2017-11-08 15:49:00

Papa ameanza Katekesi mpya kuhusu "Ekaristi" Moyo wa Kanisa!


Tunaanza leo  hii mfululizo mpya wa Katekesi ambao utajikita juu ya mtazamo wa “moyo wa Kanisa”, kwa maana ya Ekaristi. Ni msingi kwa wakristo wote kutambua vema thamani na  maana ya Misa takatifu ili kuishi daima na ujazo kamili katika mahusiano yetu na Mungu. Ni maneno ya Baba Mtaksifu Francisko, aliyo anza nayo wakati wa tafakari ya Katekesi ya Jumatano tarehe 8 Novemba 2017 Mjini Vatican. Tafakari mpya kuhusa Moyo wa Kanisa, inafuata mfululizo wa katekesi iliyopita juu ya matumaini ya Mkristo iliyo malizika jumatano iliyopita.

Baba Mtakatifu anaendelea na tafakari akisema; hatuwezi kusahau kuwa sehemu kubwa ya wakristo duniani kote katika miaka 2,000 ya historia , wamevumilia hadi mauti kwa ajili ya kutetea Ekaristi Takatifu. Ni wangapi hata leo hii wanaharatisha maisha yao kwa kuudhuria Misa za kila Jumapili.
Mnamo mwaka 304 wakati Kanisa linateswa na mtawala wa kirumi Dioclazian , kikundi cha wakristo wa Afrika Kaskazini walikutwa wanasali Misa kwa siri katika nyumba na kukamatwa. Mkuu wa Kirumi alipowauliza kwanini wanafanya hivyo wakati wamekatazwa kabisa, wao wakajibu, “bila Jumapili  hatuwezi kuishi”

Baba Mtakatifu anaongeza, anachotaka kusema ni kwamba iwapo hatuadhimishi Misa Takatifu hatuwezi kushi, kwa sababu maisha yetu ya kikristo yanaweza kufa. Na kwa hakika Yesu aliwambia mitume wake, usipokula mwili wa mwana wa Binadamu na kunywa damu yake, hamtaishi. Aulaye mwili wangu na kunywa damu yangu ataishi milele na nitamfufua siku ya mwili.( Yh 6,53-54). Wakristo hawa wa Afrika ya Kaskazini, Baba Mtakatifu anabaisha zaidi, waliuwawa kwa sababu ya kuadhimisha Misa takatifu. Waliacha mfano kwamba inawezekana kujikana maisha hapa duniani kwa ajili ya Ekaristi, kwani Ekaristi ni kujitoa maisha ya milele na kutufanya kushiriki ushindi wa Kristo dhidi ya Kifo. Ushuhuda huo unatualika kila mmoja, pia kutaka jibu la maana kwa kila  anayeshiriki sadaka ya Misa na kujongea Karamu ya Bwana.

Baba Mtakatifu ameuliza swali iwapo wanatafuta chemi chemi ya maji hai kwa ajili ya maisha ambayao yanatuwezesha kuwa na maisha ya kiroho katika sadaka ya sifa na shukrani kwenye misa takatifu na zaidi, ndiyo maana ya kushukuru, yaani Ekaristi maana yake ni shukrani. Baba Mtakatifu anafafanua hiyo ina maana ya kushukuru Mungu Baba, Roho Mtakatifu anaye badili kuwa katika umoja wa upendo. Kadhalika Baba Mtakatifu anasema, katika katekesi zijazo atapendelea kutoa baadhi ya majibu yatokanayo na maswali muhimu kuhusu Ekaristi na Misa, ili kuweza kugundua kwa upya ile  njia ya fumbo la imani inayoangaza upendo wa Mungu. Mkutano wa Mtaguso wa II wa Vatican ulijikita zaidi katika shahuku ya kutaka kuwapelekea wakristo watambue ukubwa wa imani na uzuri wa kukutana na Kristo. Kwa njia hiyo ilikuwa ni muhimu hawali ya yote kujikita katika matendo kwa maongozi ya Roho Mtakatifu na kufanya mabadiliko ya liturujia ya  dhati ili Kanisa liweze kuishi  mageuzi mapya.

Kiini cha mada ambayo Mababa wa Mtaguso walichosisitiza ni mafunzo ya kiliturujia kwa waamini na uwajibikaji wa mabadiliko ya kweli. Na ndiyo hata lengo la mwendelezo wa Katekesi hii inayoanza leo hii, Baba Mtakatifuamethibitisha, ili kuweza kukua katika utambuzi yakini wa ukuu wa zawadi ya Mungu anayoitoa katika Ekaristi. Ekaristi ni tukio la mshangao ambao Yesu Kristo anakuwapo daima katika yetu. Kudhuria misa ni kufanya uzoefu wa upendo na kifo cha Ukombozi wa Bwana. Baba Mtakatifu anasema hiyo ni “Epifania”  maana yake maonesho: Maana Bwana anakuwapo altareni kwa ajili ya kujitoa kwa Baba yake, kwa ajili ya ukombozi wa dunia. (Maneno ya mojawapo ya mahubiri yake ya kila asubuhi Katika kanisa la Mtakatifu Marta tarehe 10 Februri 2014).

