia hiyo, ni matumaini yake kuwa inawezakana kabisa maskini wakawa ndicho kiini cha maisha ya jumuiya zote za Kikristo na siyo tu kwa kipindi hiki bali iwe mwendelezo daima wa utambuzi wa maskini,kwasababu wao ndiyo ndiyo moyo wa Injili, na  tunakutana na Yesu ndani yao ambaye anatualika na kutaka tuondoke kwenda wa wale wanaoteseka na wenye kuhitaji.

Baba Mtakatifu kuwakumbuka watu wa nchi ya Lebanon:
Pamoja na hayo Baba Mtakatifu anasema kuwa anawakumbuka kwa na namna ya pekee watu wanaoishi katika uchungu wa umaskini kutokana na vita  na migogoro. Amerudia kwa upya kutoa wito kwa jumuiya za kimataifa katika kuwajibika kwa kila njia na kujikita kwa nguvu zaidi kuhamasisha amani, kwa namna ya pekee katika nchi za Mashariki. Aidha mawazo yake pia yamewandea watu wa Taifa la Lebanon na kusali kwa ajili ya nchi hiyo ili waweza kuendelea kuwa ujumbe wa kuheshimu  na kuishi katika eneo la kanda zima na kwa ajili ya dunia nzima.

Baba Mtakatifu amekumbuka wanajeshi 44 wa Argentina waliopotea majini na Nyambizi:
Halikadhalika anamegusia juu ya  wanajeshi wa Argentina ambao wamepotea majini tangu siku ya Jumatano wiki hii na Nyambizi. Ambapo hadi sasa nchini Argentina vikosi maalumu vinaendelea kuitafuta kwani ilitoweka ikiwa na wanajeshi 44 ndani yake.

Papa kukumbusha Siku ya Kimataifa ya kuwakubuka wahanga wa ajali za barabarani: Baba Mtakatifu pia amekumbua siku ya Kimataifa ya kuwakumbuka wahanga wa ajali za barabarani, ambapo anasema, ni siku iliyoanzishwa na Umoja wa Mataifa, kwa njia hiyo anawatia moyo taasisi za umma kujikita zaidi katika kuzuia na kuwashauri madreva wawe na hekima wakati wa kuendesha magari, kwa kuheshimu sheria, ambazo ni msingi wa kwanza wa kujilinda binafsi na hata kulinda wengine.

Na mwisho:Amewasalimia wote familia, parokia, vyama na kila mwamini aliyefika kutoka pande zote za Italia na katika dunia. Kwa wote amewatakia Jumapili njema na kuwao,ba wasisahau kusali kwa ajili yake.


Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.