Jumamosi Baba Mtakatifu Francisko alikabidhi tuzo ya 17 kwa washindi watatu,wa Tuzo ya Ratzinger, akiwepo pia Kardinali Kurt Koch, mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya ukuzaji wa Umoja wa Wakristo. Washindi hao siku ya Ijumaa, walikutana na Papa Mstaafu Benedikto XVI, mjini Vatican. Washindi ni Wanateolojia Theodor Dieter Mluteri, Padre Karl Heinz Mkatoliki naArvo Part Mtunzi wa muziki Mtakatifu.
Chanzo cha habari kimeutaja mkutano wa Papa Mstaafu Benedikto XVI, na washindi hao
kwamba, mazungumzo yao yalikuwa makini na tulivu, akiwepo pia Mkuu wa Shirika la Ratzinger
Padre Federico Lombardi. Wakati wa tukio hili, lilipambwa na wimbo wa Baba Yetu, uliotungwa
na Arvo Part, mwaka 2011 kwa ajili ya adhimisho la miaka 60 ya Upadre kwa Papa Mstaafu
Benedikto XVI. Kutolewa kwa tuzo hii kwa mara ya kwanza kwa msanii , inaoneysha jinsi
Papa Mstaafu Benedikto XVI, alivyo na mapenzi kwa muziki na sanaa iliyowajongeza watu
katika ukweli na katika kukutana na Mungu.
Janeth Mhella
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |