2017-11-10 09:54:00

Wito wa pamoja wa SECAM na COMECE kwa Wakuu wa Umoja wa Afrika na Ulaya!


"Tunaomba haki na usawa katika biashara ya bidhaa na huduma, lakini hasa kuhusiana na rasilimali za asili, ambazo huchukuliwa kila mwaka kutoka Afrika. Ni maneno yanayothibitishwa na Maaskofu wa Afrika na Ulaya katika Waraka wa pamoja wa Tume ya Mabaraza ya Maaskofu wa Jumuiya ya Ulaya (Comece).

Mkutano wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika na Madagascar, SECAM uliochapishwa na kutangazwa kwa mtazamo wa Mkutano wa Wakuu wa Umoja wa  Afrika na Umoja wa Ulaya utakaofunguliwa huko Abidjan nchini Ivory Coast tarehe 28-29 Novemba 2017.
Maaskofu wanaomba wahusika wa Kisiasa wa Afrika na Ulaya kushirikiana kwa pamoja ili kuwapa maisha ya wakati ujao vijana wa Afrika kwa njia ya kuunda fursa za ajira kulingana na maendeleo endelevu yanayo heshimu mazingira.

Maaskofu katika Waraka wao wanasititiza  kuwa, vijana wa Afrika ni waathiriwa wa biashara ya binadamu, kwa njia hiyo, ni mategemeo yao kuwa, washiriki wa Mkutano huo, wanaweza kujikita kwa undani zaidi kupambanua mada hiyo juu ya wahamiaji na hasa mapambano dhidi ya biashara ya binadamu. Zaidi ni mategemeo yao kwamba, Umoja wa Ulaya unaweza kujikita  zaidi katika mipango ya maendeleo endelevu kutokana na  fursa hiyo ya Mkutano na wakuu wa nchi za Afrika.

Waraka huo unaendelea kuseleza, mapambano  dhidi ya biashara ya binadamu inaweza kukatishwa iwapo wataweza kuwapa vijana wa Afrika uwezo wa kujiendeleza katika maisha yao na bara lao. Mipango mipya hasa ya ufunguzi wa viwanda vidogovidogo mahalia na maendeleo endelevu ya kilimo yanaweza kupunguza athari hizi na kuwa chachu ya kupenda nchi zao kuliko  wasukuma vijana kuacha nchi walikozaliwa. Aidha inaweza kupunguza matukio yanayo tambulikana kama ( ndoto za abuanuasi) ! wanathibitisha maaskofu hao. Kwa maana moja ya mantiki ya mawazo  ya viana kutka kukumbilia nchi za Ulaya na kusababisha umasikini wa Mataifa ya Afrika.

Kwa mujibu wa Ripoti ya mwaka ya Benki ya Dunia ya mwaka 1914, inasaema, kati ya mwaka 1980 na 2010, waliofika Ulaya kutoka Afrika walikuwa  ni milioni 30,9 za watu karibia  asilimia 3% wa watu wote Afrika. Kati ya hawa wapo  wanadiplomasia na wenye  digrii. Na kwa mujibu wa Shirika la wahamiaji duniani (OIM) , linasema kati ya wahamiaji wanaongia Ulaya kwa kwa uhalali, ni 20,000 kwa mwaka na kati yao, wapo madaktari, maprofesa wa vyuo vikuu, na wataalam wengine ambao wanaacha Afrika kila mwaka tangu mwaka 1990.

Ili kuchukua nafasi ya utaalamu huo uliopotea, mashirika ya kimataifa hutumia dola bilioni 4 kwa mwaka ili kuajiri wafanyakazi huko Afrika kutoka Ulaya na Amerika Kaskazini. Ni matumaini ya maaskofu wa bara  zote mbili. Kwamba katika nafasi na  picha hii wanaweza kupitisha sera zinazowawezesha Waafrika kuendeleza bara lao wenyewe kwa ushirikiano kati ya Bara la  Afrika na Ulaya. 

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 
All the contents on this site are copyrighted ©.