2017-11-06 13:20:00

Baba Mt.amemteua Padre Jean-Patick Iba-Ba kuwa Askofu mpya wa Francaville


Baba Mtakatifu amemteua Askofu mpya wa Jimbo la Franceville  nchini Gabon, Padre Jean-Patick Iba-Ba, ambaye hadi uteuzi huo alikuwa ni Gombera wa Seminari Kuu ya Kitaifa ya Mtakatifu Augustin” huko Libreville Gabon.  Padre Jean-Patick Iba-Ba, alizaliwa tarehe 18 Aprili 1966 huko Libreville, na kuanza shule ya msingi mnamo  mwaka 1973 - 1979  huko Port-Gentil Gabon. Aliendelea na masomo ya Sekondari  kuanzia 1979 -1989, huko Libreville. Majiundo ya upadre, alitumwa na Askofu Mkuu wake huko Seminari kuu ya Kardinali Emile Biayenda huko Brazzaville, mji Mkuu wa  Congo. Mwaka 1993-1998 aliendeleza na  masomo ya Taalimungu katika Chuo Kikuu cha Kipapa Urbaniano Roma.

Alipata daraja Takatifu la upadre tarehe 19 Julai 1999 katika Jimbo Kuu la Libreville. Na baada ya upadrisho alifanya utume mbambali kama ifuatavyo:  kama msaidizi wa Gombera katika Seminari kuu ya Mtakatifu Augustin  huko  Libreville kuanzia  1998-1999 ; Gombera wa Siminari ndogo ya Mtakatifu Jean wa  Libreville mwaka 1999-2001 na Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Michel  wa Ndjole mwaka 2001-2004.

Mwaka 2004-2009   alirudi Roma kuendelea na masomo na kupata digrii ya Sheria katika Chuo Kikuu cha Kipapa Urbaniano. Mwaka  2009-2012   kuwa makamu wa Gombera ya Seminari Kuu ya  Augustin wa  Libreville; mwaka 2010-2012   Mkurugenzi wa Shule Katoliki nchini Gabon na Msimamizi  Mkuu wa Taasisi za Elimu Katoliki. Na tangu 2012 hadi uteuzi wake amekuwa Gombera wa Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustin nchini Gabon.

 Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.