2017-11-09 12:50:00

Askofu Mkuu P.Rugambwa amekuwa Katibu wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Protase Rugambwa kuwa Katibu wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu. Askofu mkuu Rugambwa alizaliwa tarehe 31 Mei 1960 huko Bunena-Bukoba nchini Tanzania, akapata Daraja ya Upadre kutoka kwa Papa Yohane Paulo II alipotembelea Tanzania tarehe 2 Septemba 1990 na kuwa padre wa jimbo la Rulenge nchini Tanzania.

Tarehe 18 Januari 2008 aliteuliwa kuwa Askofu wa jimbo la Kigoma, na Juni 2012 aliteuliwa kuwa Katibu Mwambata wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu na Rais wa Mashirika ya Kipapa ya Kimisionari.

Aidha Baba Mtakatifu kamteua Monsinyo Giovanni Pietro Dal Toso kuwa Katibu Mwambata wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu. 

Na Padre Celestine Nyanda 
Idhaa ya Kiswahili, Radio vatican.  








All the contents on this site are copyrighted ©.