2017-11-13 16:15:00

Yesu anasema:Ole wake anayekwaza walio wadogo ingefaa jiwe shingoni!


Makwazo  yanaumiza mioyo na kuua matumaini na kutatisha tamaa. Ni mambo makuu yaliyo ongoza Baba Mtakatifu Francisko katika tafakari ya Mahubiri yake siku ya  Jumatatu asubuhi 13 Novemba 2017 kwenye misa katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta mjini Vatican.  Baba Mtakatifu anasema, siyo rahisi kuzuia makwazo hayo na hasa akitazama Injili ya Yesu anapotoa wito juu ya wale wanaosababisha makwazo hayo na kuwaambia kuwa “ ole wa yule anayesabababisha kwa maana ingemfaa zaidi mtu huyo jiwe la kusaga linafungwa shingoni mwake  na akatupwe baharini kuliko kumkosea mmojawapo wa wadogo hawa, kwa njia hiyo Yesu anasisitiza mitume wake wajilinde wao wenyewe.

Akifafanua juu ya wito wa Yesu anasema, hiyo ina maana ya kuwa makini na siyo kuwakwaza walio wadogo. Kwa maana kukwaza ni tabia mbaya  maana inaumiza wengi, waathirika, watu wa Mungu na wadhaifu wa Mungu ambao mara nyingi wanapata majeraha hadi maisha yao yote. Aidha anasema, siyo kuleta majeraha tu bali hata makwazo hayo yana uwezo wa kuua, kwa maana yanaua matumaini, yanaua kwa njia ya kukatisha tamaa, yanaua familia,  hata mioyo ya wengi wana wa Mungu.

Jilindeni wenyewe,  ni wito kwa wote,anasisitiza  hasa kwa wale wanaojiita wakristo wakati mwenendo wao ni wapagani,  hiyo ndiyo kashfa ya watu wa Mungu. Ni wakristo wangapi wanakwenda zao mbali na Kanisa kutokana  ya ukosfu wa ushuhuda thabiti wa kuishi kikristo. Uthabiti wa kikristo ni moja ya ngao rahisi ya kudhoofisha nguvu ya shetani inayosababisha kudhoofisha watu wa Mungu  waweze kukaribia Bwana wao. Udhaifu huo umesabaisha watu kusema jambo fulani lakini wanatenda kinyume. Ukosefu wa kuishi kwa dhati na utofauti  ndiyo kashfa ambayo leo hii tunapaswa kujiuliza wenyewe jinsi ganitunaishi  udhati wa maisha ya kikirsto ? je ninaishi kulingana na maelekezo ya Injili na Bwana? 

Katika kufafanua hilo ametoa mfano wa wakristo wajasiriamali ambao hawawalipi kile kinachostahili kwa kazi ya wafanyakazi wao wanao watumikia ili wao wajitajirishe wenyewe… aidha ameongeza mfano mwengine wa kashfa za wachungaji wa Makanisa wasio chunga na kujali vema kondoo wake hadi kondoo hao wanakwenda mbali na zizi lao.

Baba Mtakatifu anasema, Yesu anasema huwezi kutumikia mabwana wawili, Mungu na fedha, na kama mchungaji ameshilikia fedha ni kashfa.Watu wengi  wanakwazika na kusema mchungaji kashikilia mambo ya kifedha, kwa njia hiyo kila mchungaji wa Kanisa lazima kujiuliza uhusiano wake na fedha; au nchungaji anayekwenda nyuma ya ubatili hadi kumfikisha kuwa na kiburi, badala ya kuwa mnyenyekevu na mpole kwa maana unyenyekevu na upole vinasaidia kuwakaribia watu wa Mungu. Baba Mtakatifu anaongeza kutoa uìonyo kwa wachungaji wanaojisikia Bwana na kuamrisha wote  au kuwa mwenye  kiburi na siyo mchungaji na mhudumu wa watu wa Mungu.

Baba Mtakatifu amemalizia mahubiri yake akisitiza kuwa leo hii ni siku nzuri ya kujitafiti dhamiri kwa kutazama makwazno hayo na kashfa ili kuweza kujibu kwa Bwana na kuwakaribia watu wa Mungu kidogo lakini zaidi kumkaribia Mungu Baba!

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.