2017-11-17 15:09:00

Papa:Ni vema kufikiria kifo maana itakuwa ni siku ya kukutana na Bwana!


Kutafakari juu ya mwisho wa dunia ambao pia ni mwisho  wa kila mmoja  ndiyo mwaliko wa wa leo kutoka katika Injili ya Mtakatifu Luka 17,26-37).  Injili ambayo Baba Mtakatifu ametafakari asubuhi ya tarehe 17 Novemba 2017 katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican. Injili inaeleza maisha ya kawaida ya watu wa kwanza kabla ya Gharika kuu la dunia na siku za Lot.  Hawa walikuwa wakila , wakinywa , wakinunua na kuuza, aidha kuoa na kuolewa, lakini baadaye ikatokea maonesho ya Mwana wa Mungu na mambo yote  yakabadilika, anasema Baba Mtakatifu.

Kanisa ni Mama na inataka kila mmoja afikirie kifo chake. Kla mmoja wetu amezoeza ukawada wa maisha yake yaani ratiba na kupanga muda,kazi,kipindi cha kupumzika na kufikiria kuwa itakuwa hivyo daima. Lakini Baba Mtakatifu anongeza, siyo hivyo kwa maana kutakuwa na wito wa Yesu ukisema njoo! Kwa wengine wito huo utakuja ghafla na kwa wengine labda baada ya siku nyingi za ugonjwa, hiyo hatujuhi !

Lakini Baba Mtakatifu anarudia, siku ipo kuitwa! Na itakuwa ni ghafla, lakini pia kutakuwa na mshangao wa Bwana ule wa maisha ya milele, ndiyo maana siku hizi Kanisa linasisitiza juu ya kufikiria kifo. Pamoja na hayo, ameonesha mifano hai hasa ile ya ukawaida wa kuudhuria mkesha wa mazishi au kwenda makaburini, kama jambo la kijamii maana ni kwenda kukutana na watu au kula ili mradi usfikirie kifo.

Kanisa leo hii kwa ukarimu wake linatamka, simama ndugu, kwa maana siku zote hazitakuwa hivyo. Siyo kufikikiria kuwa dunia hii ndiyo umilele, kwa maana kutakuwapo siku ambayo utanyakuliwa hapa duniani na kuiacha dunia hii. Ni lazima kwenda kwa Bwana na hivyo simama ufikirie kwamba kutakuwa na mwisho wa maisha haya.
Kifikiria kifo siyo jambo baya na hali halisi. Kama ni jambo baya linategemea na mtu binafsi anasema Baba Mtakatifu, lakini lazima kufikiria kuwa kifo kitakuja. Itakuwa ni siku ya kukutana na Bwana,  kwa njia hiyo kifo ni jambo zuri maana unakwenda kukutana na Bwana na yeye anakuja kukutana nawe akisema njoo mlio barikiwa na Baba yangu, njoni kwangu.

Ametoa mfano mmoja kuwa, juzi juzi amekutana na padre mmoja mwenye umri wa miaka 65 ambaye amepata habarisiyo nzuri kuhusu afya yake, alipokwenda kwa daktari alimweleza kuwa  wamekuta  kuna jambo baya, lakini labda kuna uwezekano wa kufanya kila liwezekanalo kusimamisha ugonjwa huo mbaya, lakini hata kama hawataweza kusimamisha basi daktari akasema, atamsindikiza padre huyo hadi mwisho… Baba Mtakatifu ameongeza kusema, huyo Dkt ni mwema! Na kwa njia hiyo amethibitisha, nasi tusindikizwe na njia hiyo ya kufanya kila kitu na kwa hali zote  lakini daima tukumbuke kutazama mahali tunako tazamia kwenda, yaani siku ile Bwana atakuja na kutunyakuliwa ili kuishi naye.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.