Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Rais wa Jamhuri ya Austria Bwana Alexander Van der Bellen katika Nyuma ya Mkutano Vatican tarehe 16 Novemba 2017. Baada ya mkutano huo pia amekutana na Kardinali Pietro Parolin Katibu akisindikizwa na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa Mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican.
Wakati wa mazungumzo yao wameonesha uhusiano mzuri na ushirikiano uliopo kati
ya Vatican na nchi ya Austria. Pamoja na hayo wamesisitiza juu ya mambo muhimu ya
maisha hasa ya ulinzi wa hadhi ya maisha ya binadamu, kuhamasha utamaduni wa makutano
na kukuza ari ya utunzaji wa mazingira.
Na mwisho wanaonesha nafasi ya Jumuiya ya Kimataifa katika kutafuta suluhisho ya amani
katika migogoro iliyopo katika kanda nyingi za dunia na kusisitiza juu ya wajibu
wa pamoja kwa ajili ya dunia ilisiyokuwa na silaha za kinyuklia.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |