2017-11-17 15:55:00

Papa ametembelea kituo cha Afya kilichandaliwa kwa tukio la Siku ya Maskini


Baba Mtakatifu Francisko ametembelea  Kituo cha Afya katika Uwanja wa Pio XII cha madaktari kutokana na tukio la Siku ya Maskini Duniani Jumapili ijayo. Eneo hilo limeandaliwa na Baraza la Kipapa kwa ajili ya kuhamasisha Uinjilishaji Mpya. Katika kituo hiki kidogo cha afya katikati ya Roma kimeandaliwa wiki hii ili litoa  huduma ya afya  bure kwa maskini wote na wahitaji kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi za jioni masaa ya Ulaya.

Katika matembezi hayo, Baba Mtakatifu amepokaribishwa na kikundi cha maskini waliokuwa wanasubiri zamu yao ya kukutana na madaktari, ameweza kusimama na kuwasalimia na kubadilishana maneno hata matani kati yao. Pamoja na hayo Baba Mtakatifu amesikindikizwa na manesi na watu wa kujitolea wa Msalaba Mwekundu nchini Italia kutembelea kituo hiki cha afya. Amewafahamu na kuwashukuru madaktari bingwa katika mahabara mbalimbali za magonjwa kama:  ya moyo (cardiology),ya ngozi ( dermatology),ya kuambukiza( Infectology),ya akina mama (gynecology ),ya viungo vya ndani (andrology)

Aidha amewafahamu hata  watu wa kujitolea wa Shirikisho la Huruma wa kutoa msaada , ambapo  wanatoa huduma yao katika Kambi hiyo ya matibabu, kama vile walivyozoea kufanya kila wakati inapotokea kusaidia wageni, pamoja na hayo Taarifa za Vatican zinasema kuwa wamemwandalia chai ya moto Baba Mtakatifu na kunywa kutokana na baridi.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.