2017-11-09 16:35:00

Wakristo tujenga,tulinde na kutakasa Kanisa ambalo ni Jiwe Msingi!


Ujenzi wa Kanisa, kulinda Kanisa na kutakasa Kanisa. ni mada tatu ambazo zimejikita katika tafakari la Baba Mtakatifu Francisko Francisko, wakati wa Misa ya Asubuhi kwenye  Kanisa la Mtakatifu Martha Mjini Vatican tarehe 9 Novemba 2017, wakati Mama Kanisa  kiutamaduni anaadhimisha sikukuu ya kutabarukwa kwa  Kanisa Kuu la Roma (Laterano )ambalo ni Kanisa la Mtakatifu Yohane mjini Roma. Ni mama wa Makanisa yote ulimwenguni, Baba Mtakatifu anasema, na hiyo ni sifa yenye maana sana japokuwa siyo  kujivuna tu bali ni katika huduma na upendo.

Akianza na mada ya kwamnza, anasema, hawali ya yote kujenga Kanisa ikiwa na msingi upi . Haiwezekani ukawa tofauti nau le wa Yesu kwasababu yeye ni Jiwe la pembeni, ambalo linajenga Kanisa hilo. Bila Kristo hakuna Kanisa, kwa maana hakuna msingi thabiti.Tunapojenga Kanisa kwa kufikiria mambo mengine  tu bila msingi wake, Kanisa hilo lazima  lieanguke, Baba Mtakatifu anathibitisha.Iwapo hakuna Yesu Kristo aliye hai katika Kanisa, lazima linaanguka!

Sisi ni mawe hai, ambayo hayafanani kwasababu ya utofauti wake tulio nao, lakini utofauti huo ndiyo utajiri wa Kanisa. Kila mmoja wetu na kwa mujibu wa zawadi aliyopewa na Mungu tunajenga Kanisa hai. Hatuwezi kufikiria kamwe Kanisa linalofanana  kama sale ya shule laha hasaha…  kwa maana hilo siyo Kanisa hai! Kwa maana Kanisa linaundwa na sisitulio tofauti nam abo tumejaliwa zawadi na karama mbalimbali katika kujenga Kanisa hai la Kristo, anathibitisha Baba Mtakatifu. Kwa njia hiyo anaongeza, kutunza Kanisa wajibu wa  kuwa na utambuzi wa Roho wa Mungu anayeishi ndani mwetu.

Ni wakristo wangapi leo hii wanaishi na Yesu wakitambua ni kuwa ni Baba na siyo tu kwa kusali sala ya Baba yetu? Aidha ni wangapi wanatambua juu ya roho Mtakatifu, badala ya kusema kuwa ni ile njiwa na kuishia hapo? Ni lazmia kufahamu kuwa Roho Mtakatifu ni Maisha ya Kanisa, Roho Mtakatifu ni maisha yako na ya kwake pia! Hivyo sisi wote  ni ekalu la Roho Mtakatifu na tunapaswa kutunza vema Roho Mtakatifu ambaye Mtakatifu Paulo, alidiriki kushauri  wakristo wake kwamba, angalieni wasifadhaishe Roho Mtakatifu, kwa maana ya kwamba wasiwe na maisha tofauti yanayoendana na maongozi ya Roho Mtakatifu ndani mwao na katika Kanisa. Yeye ni mleta umoja katika Ekalu hilo.

Na mwisho Baba Mtakatifu Akifafanua juu ya kutakasa  Kanisa  anasema,  hiyo lazima ianzie ndani mwetu, kwa maana sisi sote ni wadhambi. Na iwapo kuna asiyekuwa na dhambi, anyoshe  mikono yake , kwa maana inawezekana ikawa ndiyo utukuta wa kutaka kutambua zaidi juu yake anavyoishi bila dhambi! Lakini zaidi tunatambua kuwa sisi wote ni wadhambi, tunahitaji utakaso na  kujitakasa daima katika utakaso wa Yesu Mwenyewe. Hiyo ni pamoja na jumuiya nzima kama vile ya Jimbo, Jumuiya za wakristo, jumuiya za Kanisa la  ulimwengu mzima ili kuweza kukua vema katika imani.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.