2017-11-14 15:39:00

Salam za Rambi rambi kutoka Vatican kufuatia kifo cha Kard. Panafieu


Baba Mtakatifu Francisko ametuma salam za rambi rambi kutokana na kifo cha Kardinali Bernard Panafieu , Askofu Mkuu Mstaafu wa Marsiglia nchini Ufaransa aliye aga dunia kiwa na umri wa miaka 85. Katika Ujumbe uliotumwa kwa Askofu Mkuu wa Sasa wa Jimbo Kuu la Marsiglia Georges Pontier, Baba Mtakatifu anaonesha kuwa Askofu Mkuu Mstaafu Panafieu alikuwa mwenye hekima ya kichungaji ambaye alitambua kuonesha wema na upendo wa Mungu kwa watu ambao alikuwa amekabidhiwa. 

Zaidi Baba Mtakatifu anakumbuka shughuli zake kwamba alijikita katika hali halisi na na utofauti wa watu katika majimbo , akipeleka mchango mkubwa wa mazungumzo kati ya tamaduni na dini na kukuza hali halisi ya kuishi kwa amani kati ya wote.
Alizaliwa tarehe 26 Januari 1931 huko Châtellerault, katika Katika Jimbo Kuu la Poitiers,alipata daraja takatifu la upadre mwaka 1956 na kukabidhiwa Kanisa la Chuo Kikuu , baadaye mwaka 1974 aliteuliwa kuwa Askfo wa Tibil na msaidizi wa Annecy. Mwaka 1978 akachaguliwa kuwa  Jimbo la Aix-en  na mwaka 1995 akachaguliwa kuongoz majimbo ya Marsiglia.

Katika shughuli zake , alipewa nyadhifa mbalimbali kama kuwa mwanachama wa Baraza la Kudumu la Baraza la Maaskofu wa Ufaransa tangu mwaka 1980 hadi 1986 , mwanachama wa Kamati ya Kitume ya Ufaransa . Aidha ameongoza Tume ya Baraza la Maaskofu katika ulimwengu wa shule na Vyuo vikuu tangu mwaka 1986- 1992.

Halikadhalikwa amekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Maaskofu katika mahusiano katu ya Madhehebu ya kidini na mashirika mapya ya kidini, Mwenyekiti wa Sekretarieti ya mahusiano kati ya dini zota na ya Kiislam na Kamati ya Baraza la Maaskofu kwa utume  Katika Kanisa la Ulimwengu tangu mwaka 2006 akastaafu uaskofu  mkuu wa Jimbo la Marsiglia.

Mazishi ya Kardinali Panafieu yatafanyika tarehe 17 Novemba 2017  saa 9.00 alasiri katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu Marsiglia. Kutokana na kifo chake , Baraza la Makardinali linapungua idadi na kubaki Makardinali 218 ambo kati yao 130 wanaweza kuchaguliwa na 89 hawawezi kuchaguliwa.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.