2017-11-11 16:59:00

Upendo kati ya Mke na Mme ni moja ya uzoefu wa kuzaa matunda mema!


“Ninawasilimieni ninyi nyote mnao shiriki katika Mkutano wa Tatu wa Kimataifa juu ya Wosia wa Kitume wa Amoris Laetitia yaani furaha ya Upendo, Mkutano ulio andaliwa na Ofisi ya Kichungaji ya Familia ya Baraza la Maaskofu wa Italia”. Ni maneno aliyo anza nayo Baba Mtakatifu Francisko kwa njia ya Video, Jumamosi 11 Novemba 2017 kwa washiriki wa Mkutano wa Tatu wa Kimataifa juu ya Wosia  wa Baba Mtakatifu Francisko Amoris Laetitia yaani wa Furaha ya Upendo ndani ya familia.

Baba Mtakatifu anasema, Kauli mbiu waliyochagua kuongoza katika  Mkutano wao inasema “Injili ya Upendo kati ya dhamiri na Kawaida”  kwamba, ni yenye umuhimu na  ambayo inaweza kuangaza mchakato mzima, ambao Kanisa la Italia linaendelea kujikita  na ambao unajibu shahuku  nyingi za dharura ndani ya mioyo ya kizazi endelevu cha vijana. Upendo kati ya mke na mme ni moja ya uzoefu wa kibinadamu unao toa matunda na kuwa chachu ya utamaduni wa makutano ambayo katika ulimwengu wa sasa  una kiu na unahitajika kama dawa ya kijamii. Ki ukweli ni kwa wema wa familia ambayo kwa dhati inatazama ulimwengu ujao na kwa Kanisa.

Familia inatokana na muungano wa wanadoa na kutengeneza urafiki wa ndani ambao unatoa nguvu zaidi katika safari ya upendo wa wana ndoa. Na maisha ya kifamilia  yanajionesha kwa misingi mikuu ya dhati na kukabiliana na dhamiri kwa busara  katika pande zote mbili. Baba Mtakatifu anasema, ni muhimu kutambua kuwa wanandoa  na wazazi wasiachwe peke yao, bali wasindikizwa kwa kufuata Injili na udhati wa maisha. Kwa upande mwingiine sisi sote tunatambua  wazi kuwa, tunaalikwa kuunda dhamiri na siyo kujidai kuiondoa dhamiri nyoofu : kwasababu iwapo unaiondoa dhamiri hiyo nyoofu ni "uchafuzi wa mazingira" ambayo hupunguza roho na huchanganya mawazo na mioyo na  kuzalisha udanganyifu na uwongo.

Baba Mtakatifu anaoonesha athari za ulimwengu kuhusu suala hili na kusema; ipo hatari ya ulimwengu wa sasa kuchanganya msingi wa dhamiri ambao daima imekuwa ikiheshimiwa na kujitosheleza kila mmoja kulingana na mahusiano ambayo anaishi mtu. Baba Mtakatifu anaongeza kusema kuwa, kama alivyokuwa amesema hivi karibuni  katika Mkutano wa Elimu ya Sayansi na Maisha, kuna wale ambao hata wanasema kujionyesha  hasa hali ya ubinafsi,  kwani ni utamaduni hasa wa watu kuongozwa na ubinafsi, ambao wako radhi  wako radhi  kutoa kafara ya kila kitu ikiwa ni pamoja na wapendwa wao muhimu. 

Mtazamo huo ni mbaya kwani unaunda sura ambayo inaonekana daima katika kioo, mpaka kufikia kushindwa kuegeuza  macho yao kwa wengine na ulimwengu na  kuenea kwa mtazamo huu unaleta  madhara makubwa kwa maslahi yote na mahusiano ya maisha. 
Akitumia Maneno ya Mtunzi mmoja wa Kitabu Romano Guardini, juu ya mada ya dhamiri na hasa njia ya kuutafuta wema, Baba Mtakatifu anaongeza kusema kila ndani ya kina cha moyo wa mtu, ipo nafasi ya fumbo ambayo hujionesha na kuangaza mtu ili aweze kuwa  kuongozi wa historia yake.  Na Mkutano wa Mtaguso wa Pili wa Vatican, unaandika kuwa, hiyo ndiyo kiini cha siri na utakatifu wa binadamu mahali ambapo ni Mungu peke yake anafika katika undani huo.

Kama mkristo kazi yake ni kukesha ili aina hii ya tabenakulo isiweze kukosa  neema ya Mungu ambayo inaangaza na kutoa upendo wa wana ndoa  katika kujikita na utume na kama wazazi. Neema hiyo inajaza chungu cha mioyo ya binadamu kwa uwezo wa zawadi ya kiajabu ya  kubadili familia ya leo  kugeuka muujiza wa arusi ya Kana.

Baba Mtakatifu anaongeza kusema, moja ya tafakari aliyowahi kufanya juu ya Arusi  ya Kana anasema alipata kusema kuwa, kubadilika kwa maji kuwa divai katika vungu vilivyokuwa vikutumiwa na usafi wa Wayahudi  kama desturi, Yesu alitimiza ishara ya kiajabu, kwani alibadili sheria ya Musa katika Injili, na kuleta furaha. Kwa namna hiyo Yesu alionesha dawa ya huruma inayoponya ugumu wa mioyo na kuponya uhusiano kati ya mume na mke, kati ya wazazi na watoto.

Amemalizia Baba Mtakatifu Francisko ujumbe wake kwa njia ya Video akiwatakia mafanikio mema ya Mkutano huo na kwamba wanaweza kusaidia Kanisa la Italia liweze kufanana na kuendeleza zaidi mantiki na mtindo wa Amoris Laetitia( Furaha ya upendo ndani ya familia ; wanaweza kuchangia kuunda viongozi wa makundi ya familia katika parokia na katika vyama vya kitume: wanaweza kusaidia mchakato wa safari ya familia nyingi na kuwasaidia waishi furaha ya Injili  aidha kuwa kiini hai cha Jumuiya.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahli ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.