2017-11-06 10:51:00

Papa amekumbuka Mwenye heri mpya wa Kanisa Sista Rani Maria Vatalil


Mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana Jumapili 05 Novemba 2017, Baba Mtakatifu amekumbuka juu ya tukio la kutangazwa mwenye heri Rani Maria Vatalil Sista wa Shirika la Waklara huko Indore India siku ya tarehe 4 Novemba 2017. Aliuwawa kwa ajili ya kutetea imani yake ya kikristo mwaka 1995, hivyo Baba Mtakatifu anaongeza kusema, Sista huyo ametoa ushuhuda wa Kristo katika upendo na upole hadi kuuungana na umati wa wafia dini wa nyakati zetu. Mtawa huyo alikuwa mwema mno, kiasi cha kumbatiza jina kuwa “sista wa tabasamu”, amesisitiza. Ni mategemeo ya Baba Mtakatifu kwamba, sadaka yake iwe mbegu ya imani, amani na hasa katika nchi ya India.

Na katika  kuelezea zaidi juu yake, naye Kardinali Amato Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya kuwatangaza wenye heri na watakatifu anasema, Sista Rani alikuwa na kiu na njaa ya haki na ndiyo maana aliuwawa tarehe 25 Februari 1995. mhalifu mmoja alimshambuliwa na kumchoma  na kisu mara 54  mwilini mwake. Sista Rai Maria alizaliwa Kerala nchini India , na kwa miaka miwili na nusu alikuwa anatoa huduma ya kichungaji huko Udaynagar katika Jimbo Katoliki  la Indore, kwenye Serikali ya Madhya Pradesh, kwa ajili ya kuwasaidia wakulima na wanawake katika vijiji. Wakati akiwa safarimi kwenya basi kuelekea Bhopal, alilazimishwa kwa nguvu kutelemka ndani ya basi mbele ya wasafiri wote, na mhalifu alimchoma kisu mwili wake.

Hiyo ndiyo ulikuwa mwisho kwa yule ambaye alitaka mabadiliko ya vijiji katika nchi ya India. Shughuli yake nyeti kwa ajili ya kusaidia maskini iliamsha hisia za chuki kwa mabwana wa eneo hili. Aidha anasema Kardinali Amato, sababu kuu ya chuki hadi kifo chake kwamba, sista alikuwa akihubiri Injili ya upendo na kuwatetea wanyonge, wale ambao kwa namna ya pekee waliokuwa wananyanyaswa na mabeberu wa ardhi. Sista Rani alitafuta kwa njia zozote kukumboa ardhi kwa  wanyonge pia kuanzisha ushirika wa mikopo midogo midogo kwa ajili ya ujasiriamali.

Kifo chake kilisababisha mivutano mikubwa mno hasa baada ya mazishi kwa maana walifanya hata maandamano ya umma kwa maelfu ya watu, kutoka katika dini mbalimbali na taasisi zote za Madhya Pradesh zilibaki zimefungwa kwa ajili ya maombolezo ya kifo chake. Hata hivyo mabadiliko ya maana yametokea mara baada mhalifu huko Gereza kukiri kosa na kutubu hadi mwisho wa mwaka 2012 alikutana na dada yake marehemu, Sista Selmy Paul wakapeana mkono wa amani. Leo hii Singh amesha maliza muda wa kukaa gerezani, kutokana na familia ya marehemu  kumwombea msamaha wa apate kuwa huru.

Hivi karibuni Gazeti la AsiaNews , linatoa ushuhuda wa dada yake Sista Selmy Paul kuwa mtu aliye muua Sista Rani Maria anaishi karibu kilometa 30 kutoka katika Comventi yao, na anakuja kila mwaka kuwatembelea, hasa katika siku ya kukumbuka kifo cha Sista Rani Maria, anafika kutoa heshima katika kaburi lake, pia  kila mwaka anatoa nusu ya ngano ya shamba lake kwa wahitaji kama ishara ya mabadiliko ya maisha. Kwa njia hiyo ni  ushuhuda hata katika kutangazwa mwenye heri Sista Rani Maria .

Kardinali Amato anasema, katika eneo la Udainagar na kwa ajili ya Kanisa Katoliki India, wamisionari wanaiga mfano mkubwa na ulinzi katika huduma yao ya changamoto kwa ajili ya wema wa wengine. Na daima wafia dini wamekuwa rutuba ya nchi kwa kizazi kipya cha kikristo. Aidha anasema,  watawa wa shirika la waklara kwa sasa wanayo furaha zaidi kuongezeka wa watakatifu , kama vile mtakatifu Alfonsa Muttathupaddathu na mwenyeheri Rani Maria Vattalil mpya!

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.