Ni historia ya ufisadi wa kila siku, inayoelezwa katika Injili ya Mtakatifu Luka akionesha tajiri aliyekuwa na wakili wake akatapanya mali zake na baada ya kugunduliwa, badala ya kutafuta kazi ya halali, anaendelea kuiba kwa kutumia ujanja kwa wengine. Baba Mtakatifu anaongeza huo ndiyo tunaita kweli ufisadi !
Hayo ni mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Misa ya asubuhi Ijumaa tarehe 10 Novemba 2017 katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican. Baba Mtakatifu akiendelea na mahubiri yake anasema, hawa ni wenye madaraka wanaoendeleza ufisasi hadi kuwa na tabia za kialifu. Hii ni historia ya halisi na siyo liwaya. Siyo historia ya kutafuta katika vitabu vya kizamani vya kihistori, maana inapatikana kila siku katika magazeti. Haya yanatokea leo hii na hasa kwa walio na madaraka na usimamizi wa mali za watu, siyo kwa mali binafsi. Hakuna anayefanya ufisadi mali binafsi badala yake ni kuitetea, kuilinda mali zao binafsi!
Katika Injili Yesu anatambua wakili mdhalimu na kusema kuwa kuwa, „wana wa ulimwengu
huu katika kizazi chao wenyewe huwa na busara kuliko wana wa nuru”: Baba Mtakatifu
anaongeza, huo ni katika ufisadi wao mkubwa, ulaghai wao wa kuelendeleza mbele wakijidai
na utafadhali ambao unajitokeza kiujanja ujanja tu… je kwa namna hiyo unaweza kuitwa
udhalimu wa kikristo?
Lakini kama hawa ni wadhalimu zaidi ya wakristo, hatuwezi kusema kuwa ni wakristo
kwasababu hata mafisadi wengi wanadai ni wakristo, je udhalimu unaingilianaje na imani
na Kristo?
Baba Mtakatifu anaendelea na maswali mengi wakati huo akitafakari tafakatri na kusema, zipo tabia za watu wanaotaka kumfuata Yesu, ili hatimaye wasishie kuliwa wakiwa wazima , kama alivyokuwa akisema hata mama yake wakati akiwa mdogo kwamba „kuwatafuna wakiwa wabichi wengine”. Je ni udhalimu gani wa kikristo ambao hautaishia katika dhambi? Pamoja na kwamba wapo wengine wanafanya ujanja kila siku wakati wanajiitia wakristo. Akifafanua zaidi, Baba Mtakatifu anaonesha mifano zaidi, hata Yesu alikuwa anawatambua wakristo wadhalimu, na ndiyo maana katika Injili pia inaeleza juu ya wakristo kuwa makini na "mbwa mwitu na kondoo” au busara kama "nyoka na rahisi kama "jiwa” . Kutokana na mifano hiyo je tufanye nini ?
Baba Mtakatifu ameelezea tabia tatu za kuishi kikristo ili kuepukana na udhalimu wa namna hiyo: kwanza kuishi na imani thabiti yaani kuwa makini dhini ya walaghai wanaokuja wakiahidi uwekezaji wa banki, ili baadaye upate faida mara mbili.
Tabia ya pili anasema, ni ile ya kutafakari mbele ya ulaghai wa shetani anayetambua
madhaifu yetu na mwisho tabia ya tatu ni ile ya sala.
Amemalizia akiomba Bwana atujalie neema ya kuwa na busara ya kikristo na kuondokana
na udhalimu. Kwa maana ndani ya Maisha ya Mkristo anahifadhi tunu msingi ambayo ni
Roho Mtakatifu. Hivyo ni lazima kutunza, la sivyo wajinga wanaibiwa roho hiyo. Mkristo
yoyote hasiache aibiwe Roho hiyo na kuruhus kuwa mpumbavu.
Injiili pia ya leo iwe fursa ya kuwaombea hata mafisadi wote. Kwa maana anasema mara nyingi wanazungumza juu ya uchafuzi wa mazingira, lakini hakuna kitu kibaya zaidi pia ya uchafuzi wa jamii utokanao na ufisadi , hivyo amesisitiza kusali zaidi kwa ajili ya hao mafisadi waliofungwa katika gereza la ufisadi walioruhusu wenyewe kuingia.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |