2017-11-16 16:52:00

Ujumbe wa Papa Mstaafu Benedikto XVI kwa Mkutano wa Kimataifa


“Nikitazama ratiba ya Mkutano na mada zilizotolewa, ninatambua jinsi gani sura ya Mtakatifu Bonaventura kwa wakati huu imekuwa na utajiri mkubwa na jinsi gani yeye bado anayo mambo muhimu zaidi ya kihistoria ya kuweza  kutufundisha. Ni maandishi ya Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto wa XVI katika ujumbe kwa washiriki wa Mkutano wa Kimataifa juu ya ( “Deus Summe Cognoscribilis)Mungu Mkuu mwenye kujulikana sana kuliko vyote. Uhalisia wa Taalimungu kwa upande wa  Mtakatifu Bonaventura. Mkutano unaofanyika katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana Roma Papa Mstaafu Benedikto XVI anaongeza kuandika, uelewa wetu juu ya karne ya XIII inazidi kukua kiukweli na kujikita kwa kina hasa kwa mtazamo wa huyu  Mwalimu wa Kanisa Mtakatifu Bonaventura.

Mkutano wa kimataifa umeanza tarehe 15 na utamalizia tarehe 17 Novemba 2017 ambapo unaudhuriwa na wajumbe 48 kutoka pande mbalimbali za dunia. Tukio hili limeandaliwa kutokana na tukio la maadhimisho ya miaka 800 tangu kuzaliwa kwa Mtakatifu Bonaventura, pia inakwenda sambamba na Mikutano mikubwa ya kimataifa, ikiwa mara ya mwisho ilikuwa mwaka 1974. Lengo la Mkutano huo ni kutaka kugundua njia mbadala ambazo Mtakatifu Bonaventura alianzisha na ndiyo chachu ya kuvumbua njia hizo, kwa kufikiria ukubwa na mawazo yake, pamoja na changamoto za sasa katika tafakari la kifalsafa, kitaalimungu na kitasaufi.

Katika Mkutano huo pia wamewakilisha Kazi ya Kitabu cha Uwelewa wa maonesho na Taalimungu ya Historia ya Mtakatifu Bonaventura , kikiwa kimetafsiriwa kamili katika Lugha ya Kiitaliano na kutolewa dibaji na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI. Mkutano huo ni tunda la ushirikiano katika ya Vyuo Vikuu vya Kipapa .Chuo Kilkuu cha Kipapa Gregoriana, Taasisi ya  Mtakatifu Bonaventura na Cha Mtakatifu Antoninum. Siku ya kwanza wamejikita katika sababu za njia ya kitaalimungu na Maonesho yake. Siku ya pili ni kujikita katika Taalimungu ya Uumbaji na elimu ya Kristo (Kristologia).Siku ya tatu na ya mwisho tarehe 17 Novemba 2017 watajikita katika mada zinazotazama kwa kina mambo ya Kanisa.

Padre Federico Lombardi ambaye ni Mwenyekiti wa Chama kiitwajo Joseph Ratizinger, akieleza juu ya ujumbe wa Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto VI anasema kuwa, katika maisha yake amejifunza mengi sana muhimu hasa akiwa kijana,pia  hayo ni masomo yake ya majiundo kwa ajili ya kuweza kufundisha katika Chuo Kikuu. Vilevile aliweza kutoa hotuba nyingi juu ya Mwalimu wa Kanisa Mtakatifu Bonaventura  katika hatua zake za maisha. Na mwisho wakati wa Utume kama Baba Mtakatifu, Padre Lombardi anasema ameweza kufanya hata katekesi mara tatu juu ya Sura ya Mtakatifu Bonaventura.

Maisha ya Mtakatifu Bonaventura: Jina la ubatizo alikuwa ni Yohane Fidanza , lakini akajulikana kwa jina la Bonaventura. Alizaliwa mwaka 1218 huko Bagnoregio Italia. Akiwa mdogo aliugua sana. Lakini alipona mara baada ya kukutana na Mtakatifu Francisko wa Asizi, ambapo muda huo alitambka maneno ya Bona Bona ventura” na ndipo jina likaanzia hapo “ kwa kiswahili likiwa na maana (matukio mema).

Na tangu wakati huo jina likaendelea kujulikana Bonaventura. Aliingia katika Shirika la Ndugu wadogo Wafransiskan akiwa na nia ya kutilimilia nadhiri za mama yake. Mwaka 1257 alichaguliwa kuwa mkuu wa Shirika la Wafransiskani. Kifo chake kilitokea mwaka 1274 akiwa na umri wa miaka 56 tu. Na mwaka 1588 Papa Sisto V akamtangaza Mwalimu wa Kanisa. (Doctor Seraphicus”) Katika maisha yake, alipata kuandika sana vitabu  na zaidi anajulikana kwa kitabu chake “Itinerarium mentis in Deum” yaani safari ya akili katika Mungu. Ni kitabu kinacholeza safari ya kifalsafa, ya kitaalimungu  na fumbo inayoambatana na mtu kupitia ngazi sita ya kuweza kupaa kwa Mungu, hadi kufikia amani kamili kwa njia ya kutafakari ya kina.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.