2017-11-07 16:12:00

Papa anawaalika waamini kutambua zawadi ya Mungu tunayopewa bure!


Iwapo hutambui neema ya bure ya mwaliko wa Mungu huwezi kutambua lolote. Mwaliko wa Bwana daima unatolewa bure. Je ili kuweza kwenda  kushiriki naye katika karamu yake unalipa nini? Tiketi ya kungia katika karamu yake ni kuwa mgonjwa, ni kuwa masikini na mdhambi. Hizi ndizo tiketi za kuweza kuingia katika karamu yake, yaani kuwa mwitaji  kiroho na hata kimwili.

Ni mahaubiri ya Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 7 Novemba 2017 katika Kikanisa cha Mtakatifu Marta Mjini Vatican, akitafakari Injili ya Siku kutoka Mtakatifu Matayo (Mt 14,15-24), Injili inaeleza juu ya  mwaliko kwenda katika karamu ya Bwana . Usipoteze uwezo wa kujisikia kupenda na kupendwa , kwa maana ukifanya hivyo ni kupoteza kila kitu. Katika Injili inaeleza kuwa “heri atakaye kula chakula cha Ufalme wa Mungu. Bwana anatoa ushauri na kumwalika  mtu ambaye hawezi kumrudishia tena mwaliko wake.

Akifafanua juu ya mwaliko wa Bwana aliyawaalika watu wengi, lakini hakuna hata mmoja anayetaka kushiriki iwe chakula au watu wengine, Baba Mtakatifu anasema kwa maana walikuwa na shughuli zao. Mwingine alikuwa na mifugo, mwingine katika shamba na mwingine alikuwa ameoa. Je hawa wangeweza kupata faida gani? Japokuwa wao walikuwa akijisumbua bure wakifanana na yule aliyekuwa amevuna mavuno mengi na kurundika katika gara lake mazao hayo lakini usiku huo akaaga dunia mara baada ya kujisifia!

Anatoa ufafanuzi zaidi kuwa, walikuwa wameshikilia mambo yao hadi mlango wa utumwa wa roho , yaani wa kutokuwa na uwezo wa kuitikia mwaliko wa Bwana. Hawa hawatambui kabisa mwaliko wa bure wa Mungu na hawatambui lolote . Pamoja na kwamba ili kuweza kuingia katika karamu ya Bwana unahitaji tiketi mwitaji kiroho na kimwili, ili uweze kupona na kuwa na upendo zaidi. Halikadhalika anafafanua juu ya tabia mbili zinazojitokeza katika Injili ya siku kwamba, ipo tabia mbili ya kwanza ni  kwa upande wa Mungu ambaye hatozi ushuru wowote, akitumia mtumishi anayewapeleke maskini, viwete , wema na wabaya. Hii ni kutaka kuonesha kuwa ni wema usio kuwa na kikomo kwa maana Mungu anapokea wote anasisitiza Baba Mtakatifu.

Kwa upande mwingine wapo walio alikwa wa kwanza lakini hawakutambua lolote juu ya wema wa bure wa Mungu . Hawa wanafanana na  Kaka yake mkuu wa Mwana mpotevu, ambaye hakutaka kwenda katika karamu aliyo andaa Baba yake mara baada ya kurudi nyumbani kwa muda mrefu. Hakufanya hivyo kwasababu hakutambua kitu juu ya zawadi ya bure ya Baba  yeke. Katika maneno yake, anasema, yeye ametumia fadha zote za urithima kufuja katika raha zake na dhambi, na  badala yake Baba wanamfanyia sikukuu, mimi ambaye ni mkatoliki, ninakwenda misa za kila Jumapili na mambo mengi inakuwaje? Baba Mtakatifu anaongeza, kwa  kufanya hivyo ni kama kutojua bado lolote juu ya ukombozi wa bure, kwa maana ni kufikiria kuwa ukombozi ni tunda binafsi na kujiokoa mwenyewe. Ninalipa mwenyewe hiki na kile Baba Mtakatifu anasisitiza, zawadi ni ya bure! iwapo wewe uingii katika mantiki hiyo basi bado hujambua lolote.

Ukombozi ni zawadi ya Mungu ambayo inajibiwa na zawadi nyingine binafsi kutoka moyoni wako, anasema Baba Mtakatifu Francisko na kusisitiza kurudia  kuwatafakari wale ambao wanapenda kurudishiwa  hasa  ambao mara  wakisikia juu ya zawadi, haraka wanafikiria kurudishiwa kwa maana wanafikiria leo hii ninatoa zawadi, kusudi kesho yake katika tukio fulani nao watanifanyia hivyo. Kwa upande wa Mungu anafafanua, siyo hivyo kwa maana hataki kurudishiwa kitu chochote zaidi ya upendo, uaminifu kama  yeye alivyo mwaminifu kwa watu wake. Anaongeza, ukombozi haununuliwi hasa yule anayeingia katika karamu  kwa maana Mungu anathibitisha “heri yule atakaye shiriki chakula cha ufalme wa Mungu, na ndiyo ukombozi!

Wale wasiojihisi kusogelea na kuingi katika karamu ya Bwana, wanajiamini, maana wanajikomboa wao binafsi nje ya meza, lakini kwa maana hiyo wanakosa zawadi ya bure ya Mungu, kukosa ule upendo na wamekosa jambo kubwa na zuri zaidi  katika maisha, kwa njia hiyo ni mbaya kutokana na kwamba wamekosa mwelekeo  na uwezo wa kujisikia kupendwa. Unapokosa uwezo wa kupenda, kwa maana ndiyo nguvu ya kujisikia unapendwa unapoteza hata matumaini na kila kitu anasema Baba Mtakatifu. Kwa njia hiyo ni lazima kufikiria maneno ya Bwana anayetuma mtumishi  kwamba “Mimi ninataka nyumba yangu ijazwe, kwa manaa ni Bwana mwenye upendo mkubwa na wa bure, yeye anataka kujaza nyumba yake. Tumwombe aweze kusaidia ili tusipoteze ule uwezo wa kujisikia kupendwa naye,  pia hata sisi kupenda.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.