2017-11-06 16:23:00

Mons.Vigano' ameadhimisha Misa katika Ubalozi wa Italia mjini Vatican!


Katika maadhimisho haya anatusindikiza  Askofu Karoli Borromea akiwa kijana ameishi kama mchungaji na kujitolea maisha yake yote kwa ajili ya wema wa watu, akiwatetea dhidi ya wenye nguvu na ukosefu wa haki na awe mlinzi na mfano daima wa kuigwa katika shughuli zenu za kila siku.
Ni maneno aliyo anza nayo Monsinyo Dario Vigano', Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Mawasiliano Vatican wakati wa kuadhimisa Misa kwa ajili ya kumbukumbu ya Mtakatifu Caroli Borromeo tukio lilofanyika tarehe 4 Novemba, lakini Monsinyo ameathimisha tarehe 6 Novemba 2017 katika jengo linaloitwa Jina la Borromeo la Ubalozi wa Italia mjini Vatican.

Akitafakari somo la kwanza la siku kutoka katika Barua ya Mtume Paulo kwa Waroma, Monsinyo Vigano anasema, ni somo linasema ukweli ya kwamba Mungu ni mwaminifu kwa ahadi zake, ambazo zinatimia wakati wake. Alihaidi ukombozi kwa watu wote na ambao utatimilizika kwa upendo, lakini ambao tayari umeoneshwa kwa njia ya kifo cha mwanae Yesu  katika msalaba. Anatumia mojawapo maneno ya tafakari ya Baba  Mtakatifu asubuhi katika Misa zkwenye Kanisa la Mtakatifu Marta  kwamba, Bwana, anatoa ahadi yake kwa kila mmoja. Hasa ahadi ya kuitwa wana ambayo inatoa matumaini. Hiyo ndiyo njia ya ukombozi. Wote tunastahili kuwa na matumaini pamoja na kwamba, mara nyingi binadamu anataka kujiokoa binafsi.  Lakini kwa kujitambua kuwa sisi ni wana, basi tufanye tendo la kukiri imani yetu, Bwana ambaye anatukomboa.

Akifafanua juu ya Zaburi ya 94  “heri mtu unayemfunza nidhamu na kumfundisha sheria yako ili siku ya taabu apate utulivu” , anasema ni elimu ya Mungu inatangulia kuelezea Injili. Kwa maana inelekeza wazi mantiki ya Ufalme wa Mungu ambao unapitia maneno  yasemayo” atakaye jikweza mwenyewe atashushwa”. Hiyo ina maana mwenye kiburi na kujikweza hawezi kamwe kutambua nafasi ya kwanza ya Mungu kwa maana haoni sababu ya Mungu katika maisha yake na ndiyo anajikuta yuko katika nafasi tofauti na matakwa ya Mungu. Kinyume na yule anayeweka Mungu nafasi ya kwanza kwa maana  Bwana anathibithsa kuwa hawezi kamwe kukosea, maana anao utambuzi wa ukuu wa Mungu ambao Bwana pia anarudishia ukubwa huo huo katika maisha yake.

 Kwa njia hiyo Monsinyo Vigano' anasema, ni Neno linatoa mwaliko wa kutambua uaminifu wa Mungu na ahadi zake anazotoa kwa watu wake na ukuu  wa historia yake. Na kupokea ukweli huo tu hautoshi iwapo hauendani na jitihada za ushuhuda , katika kazi na wajibikaji wa kila mtu. Katika shughuli binafsi kila mmoja anapaswa kuwajibika na kujibu wito huo. Katika uwajibikaji  kwa ajili ya wema wa mtu na hadhi yake , kutambua udhaifu na ulinzi wa haki zake.Kwa kuheshimu kanuni, taasisi na kila kitengo, mahali tunapokuwa kumweka  binadamu mbele  kama mfano wa Mungu na katika kanuni ya huduma ya matendo yetu.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.