2017-11-17 15:42:00

Papa amekutana na kuzungumza na Maaskofu wa Uruguay:Tangazeni Kristo


Tarehe 16 Novemba 2017 Baba Mtakatifu Francisko amewapokea na kuzungumza na Maaskofu wa Uruguay katika ukumbi wa mkutano mjini Vatican. Maaskofu wa Uruguay wako katika ziara ya Kitume Vatican kukutana na Baba Mtakatifu, ambapo ziara yao itamalizika tarehe 22 Novemba 2017. Kipindi hiki watakuwa na fursa ya kutembelea Mabaraza ya Kipapa mbalimbali kuanzia na Baraza la Kipapa la kuwatangaza Watakatifu  ili kuweza kujadili juu ya baadhi ya wenye heri na watakatifu  ktoka nchini mwako mwao ambao wako katika mchakato wa kutangazwa wenye heri au watakatifu.

Jumapili ijayo 19 Novemba 2017 Maaskofu hao watakuwa na fursa pia ya kushiriki misa na Baba Mtakatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kwa ajili ya Siku ya Maskini Duniani. Katika Mkutano na Baba Mtakatifu ameweza kusikiliza hali halisi ya Kanisa mahlia na ya nchi kwa ujumla. Hayo yamethibitishwa  na Askofu Milton Luis Tróccoli Cebedio,wa Munaziana na Kardinali Daniel Fernando Sturla Berhouet, Askofo Mkuu wa Montevideo walipohojiwa na mwandishi wa habri wa Radio Vatican.

Wote nakiri kupokelewa vizuri na Baba Mtakatifu na kujisikia kuwa nyumbani. Baba Mtakatifu ameweza kuwasikiliza kwa makini na kutaka kujua hali halisi ya nchi. Katika mazungumzo yao wamegusia juu ya  Uinjilishai kwani wanasema nchi ya Uruguay inawakilishwa hali halisi ya ulimwengu wa raia ambao wengi wao  hawana imani imani. Ni mahali ambapo Kanisa Katoliki  linawakilisha asilimia 40% tu ya watu tofauti na chi nyingine za Bara la Amerika ya Kusini  inayowakilisha wakatoliki kuanzia asilimia 80-90%.
Hata hivyo wanasema kuwa, Baba Mtakatifu amewatia moyo juu ya kuinjilisha na kutangaza Injili na zaidi ameomba maaskofu wawe makini katika kuwasaidia hasa vijana wote na zaidi wawe  karibu na vijana mapadre, kwa kuwasindikiza na kuwatia moyo na  kuwasikiliza. Vilevile Baba Mtakatifu amegusia jambo muhimu ndani ya moyo wake ya kwmba ni amani duniani, pamoja na kwamba wanasema nchi ya Uruguay haina matatizo, lakini ameomba waungane naye kusali kwa ajili ya amani  hiyo duniani.

Mwandishi wa habari amejaribu kuuliza changamoto za nchi hasa kwa upande wa  Kanisa na wakristo mbele ya sheria za nchi zinazoruhusu Eutanasia, utoaji wa mimba pia huru wa kuuza bangi. Maaskofu hao wanasema ni changamoto kubwa kwa Kanisambele ya sheria hizo, lakini pia wao wanaishi kwa mtindo wa aina mbili: kwanza ni ule wa ushuhuda wa  kueleza ukweli wa dhamiri,  kwasababu wanasema kama wakatoliki hawaweli kufanya hivyo, maana wanacho weza ni kuchanganua vizuri mada hizo nyeti. Na tabia nyingine inayo waongoza wamesema ni ile ya wasiwasi wa wakichugaji hasa katika kujikita kwenye  juhudi kubwa ya mafunzo kwa wakala au wadau wa kichugìngaji ili ili watambue wazi mantiki za kuchnganua na kusema kile ambacho kanisa inaamni, inatenda kwa kufuata mwongzo wa Mafundisho Jamii ya Kanisa. 

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.