Akiendelea kutoa mfano juu ya mienendo ya waamini wakati wa misa  ameongeza kusema, Yesu yupo pale na sisi lakini mara nyingi utakuta kuwa wengi tunakwenda katika misa, tunatazama mambo mengine au tunaongea kati yetu wakati padre anaadhimisha misa. Kwa njia hiyo sisi hatushiriki misa na Bwana japokuwa Bwana yuko pale mbele yetu. Anaongeza kutoa mfano fikirieni kama  leo hii anakuja rais  wa Serikali, au   mtu yoyote maarufu duniani;  ni uhakika kwamba wote watakuwa makini kusikiliza na kutaka kuwa karibu naye au kutaka kila mmoja kumsalimia.

Lakini  unapokwenda katika misa, yupo Bwana ambaye ni mkuu wa  wote ni maarufu wa wote, bali akili iko mbali na kufikiria mengine au kuzungumza, au kuzunguka huku na kule. Mfano mwingine Baba Mtakatifu anongeza, mara nyingi utakuta wengine wanasema misa inakera, je kweli misa inakera? Majibu hapana ni mapadre wanakera, Baba Mtkatifu anasema, basi kama wanakera waombee hao waongoke, lakini kumbukeni ya kwamba  Bwana yupo mbele ya altare na msisahau hilo. Kuudhuria misa anasisitiza tena,  ni kuishi na kufanya uzoefu wa upendo  na kifo cha ukombozi wa Bwana.

Baba Mtakatifu anasema heri kufikiria kujiuliza maswali kwa mfano kwanini inafanyika tendo la Ishara ya msalaba na sala ya kuungama kabla ya kuanza misa? Hili ni swali linalofungua mjadala mwingie: ninyi mnaona watoto wanavyo fanya ishara ya msalaba? Wakati huo nawambia hamju kufanya ishara vizuri  ya msalaba au kuchora, lakini basi kama hawajuhi wafundisheni ninyi kufanya ishara ya msalaba na ndiyo hivyo inapoanza misa, kuanza maisha na kuanza siku.

Kufanya ishara ya Msalaba: ina maana ya kwamba sisi sote tunakombolewa na msalabani na Bwana, Tazameni watoto na kuwafundisha kufanya ishara ya msalaba. Aidha maswali mengine Baba Mtakatifu amauliza, kwanini masomo yapo katika misa? Kwanini yanasomwa jumapili masomo matatu na siku nyingine masomo mawili tu? Kuna maana gani ya masomo katika Misa? Kwanini yanasomwa au kwanini hatua nyingine Padre anasema “inueni mioyo”.
Hasemi inueni simu zenu mikononi kwa ajili ya kupiga picha, jamani siyo jambo zuri! Anaongeza, kwa upande wake, anashikwa uchungu sana anapoona katika Uwanja wa Mtakatifu Petro au katika maeneo mengine akiadhimisha misa, anaona simu nyingi za mikonomi zimeashwa juu zikipiga picha na hiyo anasema, sio tabia ya waamini walei tu, bali hata baadhi ya mapadre na hata maaskofu; ni jambo baya !  anasema Baba Mtakatifu.

Kwa njia hiyo ameomba tafadhali: Misa siyo tamasha, misa ni kwenda kukutana upendo , kukutana na ufufuko wa Bwana. Na ndiyo maana Padrea anasema “Inueni mioyo” , ikiwa na maana yake? Kumbukeni siyo kuansha simu za mkononi. Baba Mtakatifu ameendelea kusisitiza kuwa ni muhimu kurudi katika msingi  ili kuweza kugundua jambo muhimu kwa njia ya kugusa na kuona katika maadhimisho ya Misa Takatifu. Swali la Mtume Thomas (Yh 20, 25) juu ya kutaka kugusa madonda ya majeraha ya misumari mwilini mwake Yesu , ni shahuku  kwa namna nyingine ya kugusa Mungu na kumwomba.Kwa maana hiyo alichokiomba Mtakatifu Tomas kwake Bwana ndicho hata siki tunahitaji, kuona, kugusa ili kuweza kutambua. Sakramenti zote zinazotolewa ni kwasababu ya mahitaji haya ya kibinadamu . Sakramenti na maadhimisho ya Ekaristi Takatifu  kwa namna ya pekee ni ishara nyingi za upendo wa Mungu , ni njia mwafaka ya kukutana naye Baba Mtakatifu anathibitisha. Kwa njia ya mfululizo wa katekesi hizi zilizo anza leo, Baba Mtakatifu anarudia kusema, anataka kuwafanya wagundue uzuri unaojificha katika maadhimisho ya Ekaristi ili mara utakapogundua uweze kuleta maana na ujazo katika maisha ya kila mmoja. Mama Maria awe msindikizaji wa njia mpya hii.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.