2017-11-11 16:22:00

Papa Francisko amekutana na Rais wa Sierra Leone Bw.E Bai Koroma


Jumamosi asubuhi ya Tarehe 11 Novemba 2017, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na kuzungumza mjini Vatican Rais wa Jamhuri ya Sierra Leone, Bwana Ernest Bai Koroma na mara baada mkutano na Baba Mtaktifu pia   amekutana na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican.

Katika mazungumzo yao wameonesha furaha kuhusu uhusiano mwema na  mshikamano  ulipo baina ya Vatican na nchi ya  Sierra Leone na umuhimu wa mchango wa Kanisa Katoliki  unatoa  kwa namna ya pekee wa  vifaa nyenzo, na kimaadili katika nchi  hiyo kwa upande wa elimu, kijamii na Afya.
Aidha wamejadili juu ya uhuru wa kidini amani na heshima ya pamoja kati  ya makundi yote mawili. Wamasisitiza juu ya umuhimu wa kukuza na kuonesha ushirikiano wa kitaifa, katika kukuza utajiri wa historia ya  mila na desturi mbalimbali za nchi, dini, utamaduni wa nchi na kuheshimu haki za binadamu na haki za madhehebu ya walio wachache.

Mwisho hawakukosa kubadlishana kama kawaida zawadi zenye kulenga  mada mbalimbali husika kimataifa kwa namna ya pekee inayo husu changamoto ya kanda ya nchi hiyo. 

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya kiswahili ya Radio Vatican

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.